TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, June 3, 2016

CHAMA CHA KUTETEA ABIRIA TANZANIA (CHAKUA) KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA SAFARI INDOOR DIGITAL (SID) WAZINDUA MPANGO MPYA WA KUTOA ELIMU KWA ABIRIA KUPITIA TELEVISHENI ZILIZOPO KATIKA MABASI YAENDAYO MIKOANI NA MASAFA MAREFU.

Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria TAnzania(CHAKUA), kulia akifafanua jambo kuhusiana na Ushirikiano na KAmpuni ya Safari Indoor Digital (SID) wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa kutoa Elimu kwa Abiria kupitia Televisheni (Screen) Zilizopo katika Mabasi Yaendayo Mikoani na MAsafa Marefu.Wengine kutoka kulia ni Innocent Malethowa kutoka Safari Indoor,(pili kulia),Mkurugenzi wa Utawala wa kampuni ya Usafiri ya Safari Indoor, Doreen Chamberlain wa pili kutoka kushoto na Lulu Masawe kutoka Kilimanjaro Express, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo. (PIcha Kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Na: Shaaban Mpalule- Maelezo.

Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA), kwa kushirikiana na Kampuni ya Safari Indoor Digital (SID) na Kampuni ya Mabasi ya Kilimanjaro ExPress , imezindua mpango wa mpya na wa Kisasa katika kutoa Elimu kwa abiria kupitia Televishen zilizopo katika mabasi yaendayo Mikoani na Masafa Marefu na nje ya nchi.

 Akizungumza kwenye Ukumbi wa Idara habari Maelezo leo, Mkurugenzi wa Utawala wa kampuni ya Usafiri ya Safari Indoor, Doreen Chamberlain, amesema kuwa mpango huo utawawezesha abiria kupata na kujifunza masuala mbali mbali.
aidha Safari Indoor Digital wakiwa kama wadau wakubwa wa usafiri kwa kushirikiana na jeshla polisi, SUMATRA wametengeneza kipindi maalum ambacho ambacho kitaandaliwa na kampuni ya SAFARI INDOOR DIGITAL (SID).

kutokana na hali hiyo CHAKUA inawataka abiria wote kuitumia fulsa hiyo vizuri kusogezewa huduma ya elimu ili kujitetea au kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika ikiwemo polisi , Sumatra na chakua pindi wanapofanyiwa manyanyaso katika vyombo vya usafiri kwani wakati elimu ikitolewa katika Screen kutatolewa pia na namba za simu kwa ajili ya malalamiko.
 

No comments:

Post a Comment