TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, May 30, 2016

BINTI AKIMBIA NDOA YA KULAZIMISHWA NA BABA YAKE-MBAGALA



NA : Mwandishi Wetu.

Mkazi mmoja jijini Dar es salaam maarufu kwa jina la Ally Abdalah Sharif mfanyabiashara mkazi wa Mzambarauni Mbagala, kwa kushilikiana na Mwenzake aliyepatikana kwa jina la Ustadhi Twaha mkazi wa Picha ya Ndege Kibaha –Pwani wanaendelea kumshikilia Msichana Aziza Ally mwenye umri wa miaka 19 maeneo ya  Picha ya ndege kwa kutaka kumuozesha  kwa mwanaume ambaye siyo kwa ridhaa yake.   
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Aziza ambaye pia ametoka kuishi na mume wa kwanza ambaye inasemekana kwamba aliozeshwa kwa shinikizo la baba yake bila lidhaa ya msichana huyo ambaye pia ni sawa na yatima kutokana na kufiwa na mama yake mzazi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa maeneo ya mbagala ambao haawakutaka kutajwa majina yao walisema kuwa,” Kuna Mzazi amewahi kumuozesha Binti yake akiwa na Umri wa Miaka 17 kwa Mwanaume ambaye Binti akuwa chaguo lake, pamoja na kwamba msichana huyo alitaka kusoma lakini baba yake alimkatalia na kumtafutia mwanaume ambaye akuwa chaguo lake na baada ya Muda wa Mwaka mmoja huyo Binti alishindwana na huyo Mume.

Na kuongeza kuwa kuondoka kwa mume wa kwanza siyo kwamba aliachika, bali aliondoka mwenyewe kwa kuwa huyo mume aliozeshwa bila yeye kuwa na ridhaa ya moyo wake, hivyo aliamua kutafuta sababu za kuwagombanisha ili kutaka kuondoka, hivyo ikaonekana kama Wameachana lakini pamoja na kuondoka kwa huyo mume aziza ajawahi kupewa Talaka, ila alirudi nyumbani kwa Baba yake ambaye mpaka sasa anaishi yeye na mama yake wa kambo, 

Lakini tunashangaa tunasikia kwamba Baba yake Katafuta Jibaba lenye Umri wa Zaidi ya Miaka 40 na kumtaka Aziza aolewe tena baada ya Baba yake kuchukua Pesa kwa huyo Mtu, “baada ya Muda Binti aliambiwa nia ya kuolewa na huyo mtu ambaye akuwa tena chaguo lake, baada ya binti huyo kusikia hayo aliamua kutoroka nyumbani ili kukimbilia kwa ndugu wengine wa familia, tunasikia kwamba akiwa njiani baada ya kutoroka katika kujiokoa na hiyo hali gafla rafiki wa Baba yake, ambao tayari walikuwa wamepewa taarifa ya kukimbia kwa aziza walifanikiwa kumkamata akiwa kwenye harakati za kusafiri, 


Masikini Binti wa watu, mama yake Mzazi alishafariki hivyo anaishi na baba yake na mama wa Kambo, Maeneo ya Mbagala Mzambarauni, tunasikia baada ya kukamatwa na huyo Rafiki wa baba yake anayetambulika kwa jina la Twaha, huyo mtu alijidai kwamba angemsaidia kutomuambia baba yake, na huyo binti alikubali kwenda kujificha akitarajia huyo baba yake Mkubwa kama anavyojitambulisha angeweza kumsaidia.

Pamoja na kuaidi kumsaidia kumpeleka katika hifadhi nyumbani kwake Maeneo ya Picha ya Ndege Kibaha kuelekea mlandizi maana alikamatiwa kibaha, huyo Binti baada ya kufika kwa huyo mtu baadaye alimwambia kwamba awasiliane na baba yake waje wazungumze ila hawatamuozesha kwa nguvu, lakini baada ya baba yake kufika eneo hilo walimtishia huyo binti kwamba, asipoolewa yeye na baba yake ndiyo utakuwa mwisho wa kujuana, hivyo akubali ili wasigombane na baba yake ambaye tayari ameshachukua Badhi ya Mahali, huku pia wakimdanganya huyo binti kwamba huyo mume ni tajiri wa ng'ombe, atamuwekea ng'ombe wawili na kumpangishia chumba kutokana na huyo mtu kuwa dereva wa malori.
Habari za kuaminika zinasema kwamba mtu huyo pia yupo na mke mwingine na watoto wakubwa kama yeye, mpaka sasa huyo binti anashikiliwa huko kibaha kuelekea mlandizi ambako wakati wowote wanatarajia kumfungisha ndoa hiyo ambayo yeye moyoni mwake haipo, Umasiki na kufiwa na mama yake pamoja na roho ya kikatili na Tamaa ya Pesa ya baba yake, ambaye pia anajidanganya kwa ibada nyingi na kujiita Ustadhi inamuweka Binti huyo katika kutenda pasipo matakwa yake, 

