TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 1, 2016

DR MWAKA NDONDO CUP, TIMU ZOTE ZAKABIDHIWA VIFAA LEO

Timu 32 zinazoshiriki ligi ya Michuano ya Dr MWaka Ndondo Cup za jijini Dar es SAlaam, zimekabidhiwa vifaa leo katika ukumbi wa Escape uliopo maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mwaka wa Tatu sasa tangu Michuano hiyo ilipoanza chini ya Waandaji Clouds Media Group  kwa kushirikiana na DRFA ambao ni chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mwakilishi wa Clouds Media Group, Shaffi Dauda, amesema kuwa michuano hiyo imefikia hatua ya MAkundi baada ya kumalizika mzunguko na ambapo jumla ya timu 16 zilifanikiwa kuingia hatua hiyo toka mwaka jana na timu zilizobaki pia zimeweza kuingia hatua hiyo baada ya kupambana kwa udi na Uvumba hadi kufanikiwa kupata nafasi hiyo.

 Jumla ya vifaa vyenye tahamani ya Milioni 40 zimekabidhiwa ikiwa ni pamoja na Jezi full kwa timu zote shiriki, jezi za waamuzi na na jezi za makipa kwa timu zote, ambapo msemaji wa foreplan Clinic BAraka Samweli, wamesema kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa MAra mbili ukilinganishwa na michuano ya miaka miwili iliyopita, ambapo pia imeongezeka kwa Kikundi cha Ushangiliaji. 

panda kutoka Milioni Tano na kufikia Milioni 10, ambapo pia amewataka washiriki wa michuano hiyo kuyatumia mashindano hayo kwa nidhamu ili kuleta tija ya kuokoa vijana wengi katika kukuza Vipaji kwa vijana wa jiji la Dar es Salaam.


MWenyekiti wa chama cha Mpira wa Mkoa wa Dar es SAlaam kama mwakilishi wa kamati ya mashindano bwana almasi KAsongo amesema kuwa anajivunia na kufarijika kutokana na kuwajumuisha makundi mbalimbali baina ya Wachezaji wa timu, Viongozi, Vyama vya Soka na Waandishi wa habari ambapo Faida kubwa imeendelea kupatikana ikiwa ni baada ya timu za Ligi kuu ya Tanzania na Ligi zingine kujikuta ikiwatumia wachezaji wengi wanaoshiriki kwenye hii michuano ya DR MWAKA NDONDO CUP.

na kwamba pamoja na kushiriki mwaka wa tatu hadi sasa michuano hiyo aijaingia kwenye dosari yoyote kama zilivyo ligi zingine ambapo mara nyingi wachezaji wanafikia wakati mwingine kushikana mashari, ugomvi pamoja na kuharibu sifa za mashindano imekuwa tofauti sana na michuano hii.

Kwa upande mwingine Shaffi Dauda kutoka Clouds MEdia Group amesema Changamoto kubwa iliyoonekana kwenye michuano hiyo kwa mwaka jana ni baadhi ya timu ususani mashabiki kujazana kwenye eneo la wachezaji ambapo kwa mwaka huu wametakiwa mashabiki wote kutojihusisha na eneo la Timu zinazoshiriki na kuwaacha wachezaji eneo husika kwa ajili ya usalama wa timu na wachezaji.
Timu Zinazoshiriki ni pamoja na Kundi A, Faru Jeuri, Temeke Market, Vijana Rangers, Kinondoni Fc, kundi B : Boom Fc, Abajalo FC, Temeke Squard, Kijiji FC, kundi C : Keko Ferniture, Stakhshari, Tabata United, Mjivuni Fc,  Kundi D: Makumba FC, Kiluvia United, Agrrey Fc, Brokein Chain, Kundi E: Wauza MAtairi, Goms United, Urafiki Shooting,
  
Waandaaji wa Michuano hiyo, Shaffi Dauda Kushoto, akiwa na wadhamini Mke wa Dr MWaka, MWakilishi wa DRFA, Msemaji wa Dr. MWaka BAraka Samweli wa Pili kulia na Kanu wakionyesha kwa  Timu zawadi hizo
Mtoni City, Kundi F: Frendr Rangers, Buguruni United, Jack Pro Fc, Misosi Fc, Kundi G: Burudani Fc, Ndanda FC, Mlalakuwa Rangers, Kibada one na kundi H: FC Kauzu, Black 6, na Madiba FC.
  

No comments:

Post a Comment