TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, June 3, 2016

SERIKALI KULICHUKULIA HATUA ZA KISHERIA GAZETI LA ECCONOMICS LA UINGEREZA KWA UPOTOSHAJI WA TAARIFA DHIDI YA SERIKALI YA UTAWALA WA AWAMU YA TANO.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimetoa Ufafanuzi kuhusu Taarifa iliyotolewa na Gazeti la kiingereza ikihusisha juu ya Utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli.kwamba Wawekezaji wa nje wameendelea kusuasua ya kuingia Madarakani ukilinganisha na Utawala wa Awamu ya nne.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo Zamaradi Kawawa, amewataka Wanahabari kutumia Kalamu zao na vyombo vya habari kuandika habari zilizo sahihi ili kuepusha upotoshwaji wa taarifa mbali mbali kwa wananchi, "ndugu zangu na wenzangu wandishi wa habari, kumekuwepo na wimbi kumbwa la vyombo na wanahabari kuandika habari za upotoshaji, kwa kweli kitendo hiki siyo kizuri na inavyoonekana ivi sasa kuna vyombo ama kama siyo watu binafsi wenye nia mbaya ya kuitakia mabaya tanzania, kama ambavyo mwandishi wa habari la Economics la nchini Uingereza alivyofanya katika taarifa yake ya kwamba Tanzania ivi sasa inayumba kwenye suala la Uwekezaji kwa wawekezaji" amesema Zamaradi. 

 Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini DAr es salaam leo Daudi Riganda amesema kuwa ni taarifa za uzushi zinazoenezwa na baadhi ya vyombo vya nje kuhusiana na kuitakia mabaya Tanzania na kwamba si kweli kuwa Wawekezaji wengi wamesitisha kuingia nchini kuwekeza.

aidha amewahakikishia watanzania kuwa takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba Tanzania mpaka sasa bado inaendelea kuwa na mahusiano mazuri na wawekezaji wengi na wanaendelea kuwapokea wawekezaji bila Ubaguzi wa aina yoyote.

Na kwamba Tanzania aina vikwazo vyovyote ilivyoviweka kwa wawekezaji kuja kuwekeza kutokana na kwamba tanzania ni nchi yenye Amani na kuhusiana na taarifa hiyo tayari Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza umetaarifiwa ili kufuatilia gazeti hilo amabapo taratibu za kisheria zinaendelea kupitia Mwanasheria wa Serikali ili kuwachulia hatua Stahiki wahusika wa Taarifa hizo za Upotoshaji dhidi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo Zamaradi Kawawa(kushoto),Meneja Uhusiano kituo cha Uwekezaji TAnzania (T.I.C) Daudi Riganda, akifafanua Taarifa ya Upotoshaji iliyoandikwa na Gazeti la Econonic na Mwanahalisi.katika Idara habari maelezo jijini Dar es Salaam leo( Picha na Raymond Urio).

  

No comments:

Post a Comment