Mkurugenzi
 wa Doricas Aide International – Tawi la Tanzania, Bi. Stella 
Sozigwa(kushoto) akikabidhi Misaada ya Kibinadamu ya Wafungwa Waliopo 
Magerezani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja. 
Hafla fupi ya Makabidhiano ya Misaada hiyo imefanyika leo Desemba 27, 
2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
 Kamishna
 Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi 
wakati wa hafla ya kupokea Misaada ya Kibinadamu kwa Wafungwa waliopo 
Magerezani iliyotolewa na Asasi ya “New Life In Christ” leo Desemba 27, 
2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
  
Baadhi
 ya Askari wa Jeshi la Magereza wa Gereza Kuu Karanga – Moshi 
wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini,
 John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati wa Makabidhiano ya Misaada ya 
Kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani iliyotolewa na Asasi ya “New 
life In Christ”.
  
  
Aina
 mbalimbali ya Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa kwa Wafungwa waliopo 
Magerezani na Asasi ya “New Life In Christ”. Hafla ya Makabidhiano ya 
Misaada hiyo imefanyika leo Desemba 27, 2013 katika Viwanja vya Gereza 
Kuu Karanga, Moshi ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Kamishna Jenerali wa 
Magereza Nchini, John Casmir Minja.
 
 
Kamishna
 Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika 
picha ya pamoja na Viongozi Wawakilishi wa Asasi ya “New Life In Christ”
 mara baada ya kupokea Misaada ya Kibinadamu ya Wafungwa waliopo 
Magerezani (wa tatu kulia) ni Mwenyekiti wa New Life In Christ Mkoani 
Kilimanjaro, Bi. Elly Makyao(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Doricas 
Aide International – Tawi la Tanzania, Bi. Stella Sozigwa(wa tatu 
kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma 
Malewa( wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna 
Mwandamizi Msaidizi wa Magereza, Hamis Nkubasi na wa kwanza kulia ni 
Mratibu wa Huduma za Magereza toka Asasi ya “New Life In Christ”, Bw. 
Charles Shang’aa(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment