TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, December 22, 2013

IRINGA SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI WAFANYABISHARA WATAKAO PANDISHA BEI YA VYAKULA MSIMU HUU WA SIKUKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA



RC Iringa Dr Christine  Ishengoma
Mkuu wa mkoa  wa  Iringa  Dr Christine  Ishengoma ametuma  salama  kali za  Krismas na Mwaka  mpya kwa   wafanyabiashara  watakaopandisha bei  ya  vyakula msimu  huu wa sikukuu kuwa watachukulia hatua  kali.
 
Huku  akiwataka wakurugenzi  wa Halmashauri  zote za wilaya ,wakuu wa wilaya ,maofisa  biashara  wa  wilaya  na mkoa huo  kuanza  kuzunguka mitaani  kuchunguza  bei ya  bidhaa na  kuwataka kuchukua hatua kwa  wote  wanaliopandisha  bei kiholela. 
Akizungumza na  wanahabari jana  ofisini  kwake  ,mkuu  huyo wa mkoa alisema  kuwa imekuwa ni kawaida kwa baadhi  ya  wafanyabiashara  kutumia  sikukuu mbali mbali  kujipatia fedha  kwa kuwanyonya wananchi jambo ambalo katika mkoa huo halitavumiliwa kamwe.
Alisema  kuwa  lengo  la  serikali  ya  mkoa kuwabana  wafanyabiashara ni kutaka  kuona  wananchi  wanasherekea  sikukuu  hizo   na kununua vyakula na vitu  mbali mbali  vya sikukuu kulingana na bejeti  waliyoitenga  kwa  sikukuu  hizo.
” Serikali  ya  mkoa haitakubali  kuona  wananchi  wakiibiwa kwa kuuziwa vyakula kwa bei   kubwa za  sikukuu….tumejipanga  kuchukua hatua  kali na tunaomba  wananchi pia  kutoa ushirikiano “
Hata  hivyo mkuu  huyo wa mkoa alivipongeza  vyomba vya  habari  mkoani Iringa kwa mchango  mkubwa  wa kuhamasisha maendeleo   na kutaka  kuonyesha  ushirikiano katika wakati  huu wa sikukuu kwa  kufanya  uchunguzi  wa  wafanyabiashara  wanaopandisha  bei.
Katika hatu  nyingine  mkuu  huyo wa mkoa aliwataka  wakulima  kutumia mvua  zinazoendelea  kunyesha  kwa  kupanda  mazao mbali mbali yakiwemo  yale yanayohimili ukame kwa maeneo  yeye  changamoto  ya  mvua.
Pia  aliwataka  maofisi  kilimo na  mabwana shamba  kuachana na mpango  wa kuvaa suti na  kushinda maofisini wakati  huu wa msimu wa kilimo badala ya kwenda  kuwaelimisha  wakulima .
Dr  Ishengoma  aliwataka  wakulima  kuendelea  kutumia mbolea  ya Minjingu ambayo  alidai hata  yeye  amekuwa akiitumia na ni miongoni mwa mbolea  bora nchini na kuwataka  kuepuka maneno ya kukatisha tamaa yanayoendelea  kutolewa na  watu juu ya mbolea  hiyo.
Wakati  huo huo  serikali  ya  mkoa  wa Iringa imepiga marufuku  wazazi kuwaruhusu watoto  wao kwenda  kushiriki madisco toto  ambayo alidai ni hatari  na ni  vema  wazazi na walezi wa watoto mkoani Iringa  kuwa makini na kuachana na tabia ya  kuwaacha  watoto  wao peke  yao wakati  huu wa sikukuu.

No comments:

Post a Comment