TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, July 20, 2016

Vyuo vikuu vyatakiwa kuunga mkono Serikali katika kujenga Tanzania ya Viwanda

Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amevitaka vyuo vikuu Tanzania kuunga mkono serikali ya Awamu ya Tano juu ya uanzishwaji wa viwanda kuelekea uchumi wa kati.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua maonyesho ya kumi na moja ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Julai 20 mpaka Julai 22 mwaka huu.

“Vyuo vikuu vinatakiwa kuangalia sera za nchi na mwelekeo wa Taifa kuelekea kukuza uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha wanatoa wataalamu ambao watashiriki katika uchumi wa viwanda ambavyo vitaanzishwa nchini,” alifafanua Prof. Ndalichako

Prof. Ndalichako aliendelea kwa kusema kuwa Serikali iko katika mkakati wa kuboresha vyuo vya ufundi kwa kuanzia na vyuo vitatu vya ufundi vya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya ili kuboresha mafunzo wanayoyatoa kuendana na uhitaji uliopo katika uanzishwaji wa viwanda.

Mbali na hayo, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi inashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika uanzishwaji wa mafunzo katika sekta adimu ikiwemo gesi kwa ajili ya kupata wataalamu watakaoajiriwa katika viwanda vitakavyo anzishwa.

Vile vile wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu hupewa maelekezo ya namna ya kuomba vyuo kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) pamoja na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) katika maonyesho hayo.

Maonyesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia hufanyika kila mwaka yakiwa na Lengo la kutoa elimu kwa wazazi na wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu hapa nchi waweze kujua kozi zinazotolewa katika vyuo hivyo pamoja na maelezo ya kozi hizo.
 
============================================

Serikali yapongezwa kwa kuwajali watu wenye mahitaji maalum

Wakonta Kapunda akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wake,Dada yake, marafaiki zake aliosoma nao shule ya Sekondari Korogwe na mshiriki mwenzake katika Shindano la uandishi wa Miswada lililofanyika mjini Zanzibar leo Jijini Dar es Salaam. Picha Zote na: Frank Shija, MAELEZO.
Wakonta Kapunda : Msichana mwenye umri wa miaka (22) akitumia ulimi kuandika meseji kwenye simu yake ya Mkononi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Dada yake Bi. Judith Assenga.Binti huyo ameanza kutumia kiungo hicho katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutokana na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa wakati wa Mahafali ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe Mkoani Tanga.

Msichana mwenye umri wa miaka (22) Bi. Wakonta Kapunda akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa Radio ya Kimataifa ya Ufaransa (Rfi) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Binti huyo anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga.

Judith Assenga(kushoto) dada yake na Wakonta Kapunda akimuelekeza jambo mdogo wake wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wakonta anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga.
  
Mratibu wa Masuala ya Habari katika Kampeni ya kumsaidia Wakonta Bw. Joseph Kithama akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namba ambazo wadau wanaweza kutumia kumchangia Binti huyo anayehitaji msaada ili apatae matibabu na kutimiza ndoto zake za kwasaidia wengine wenye matatizo kama yake leo jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia ni Wakonta Kapunda, Judith Assenga(dada yake na Wakonta), Mwajuma Selkemani na Chritina Rubangula(waliokuwa wanafunzi wenzake na Wakonta) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wakonta anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga. Baba mzazi wa Wakonta (hayupo pichani) Bw. Brazilio Kapunda akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa Radio ya Kimataifa ya Ufaransa (Rfi) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.Mwenye brauzi nyekundu ni Mama wa binti huyo Bibi. Rahel Lymo,Wakonta anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Waandishi wa habari wakiwa wameshika karatasi lenye namba ambazo wadau wanaweza kutumia kumchangia Wakonta Kapunda (aliyekaa kwenye kiti cha matairi) ili apatae matibabu na hatimaye kutimiza ndoto zake za kwasaidia wengine wenye matatizo kama yake leo jijini Dar es Salaam.Binti huyo amekusudia kutumia kalama ya uandishi wa Filamu na kuanzisha Taasisi itakayo kuwa msaada kwa watu wenye matatizo ya kupooza.


Na: Frank Shija, MAELEZO

Msichana anayetumia Ulimi katika kuandika miswada ya Filamu amewashukuru wadau mbambali kwa misaada yao iliyomfanikisha kuweza kushiriki katika mashindano ya uandishi wa miswada ya Filamu yaliyofanyika mjini Zanzibar.

Shukuruani hizo amezitoa leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anaongea na waandishi wa habari kuhusu malengo yake ya kuanzisha Taasisi itakayosaidia watu wenye matatizo kama yake.

Wakonta amesema kuwa kwa namna ya kipekee kabisa anaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kupitia kwa Bodi ya Filamu kumgharamia nauli iliyomsaidia kutoka kijijini kwa Kipili wilayani Nkasi mkaani Rukwa hadi kuanikisha ushiriki wake katika mashindano hayo.

“Ninaishukuru sana kwa kipekeke Serikali ya awamu ya Tano, kwani kupitia kwa KatIBU Mtendaji wa Bodi ya Filamu nimeweza kusaidiwa fedha iliyoniwezesha kushiriki katika mashindano ya Uandishi wa Miswada ya Filamu nashukuru sana”. Alisema Wakonta.

Aliongeza kuwa pamoja na Serikali kumpa msaada huo wapo baadhi ya wadau ambao nao wametoa michango yao katika kufanikisha Kampeni yake ambapo amewataja wadau hao kuwa ni Clouds Media waliomsaidia kuhabarisha umma, Joyce Kiria aliye safiri hadi kijijini kwao Kipili ili kumsaidia kupitia kipindi chake cha Wanawake Live.

Wengine ni pamoja na magazeti ya Mwananchi na Uwazi kupitia waliokuwa msaada kupitia habari zao, Fastjet waliomsaidia huduma ya usafiri kutoka Mbeya na Hoteli ya Serena waliomsaidia upande wa malazi wakati alipofika Dar es Salaam akitoea kijini kwao Kipili, Mkoani Rukwa.

Ametoa rai kwa wadau wenye nafasi zao kujitokeza na kushirikina naye katika kukuza kipaji chake ili aweze kukitumia katika kuleta tija kwa Taifa kwani kupitia Filamu unaweza kutangaza Utalii wanchi na ata biashara.

Wakonta alikuwa miongoni mwa washiriki 15 kutoka Afrika Mashariki katika Shindano la Uandishi wa Miswada ya Filamu la Maisha Scree Writer’s Laboratory Course lililofanyika mjini Zanzibar na huku yeye akiwa mshiriki pekee anayetumia Ulimi katika kuandika.
 
=============================================

CHUO KIKUU CHA KIISLAMU CHA MOROGORO WASHIRIKI MAONESHO YA VYUO VIKUU, FROF. NDALICHAKO ATEMBELEA BANDA LA CHUO HICHO

No comments:

Post a Comment