Na Mwandishi Wetu, Nairobi 
 
  Timu
 ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) inayodhaminiwa na bia ya 
Kilimanjaro jana imeshuka uwanjani kumenyana na Zambia, katika mechi ya 
ufunguzi ya michuano ya Kombe la Chalenji. 
Kilimanjaro
 Stars na Zambia zimechuana kuwania pointi tatu katika mchezo 
uliochezwa Uwanja wa Machakos ulioko nje kidogo ya jiji la Nairobi. 
Timu
 hiyo ya Tanzania Bara iliyopangwa Kundi B, ilihitaji ushindi ili kupata
 pointi tatu ambazo zingeiweka katika nafasi nzuri kwenye michuano hiyo. 
Akizungumzia mchezo huo wa jana, Kocha Mkuu wa Kili Stars, Kim Poulsen alisema timu yake imeshindwa kupata ushindi kutokana na wachezaji wengi kuwa wachovu wa safari, 
Alisema
 kikosi chake kimefanya mazoezi  magumu, amb a y o bado wachezaji wanauguza viungo vyao,  hata hivyo kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya Zambia inayosifika kwa kutandaza soka ya kiwango
 bora Afrika. 
Kilimanjaro
 Stars iliwategemea zaidi wachezaji kama Mrisho Ngasa, Amri Kiemba, Erasto 
Nyoni, Kelvin Yondani, Said Morad, Athuman Idd na Salum Abubakar. 
Pia, wamo Frank Domayo, Himid Mao, Haruna Chanongo, Ramadhan Singano ‘Messi’, Farid Mussa na Elias Maguli. 
 
Katika
 mechi ya ufunguzi iliyochezwa juzi mchana timu ya taifa ya Zanzibar 
iliifunga Sudan Kusini mabao 2-1 katika mchezo mkali uliokuwa na 
ushindani.
No comments:
Post a Comment