Alvaro
 Negredo ameifungia Manchester City bao la ushindi usiku huu  dhidi ya 
Liverpool na kuendeleza ubabe wao katika dimba la Etihad.
Liverpool
 ambao wamekuwa wapinzani wa Man City nafasi za juu katika msimamo wa 
ligi kuu nchini England msimu huu walikuwa wa kwanza kuandika bao la 
kuongoza dakika ya 24 kupitia kwa  Philippe Coutinho akipokea pasi nzuri
 kutoka kwa Raheem Sterling.
Lakini
 wenyeji walijibu mapigo katika dakika ya 31 baada ya beki wa kati na 
nahodha wa Man City, Vincent Kompany kuunganisha mpira wa kona 
uliochongwa Mhispania David Sliva.
Sherehe
 ya ushindi kwa City ilikuja dakika ya 45 baada ya mshambuliaji 
hatari Alvaro Negredo kufunga bao la pili kufuatia kazi nzuri ya Jesus 
Navas.
Huwezi
 amini mpaka saa 12 kasorobo jioni ya leo, Liverpool walikuwa kileleni 
mwa EPL, hivi sasa ni saa nne usiku wameporomoka mpaka nafasi ya nne 
katika msimamo na Arsenal wakirudi kileleni kama kawaida.
Kali zaidi wiki ijayo, Liverpool wataingia kwenye kibarua kizito dhidi ya vijana wa Jose Mourinho, klabu ya Chelsea ya London.
Baada ya mechi za leo, timu tano za juu ni kama ifuatavyo;
| Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts | 
| 1 | Arsenal | 18 | 12 | 3 | 3 | 36 | 18 | 18 | 39 | 
| 2 | Manchester City | 18 | 12 | 2 | 4 | 53 | 21 | 32 | 38 | 
| 3 | Chelsea | 18 | 11 | 4 | 3 | 33 | 18 | 15 | 37 | 
| 4 | Liverpool | 18 | 11 | 3 | 4 | 43 | 21 | 22 | 36 | 
| 5 | Everton | 18 | 9 | 7 | 2 | 29 | 17 | 12 | 3 | 
 
Raha duniani: Alvaro Negredo (kulia) akishangilia bao lake la ushindi kwa klabu yake ya Manchester City
Kikosi
 cha Man City usiku huu: Hart 7, Zabaleta 6, Kompany 7, Lescott 7, 
Kolarov 5, Y Toure 6, Fernandinho 7, Navas 8, Silva 7 (Garcia, 86), 
Nasri 6 (Milner 71, 6), Negredo 8 (Dzeko 76).
Kikosi
 cha Liverpool: Mignolet 6, Johnson 6, Sakho 7, Skrtel 6, Cissokho 5; 
Lucas 6 (Aspas, 81), Sterling 7, Henderson 7, Allen 6, Coutinho 6 
(Moses, 67), Suarez 7.
 
Shambulizi: Negredo akipiga mpira wakati Simon Mignolet  akijaribu kuokoa
 
Manyoya: Mignolet akijaribu kuokoa mpira uliotinga wavuni, huku Negredo (kushoto) akianza kushangilia
 
 
 
 
Kompany Mzuri: Nahodha wa City , Vincent Kompany (wa pili kushoto) akiruka juu na kupiga kichwa mpira uliozaa bao la kusawazisha
 
 
Akiruka
 kwa furaha: Samir Nasri (kulia)  akionesha furaha yake wakati kipa 
Mignolet akiwa amejipigia magoti kuugulia maumovu ya goli hilo
 
Anajua alichofanya: Mignolet  akijutia makosa yake yaliyosababisha Negredo afunge bao zuri na la ushindi
 
Chini
 na alitoka nje: Negredo akiwa amelala chini akiugulia maumivu ya mguu 
na alitolewa nje huku nafasi yake ikienda kwa mshambuliaji mwingine Edin
 Dzeko
 Kompany Mzuri: Nahodha wa City , Vincent Kompany (wa pili kushoto) akiruka juu na kupiga kichwa mpira uliozaa bao la kusawazisha
 
Kipaji cha juu: Kompany (katikati) akishangilia bao lake na wachezaji wenzake
 
Huendi mzee:  Joleon Lescott (kushoto) na  Luis Suarez wakigombania mpira
 
Anajiribu kutafuta njia: Suarez akijaribu kupasua njia pembeni ya  Lescott  huku  Yaya Toure (katikati) akiunga `traila`
 
 
Wawili jamani!: Jesus Navas (kushoto) na Pablo Zabaleta (kulia) wakiungana kumzuia Aly Cissokho
No comments:
Post a Comment