TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 1, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI NCHINI PAPUA NEW GUINEI LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mzungumzaji Mkuu wa Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye mkutano huo uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo akimpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo wakati Makamu wa Rais alipomaliza kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano huo. Katikati Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Mhe. Natumbo Nandi Ndaitwah. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandaaji wa Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP baada ya kuhutubia kwenye mkutano huo uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na OMR).

No comments:

Post a Comment