TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, July 18, 2016

Rais Magufuli ateua Mkurugenzi Mkuu SIDO na Mkurugenzi Mtendaji Hosp ya Benjamin Mkapa Dodoma

KUTOA MSAADA HAIMAANISHI NI KUTENGENEZA MAZINGIRA YA KUKWEPA KODI-MAKONDA








=====================================

MKURUGENZI KISHAPU AKUTANA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI,AWATAKA KUWA NA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA NA RASILIMALI ZA SERIKALI.

Rais Magufuli aagiza wafanyakazi wa Polisi ambao ni raia wapelekwe Utumishi

Hussein Makame-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemwelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu kuwahamishia Utumishi baadhi ya wafanyakazi wa jeshi hilo ambao si askari ili kujenga nidhamu ya kijeshi katika wizara hiyo.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo Ikulu jijini Dar es Salaam, mara baada ya kushuhudia kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kwa askari 58 wa jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo hivi karibuni.

Alilazimika kutoa agizo hilo kufuatia tukio la kusimamishwa kazi kwa Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Frank Charles Msaki kutokana na tuhuma za kufanya malipo hewa huku akidaiwa kutumia madaraka yake vibaya.

“Wahamishieni kule Utumishi wale wakorofi ili hawa raia wanaofanya kazi kwenye nafasi za jeshi waondoke, kwani hakuna askari wanaojua masuala ya fedha? Huwezi ukachanganya askari na wafanyakazi wasio askari.Naomba IGP uliangalie vizuri hili ili raia ambao wanasumbua jeshi uwapeleke Utumishi” alisema Rais Dkt. Magufuli.

Akifafanua kuhusu mhasibu aliyesimamishwa, Rais Magufuli alisema mhasibu huyo alikuwa na mamlaka hata ya kuwakemea askari, ndipo alipotoa agizo asimamishwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amemuagiza IGP kufuatilia taarifa inayodai kuwa kuna mfanyabiashara aliyelipwa mabilioni na Jeshi hilo bila ya kutoa huduma ya kushona sare za askari.

Alisema taarifa za mfanyabiashara huyo zinadai kuwa alilipwa kati ya Shilingi bilioni 20 hadi 60 bila ya kutoa huduma hiyo, huku jeshi la Polisi likiwa halijatoa taarifa yoyote kuhusu madai hayo.

Alisema wakati fedha hizo zikidaiwa kulipwa bure, fedha hizo zingeweza kusaidia jeshi hilo kulipia kodi magari yake 77 yanayodaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Pamoja na maagizo hayo, Rais Dkt. Magufuli alieleza kuridhishwa na utendaji kazi wa jeshi hilo na kueleza kuwa kutokana na hali hiyo aliona ni wajibu wake kuwapandisha vyeo askari ambao utendaji kazi wao ni wa kuridhisha.

Lukuvi amteua Jaji wa Mahakama Kuu kuchunguza mgogoro wa ardhi wa miaka 27

Vijana 559 waishio katika mazingira magumu,wahitimu VETA









RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAAFISA WA JESHI LA POLISI WALIOPANDISHWA VYEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM,AWATAKA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WANAOLETA MATATIZO


Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo vya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na Naibu Kamishna wa Polisi DCP mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) mara baada ya kula kiapo cha Maadili ya Watumishi wa umma Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagaia vitafunwa wageni mbalimbali waliofika Ikulu kwa ajili ya kushuhudia Maafisa wa Polisi walipondishwa vyeo wakati wakila kiapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagaia vitafunwa baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria tukio hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Pamoja na kutoa agizo la kutaka wasio askari polisi kuondolewa katika utumishi wa jeshi la polisi, Rais Magufuli pia ameagiza jeshi hilo lichukue hatua dhidi ya wote wanaokabiliwa na tuhuma za wizi wa fedha wakiwemo wanaodaiwa kuiba mabilioni ya shilingi zilizotolewa kwa ajili ya ununuzi wa sare za askari mwaka jana 2015.
"Mnajua kupeleleza, mna vyombo vyote, ofisi ya IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) ipo palepale, ofisi ya DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai) ipo palepale, Makamishna wote mnazunguka mnakwenda palepale, mwizi mnae palepale, mnashindwa kumshika.
"Kama mnafikiri kuwa na raia katika jeshi la polisi wanawaharibia kazi zenu hamisheni raia wote na wapelekeni utumishi, kwani hakuna mhasibu ambaye ni askari polisi? hakuna mhandisi ambaye ni askari polisi? hakuna afisa tawala ambaye ni askari polisi? Mimi nafikiri kama matatizo ya wizi na wafanyakazi hewa yanaletwa na raia waliomo ndani ya jeshi la polisi na majeshi yetu mengine, IGP kaorodheshe raia wote wanafanya kazi Jeshi la Polisi ili waondolewe na tuwapangie kazi nyingine uraiani" Amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri linayofanya iliyoliwezesha kujenga imani kubwa kwa watanzania na ametaka viongozi wa Jeshi hilo wawaongoze askari walio chini yao vizuri, wawatie moyo na waache vitendo vya kuwakatisha tamaa kwa kuwaadhibu ama kuwatisha pale wanapochukua hatua stahiki dhidi watu wanaovunja sheria.
"Sasa mimi niwaombe nyinyi, wale wadogo mnaowaongoza mkawape mamlaka ya kutimiza wajibu wao, hata kama ameshika gari la IGP liache lishikwe IGP atakwenda kujieleza mwenyewe, hata akishika gari la RPC afanye hivyohivyo, hata akishika gari la Waziri au gari la Rais mwacheni atekeleze wajibu wake, sheria ni msumeno, tunawanyima nguvu hawa wa chini wanapotimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria halafu unamwambia liachie, ukifanya hivyo aliyeshikwa anatoka pale akiwa anatamba kwelikweli na yule askari unamvunja nguvu ya kufanya kazi" Amesisitiza Rais Magufuli. 
Rais Magufuli pia amelitaka jeshi hilo kuungana na vyombo vingine vya serikali katika kutekeleza shughuli zake zikiwemo kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali bandarini, katika sekta ya utalii na maeneo mengine, kukabiliana na vitendo vya rushwa na kuondoa watumishi hewa.
Tukio hili la Naibu Makamishna wa Polisi na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yusuf Masauni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Makatibu Wakuu na Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
18 Julai, 2016

BLESSING KUFAYA UCHANGIAJI WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI WASIO NA UWEZO.







=======================================

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA 27 WA AU NCHINI RWANDA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 27 kwa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU ulioanza jana katika ukumbi wa KCC mjini Kigali Rwanda. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.Picha na OMR.
KIGALI, RWANDA.
Tanzania imeuhakikishia Umoja wa Afrika (AU) kwamba itaendelea kufanya kazi kwa karibu na nchi wanachama wa AU katika kujadili changamoto za kiusalama zinazolikabili Bara la Afrika kwa njia ya mazungumzo na upatanishi kama inavyoelekeza Katiba ya umoja huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akichangia mada kuhusu Hali ya amani na usalama katika Bara la Afrika katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika hapa Kigali, Rwanda.Mheshimiwa Samia alisema Tanzania inasikitishwa na inalaani vikali matukio ya uvunjifu wa amani yanayoendelea kujitokeza katika baadhi ya nchi za Kiafrika kiasi cha kutishia usalama wa raia.

Alielezea mauaji ya Hafsa Mossi, aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na waziri wa zamani wa Burundi na mapigano ya hivi karibuni Sudan ya Kusini ambapo mamia ya raia wasiokuwa na hatia waliuwawa na wengine maelfu wameachwa bila makazi kwamba ni muendelezo wa uvunjifu wa amani katika nchi hizo.

Aliwataka wadau husika katika nchi za Burundi na Sudan ya Kusini kushiriki kikamilifu katika mazungumzo yanayoendelea kwa kuwa hiyo ndiyo njia muafaka ya kuleta amani, usalama na utulivu wa kudumu  katika nchi zao.Aidha, Makamu wa Rais ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo aliiomba Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kuisadia Sudan ya Kusini katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu katika mgogoro ulioikumba nchi hiyo.

Akichangia kuhusu mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Makamu wa Rais alisema Tanzania kwa ujumla inaunga mkono msimamo wa Afrika wa kuwa na viti viwili katika baraza hilo na kura ya turufu bila ya masharti yoyote.Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo viongozi walisisitiza suala la kuimarisha umoja baina ya nchi wanachama na kusema hiyo ndiyo nguzo muhimu katika kukuza uchumi na ustawi wa wananchi wa Bara la Afrika.

Katika mkutano huo kulikuwa na uzinduzi wa pasi ya kusafiria ya Afrika ambayo ilitolewa kwa Mwenyekiti wa AU, Rais Idris Deby wa Chad na nchi mwenyeji wa mkutano, Rais Paul Kagame wa Rwanda.Mkutano huo ambao ulizungumzia pia gharama za kuendesha umoja huo na masuala ya haki za wanawake ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi zaidi ya 35, Marais wastaafu, wake wa Marais pamoja na viongozi wa serikali.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais 
==================================================

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kongamano la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji.










No comments:

Post a Comment