Mashaidi wa huyo Binti ambao ameweza kuwaelezea hiyo habari ni pamoja na mjomba wake mzaliwa na mama yake ambaye yeye anaishi arusha, isipokuwa ameshindwa kufika kumsaidia huyo binti kutokana na kuugua lakini namba yake ya simu ni 0784907253, pamoja na namba ya baba yake Mkubwa ambaye anaishi mwanza ambaye ndiko alikokuwa akikimbilia huyo Binti kabla ya kukamatwa na hao watu namba yake ni 0767554920, namba ya mtu ambaye anamshikilia huyo binti kama mateka wa udanganyifu kwa jina maarufu la Twaha, ni 0713237573, ambaye ni mkazi wa maeneo ya Picha ya Ndege, Binti huyo kwa sasa amenyang'anywa simu atakiwi kuwasiliana na Mtu hadi azimio lao litimie, namba ya Baba yake mzazi ni 0755837343,

 kinachonishangaza mimi ni pale inapovunjwa Sheria ya Ndoa na kupinga Mahudhui ya Mungu, Kwani huyo Binti ameolewa na Bado ajapewa talaka na Mume wake wa Mwanzo pamoja na kwamba huyo Binti kamkimbia mume kwa hizo sababu za kupewa mume asiyekuwa na makubaliano naye, Je Siku hizi dini ya Kiislamu imefikia hatua ya kutenda hayo ambayo ni kinyume na maadili ya Mungu? 

lakini je inakuwaje Wazee ambao wanajiita waislam wanashiriki Huo uovu tena mchana kweupe? ni kweli nyie wote mnaosoma hii Habari ni Wakristu kwamba hamtaki kufuatilia hiyo habari? Dawati la Jinsia na nyie siku hizi hampo kwa kuwasaidia wanawake wanaopata majanga kama haya? 

Ustawi wa Jamii mko wapi kuwashugulikia hawa na kuwasaidia watoto Yatima? Tume ya Haki za Binadamu nadhani mnaisoma hii habari, Vipi na Nyinyi kuhusu Haki za Watu hakuna siku hizi? TAKUKURU pia hamjaisoma hii habari? maana hiyo ni Rushwa tena mbaya sana, Binadamu Kuuzwa sasa bila ridhaa yake tunaelekea Dunia ya ngapi?
 JEshi la polisi kwani Tanzania sasa tunajihesabia wenyewe makosa au mnatuhesabia Nyinyi makosa? TGNP kwa nini msiwafuatilie hawa watu ili kukomesha tabia hizi chafu na za udhalilishaji wa kijinsia? dhambi hizi zitaendelea kutendwa hadi lini? au ndiyo Mwisho wa Dunia kwamba hata tukiambiwa hatutoi Misaada kwa hawa watoto Waliozaliwa bila Uzazi wa Mpango?

 kwanza baba ameshiriki kuwazaa watoto nje ya ndoa, kisha kuwauza kwa Wanaume na sasa anambadilishia wanaume, kwani ni haki hii? Wapi imeandikwa kwenye Vitabu vya Dini au Katiba ya Tanzania inasema hivyo? je kwa tabia hizo Watoto wa mitaani kweli watakosekana? na Malezi ya hao watoto watakaozaliwa kweli wataweza kupata maadili? au ndiyo tunazidi kuongeza idadi kubwa ya Panya Road, Paka Road wanajiita Black Ninja au Wakabaji mnadhani watakosekana kwa mfumo huo?

 Alafu huyo baba wa huyo Binti anawatishia Watu kukosana nao endapo watamfuatilia kuhusu maamuzi yake, je ni kweli anadhani watu wanamuogopa/ tunamuogopa? na hao wanaoshirikiana naye katika hilo si ni sawa na wale wabakaji? kwani kuna tofauti gani kati ya Mtu anayebaka na huyu anayeshiriki kumlazimisha binti kwenda kwa mtu kwa nguvu bila idhini yake? Jamani Waislam na Wakristu, ebu sasa tutumie mamlaka ya Mungu kuwashikisha Adabu watu kama hawa, Taifa linazidi kupotea kutokana na tabia za kuzaa watoto nje ya Ndoa, kuoa wake kisha kuwaacha, kulazimishwa kwa wasichana kuolewa na waume wasiowataka, na kukubali uwepo wa maeneo ya Wafanyabiashara wa kuuza miili yao yaani Wanawake kuuza na wanaume kununua, 

wote hao wanatakiwa kushikishwa Adabu tena siyo watu wa kuwaacha hata kidogo, nawambia kwamba, MSIWAOGOPE WATU/ WANADAMU hapa Duniani bali MUOGOPENI MUNGU PEKE YAKE, kila mmoja kwa Imani yake Tushirikiane kuhakikisha tunakomesha baadhin ya Tabia ambazo ni Machukizo mbele ya Mungu WEtu: IMeandikwa na Mimi namba yangu ni 0767-869133 na 0713869133, nimefanya uchunguzi wa kina kuhusu jambo hili na ni uhakika nalo asilimia mia.

No comments:

Post a Comment