Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (wa tano kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba (wa tano kulia),
wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka hiyo, mara baada ya
Katibu Mkuu kumaliza ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo,
jijini Dar es Salaam.
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Sunday, May 29, 2016
KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA NIDA, ATOA HABARI NJEMA KWA WATUMISHI 597 WALIOSITISHWA MIKATABA YAO
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (wa tano kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba (wa tano kulia),
wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka hiyo, mara baada ya
Katibu Mkuu kumaliza ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo,
jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (kulia) akimsalimia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, wakati alipokuwa
anawasili katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo katika Jengo la BMTL, jijini Dar
es Salaam, jana. Katika hotuba yake, Rwegasira aliwataka watumishi 597
waliositishiwa mikataba yao waondoe hofu kwani hivi karibuni Serikali
itaanza kuwalipa fedha zao baada ya taratibu chache za kiutendaji
kukamilika.
Afisa
Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Ansigar Chilemba akitoa
maelezo jinsi taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Taifa
zinavyohakikiwa, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus
Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka
hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
Afisa
Usajili Kitengo cha Ubora wa Kadi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), Jemima Mulokozi (kushoto) akimuonyesha vitambulisho
vilivyokamilika vikiwa na ubora unaohitajika, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati).
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba.
Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini
Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment