TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, June 2, 2016

VINGUNGUTI SUPER 8 CUP 2016

 
 Na: Rajabu Ally Mohamed

Mashindano ya Ligi yaVingunguti Super 8 Cup 2016, yamefunguliwa leo kwenye Uwanja wa Msikate Tamaa uliopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam, ambapo inashirikisha jumla ya timu 8 kutoka maeneo ya kata jiji la Dar es Salaam huku yakiwa yamefunguliwa na Mheshimiwa, Naibu Meya wa Manspaa ya Ilala Omari Kumbilamoto. aidha mashindano hayo yapo hatua ya kwanza ya Makundi kabla ya kuingia hatua ya pili na yatafanyika kila siku isipokuwa siku za jumatatu, Jumanne na Jumatano ambazo zitakuwa ni siku za mapumziko kwa mujibu wa waandaaji wa Mashindano hayo, Timu zinazoshiriki ni pamoja na Vingunguti Kombaini, Vingunguti Rangers, Jua Kali, Home Boys, Makongo, Buguruni United, Dar Stars ya Ilala, na Danger Fc, katika ufunguzi huo timu zilizochuana leo ilikuwa ni Vingunguti Rangers dhidi ya Home Boys ya Tabata na matokeo timu hizo zimegawana poini kwa kufungana 1-1, huku wafungaji wa magoli wakiwa ni Ally Waziri wa Home boys na Matheo Angelo.

Akizungumzia Mashindano hayo mara baada ya Ufunguzi, mheshimiwa Diwani alisema kuwa, ni faraja kwa vijana wa maeneo ya Ilala ususai katika Maeneo yote ya Vingunguti kwa lengo la kuinua Vipaji kwa vijana, ambapo zawadi mbali mbali zitatolewa katika kilele cha michuano hiyo ikiwemo Jezi Seti mbili zenye thamani ya shilingi laki tano kwa mshindi wa kwanza, Jezi seti moja yenye thamani ya shilingi laki mbili na nusu kwa mshindi wa pili na mpira mmoja kwa mshindi wa Tatu, na mfungaji bora atazawadiwa pia pea moja ya Jezi, timu yenye nidhamu itapatiwa zawadi ambayo itatangazwa hapo baadaye wakati mashindano yakiendelea.

hata hivyo amewataka vijana wote wanaoshiriki kwenye ligi hiyo, kuyatumia vyema mashindano hayo ili kuleta tija ya umoja, mshikamano, na pia iwe moja ya njia za kuwakutanisha katika kubadilishana mawazo, lakini pia akisisitiza  wawe watulivu wakati wote wa mchezo na wawe na nidhamu kwa waamuzi na pia wao wenyewe ndani ya Uwanja, Siku ya Jumamosi timu zitakazochuana ni kati ya Vingunguti Kombaini dhidi ya timu ya Danger fc ya Gongolamboto. 



 Wachezaji wakiwa kwenye ukaguzi




 Wachezaji wa timu hizo wakiwa kwenye ukaguzi
 Mwandaaji wa Ligi hiyo, Twalib Hamdani(wa pili kulia), akiwa kwenye kutafakali jambo wakati wa funguzi wa michuano hiyo.
 Mheshimiwa Diwani wa Vingunguti, Omari Kumbilamoto akifuatilia mpambano huo kwa makini.
 Kocha wa Timu ya Vingunguti Kombaini, Spia Mbwembwe(kushoto)na Mdau wa michezo wakifuatilia mpambano huo.
 Baadhi ya Viongozi. kulia ni Mwandaaji wa ligi hiyo Twalib Hamdan, Diwani na mstahiki Meya wa Ilala Omari Kumbilamoto(kati) na MWenyekiti wa Serikali ya Mtaa. 

No comments:

Post a Comment