TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, April 12, 2016

WAFANYAKAZI HEWA WAMPONZA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA,MAMA ANNA KILANGO, RAIS DKT. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WAKE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, mchana huu ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anna Kilango Malecella, kwa kubaini kuwa alimwambia uwongo kuwa Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa wakati kumbe wapo wengi tu.
Rais Magufuli amesema kwamba hakuamini kwamba kuna mkoa ambao hauna wafanyakazi hewa, hivyo akatuma kikosi kazi ambacho hadi usiku wa kuamkia leo kimebaini kuwepo na wafanyakazi hewa 45 mkoani Shinyanya.
Rais Magufuli, ambaye alikuwa anaongea baada ya kupokea Ripoti ya TAKUKURU  toka kwa Mkurugenzi wake Mkuu  Valentino Mlowola,  amesema kasikitishwa sana na kauli ya Mama Malecela ambaye bila shaka alikuwa amepata ushauri mbaya toka kwa watendaji wake. 
Amesema idadi hiyo ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili zilikuwa bado zinaendela kuhakikiwa. Rais Magufuli amesema pia kwamba hadi jana jumla ya wafanyakazi hewa zaidi ya 5, 507 wamebainika nchi nzima, wengi wao wakitoka katika halmashauri.
Hivyo Rais pia ametengua uteuzi wa  Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi. Wakuu wa mikoa waliapishwa mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment