WILAYA YA MOMBA – MAUAJI.
·         KUFUATIA
 TUKIO LA MAUAJI LILITOKEA MNAMO TAREHE 19.12.2013 MAJIRA YA SAA 
14:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA TAZARA -TUNDUMA   KATA NA TARAFA YA 
TUNDUMA   WILAYA YA  MOMBA  MKOA WA MBEYA. AMBAPO MTOTO KALIBU S/O 
KIMWELU, MIAKA 6, MNYAMWANGA,  MKAZI WA MTAA WA TAZARA TUNDUMA ALIUAWA 
KWA KUCHINJWA SHINGONI KWA KUTUMIA  KISU   NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. 
AIDHA WATU HAO WALIMNYONGA SISTA D/O NYILENDA, MIAKA 17, MNYIHA, 
MFANYAKAZI WA NDANI [HOUSE GIRL] KWA KUTUMIA WAYA WA TELEVISHENI 
ULIOKUWEPO SEBULENI. MBINU NI KUWAVAMIA WAHANGA WAKIWA NDANI NYUMBANI 
KISHA KUWAUA KINYAMA. MIILI YA MAREHEMU WOTE ILIKUTWA SEBULENI. WAKATI 
WA TUKIO BABA WA MTOTO AITWAE ESTON S/O KIMWELU,MIAKA 55, MNYAMWANGA,  
DIWANI WA KATA YA  MKANGAMO – CCM,  MKAZI WA TAZARA  ALIKUWA  SHAMBANI 
KIJIJI CHA KIPAKA NA MAMA WA MTOTO AITWAE  TUMAINI D/O YOHANA, MIAKA 29,
 MNDALI, KATIBU MUHTASI  HALMASHAURI YA  MJI MDOGO WA TUNDUMA ALIKUWA 
KAZINI.  KATIKA TUKIO HILO WATU HAO PIA WALIIBA MABEGI MAKUBWA MAWILI 
YENYE NGUO MBALIMBALI YALIYOKUWA KATIKA CHUMBA WANACHOLALA WATOTO.  
·         KATIKA
 TUKIO HILO MMOJA WA WATILIWA MASHAKA WALIOKUWA WAMESHIKIWA NA JESHI LA 
POLISI KWA MAHOJIANO NA UCHUNGUZI ZAIDI AMBAYE NI NDUGU WA MAREHEMU 
ENOCK S/O SIMWELU, MIAKA 23, MNYAMWANGA, MKULIMA AMEKIRI KUHUSIKA NA 
TUKIO HILO AKISHIRIKIANA NA GABRIEL S/O KIMWELU, MIAKA 19, MNYAMWANGA, 
MKULIMA.  WOTE NI WATOTO WA MKE MKUBWA, WAKAZI WA MAJENGO MAPYA TUNDUMA 
 NA PATRICK S/O MSIGWA, MIAKA 18, MKINGA, MKULIMA MKAZI WA MAJENGO MAPYA
 TUNDUMA NI MAJIRANI NA RAFIKI WA WATOTO HAO.
·         AIDHA
 AMESEMA KUWA CHANZO CHA KUHUSIKA NA MAUAJI HAYO NI KUTOKANA NA BABA YAO
 KUWATELEKEZA NA KUANDIKA MALI ZAKE ZOTE KWA JINA LA MAREHEMU KALIBU S/O
 KIMWELU KUWA MRITHI WA MALI HIZO.
        KAIMU
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL 
MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUZINGATIA SUALA LA MALEZI BORA KWA
 WATOTO NA VIJANA WAO ILI WAKUE KATIKA MAADILI MEMA NA KUJIEPUSHA NA 
MATUKIO YA UHALIFU. 
{B.N.MASAKI — ACP )KAIMU: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments:
Post a Comment