TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, December 25, 2012

WAKAZI WA MJI WA MOSHI WAITAKA SERIKALI KUBADILI MIUNDOMBINU YA MAKUTANO YA BARABARA- WATAKA ZIWEKWE TAA ZA KUONGOZA MAGARI

 Wakazi wa Mji wa Moshi Wamemtaka Waziri, Magufuli kuweka Taa za Kuongoza Magari katika makutano ya Barabara zinazoingia na kutoka katika Manspaa ya mji huo, hata hivyo kutokana na hali ya mambo kuwa tete, imebidi Jicho la Kamera ya Blog hii kumulia kwenye Barabara hizo ili kujionea hali ya Msongamano wa Magari, ambayo barabara moja katika mji wa Moshi ni kiunganishi cha Barabara tano,kitendo ambacho sasa kinaufanya mji wa Moshi kuweka Foleni ambayo itakuwa kero hapo baadae.
"kwa kweli aisee chalii hii sasa siyo yenyewe@ maana hata hapa kwa nini mkuu wetu Magufuli aisee asifanye mipango tuweze kuwekewa taa kama ambavyo sehemu zingine zinazopata maendeleo zinawekewa Taa za Kuongoza Magari@ "alisikika mtu ambye bila shaka ni mkazi wa siku nyingi katika mji wa Moshi
 Watembea kwa Miguu wakipita kwa Taabu kupisha Magari ambayo sasa yanaweka Msongamano mkubwa kutokana na kukosekana kwa Taa za Kuongoza Magari katika Mji wa Moshi.
 kuna haja sasa ya kuwekewa Taa za Kuongoza Magari Mji wa Moshi
 Foleni ikizidi kuongezeka kutokana na kutumia mfumo wa Keep left
 Magari yakisubiri foleni ya kuzunguka keepleft
Eneo hili ni kati ya Sehemu ambazo Barabara tano zinakutana kwa ajili ya kuzunguka kiplef, kitendo ambacho kinasababisha msongamano mkubwa sasa wa magari(Picha Zote na Shaaban Mpalule).

No comments:

Post a Comment