TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, July 20, 2016

Hili ndilo Tamko la Spika wa Bunge chuo cha elimu UDOM



Habarini za muda na wakati kama huu wapendwa watanzania wenzangu. Ni matumaini yangu kuwa mnaendelea vizuri katika shughuli zenu za kila siku.

Nichukue fursa hii kuwashukuru Mtandao wa wanafunzi TSNP na vyombo vya habari nchini kwa kukubali kushirikiana nami GIBSON JOHNSON (Spika wa Bunge chuo cha elimu UDOM) na wanafunzi wa SPECIAL DIPLOMA KWA UJUMLA katika kutafuta na kutetea maslahi yao juu ya kile kinachoitwa uonevu waliotendewa na serikali. Lakini pia niwashukuru wanasiasa na wanaharakati mbalimbali waliopaza sauti zao kukemea vikali ukiukwaji wa utu kwa wanafunzi wa special diploma UDOM.

Nimepitia vizuri maelezo ya serikali juu ya msimamo wake na hatma katika suala hili la UDOM lakini nimegundua pia haki haijafuatwa hata kidogo zaidi sana ubabe ndio uliotumika katika maamuzi haya. Nasema hivyo kwasababu zifuatazo;
1. Vigezo vilivyotumika katika kuchambua wenye sifa na wasio na sifa si vile vilivyotumika mwanzo wakati wanafunzi hawa wanachaguliwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Mh. Rais mstaafu na waziri Mkuu pamoja na waziri wa elimu. Tamko la sasa la serikali linasema kuwa wanatakiwa wenye angalau krediti mbili kwenye tahasusi (comb) hii ni kinyume na makubaliano ya awali ambayo yalikuwa yakihitaji mtu awe na angalau C moja kwenye tahasusi (comb) atakayosoma.
 Serikali imetoa msimamo wake ambao ni hasi kwa wanafunzi 1210 waliokuwa wanasoma diploma in primary kwani imesema walikuwa nje ya malengo hivyo mpango huu wa diploma maalumu ulikuwa hauwahusu bali ulikuwa maalumu kwa wale wa sekondari. Jambo hili ni kinyume na haki kabisa kwani wamepotezewa muda mwingi sana kwani kuna waliokuwa wanasoma mwaka wa kwanza na wengine mwaka wa pili ambao wote walichaguliwa na mamlaka husika yaani TCU pamoja na NACTE na hawakujichagua wenyewe. Hivyo basi kulingana na hivyo seeikali haina budi kuwatafutia vyuo ambavyo watamalizia masomo yao kinyume na kuwaacha tu kwa kuwaambia haiwatambui, huu ni uzalilishaji mkubwa na ukiukwaji wa haki.
My Note:
Ni vizuri sana kuihimiza serikali kufuata sheria, kanuni na taratibu katika kuiongoza nchi na si kuongozwa na mawazo ya mtu mmoja tu. Pili, suala la kuwaacha nyumbani wanafunzi waliokuwa wanasoma diploma in primary kwa kigezo eti haikuwatambua halileti tija wala mantiki yoyote kwa taifa na wananchi pia hivyo serikali inapaswa kuliangalia upya jambo hili na kuwawajibisha wahusika waliokubali kuwepo kwa  na sio program hii.

Mwisho:
Niwaombe vijana wote waliokumbwa na janga hili tuwe na ushirikiano na umoja wa hali ya juu katika kuitafuta haki.

Imetolewa na;
Gibson Johnson E.

No comments:

Post a Comment