Mkurugenzi
  wa shule  ya kimataifa  ya  Southern Highlands Mafinga  Bi Mary 
 Mungai akimkabidhi  cheti mmoja kati ya  wahitimu wa mahafali ya 13 
 shule  hapo ,kulia  kwake ni kaimu meneja  wa Benk ya wananchi Mufindi 
(Mucoba) Bw Ben Mahenge 
 Walimu
 na  wafanyakazi wa shule ya Southern Highlands Mafinga  wakiwa katika 
 picha ya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Bi Mary Mungai 
kushoto wa kwanza .
 ……………………………………………………….
 Na Francis Godwin
 MAENDELEO
 mazuri  ya ufaulu  wa  wanafunzi  wa shule  ya kimataifa  ya Southern 
Highlands Mafinga mkoani Iringa iliyoisukuma benk  ya wananchi Mufindi 
(MUCOBA) kujitokeza kuunga mkono jitihada za  elimu  katika shule  hiyo .
 Ifahamike   kuwa  suala
 la motisha  kwa  walimu na  wanafunzi  wanaofanya  vema  katika 
masomo  yao  na walimu  wanaofundisha wanafunzi  hao  ni  moja na 
hamasa  kubwa  kwa  kuwawezesha  kufanya  vizuri  katika 
maendeleo  ya  elimu nchini.
  Yamekuwepo  malalamiko  mbali  mbali  kutoka
 kwa  wadau  wa  elimu nchini  ambao  wamekuwa  wakilalamikia maendeleo 
mabaya  ya  elimu nchini hasa kutokana na mazingira 
duni  ya  kufundishia malalamiko ambayo  serikali  kupitia  wizara 
ya  elimu na mafunzo  ya ufundi  imeendelea  kuyafanyia kazi
 Huku  wale  waliokuwa  wakibeza  shule  za
 kata   hivi  sasa  kuanza kuzipongeza shule  hizo  kutokana na baadhi 
ya  shule  hizo  kufanya  vizuri  kuliko shule  za 
awali  ambazo  walikuwa wakizisifia  na hapa ndipo tunaungana 
na  wahenga  waliosema kupanga ni  kuchagua .
 Pia  miaka  ya  hivi  karibuni  zimezuka   shule  nyingi  za
 sekondari  na msingi za  watu  binafsi ambazo 
baadhi  ya  shule  hizo  zimeendelea kufanya vizuri 
na  kutoa  changamoto  kubwa kwa  shule  za  serikali na baadhi  ya 
shule  zilizoanzishwa na watu binafsi zikionekana  kuendelea  kushuka 
zaidi  na  wazazi  hata  kuamua  kuhamisha   watoto  wao.
 Shule
 ya Southern Highlands Mafinga imeonekana kuivutia zaidi  benki hiyo ya 
MUCOBA  kutokana na rekodi  yake nzuri  ya kufaulisha vizuri wanafunzi 
wote darasa la saba tangu ilipoanzishwa mwaka 1997.
 Kiwango  cha  elimu  kinachotolewa
 katika  shule  ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga kinaisukuma 
benk ya  wananchi  wilaya ya  Mufindi (MUCOBA)   kuahidi  kutoa  kiasi  
cha  Tsh milioni 2.5  kwa  ajili ya  kuwafuingulia  akaunti  katika benk
 hiyo  wanafunzi  waliofanya  vema  matokeo ya  mtihani  huo  mwaka  
huu.
 Bw
 Ben Mahenge  anasema  kuwa  moja kati ya  sababu  iliyopelekea  benki  
yake kujitokeza  kuunga  mkono  jitihada za  shule  hiyo  ni  kutokana 
na ufaulu  mzuri  wa  mitihani  ya Taifa  ya  darasa  la  saba  ambayo 
shule  hiyo  imeendelea  kuongoza na  hivyo  kutoa  heshima kwa  wilaya 
 ya  Mufindi na Tanzania  kwa  ujumla.
 Kwani 
 anasema  kuwa  mbali ya  benk hiyo  kuendelea  kutoa  mikopo mbali 
mbali  ila imekuwa  karibu  zaidi na  shule  hiyo ya  Southern Highlands
 Mafinga  ambapo  mkurugenzi  wake Bi Mary A. Mungai  ni mmoja kati ya  
wateja  wakubwa  wa  benk  hiyo  kutokana na
 wazazi 
 wote  wanaosomesha  watoto  katika  shule hiyo  kulipia ada kupitia  
benk  hiyo hivyo  kiasi  hicho cha fedha  kilichotolewa na  MUCOBA ni  
kutambua mchango  wa  shule  hiyo katika  uendelezaji  wa  benk hiyo. 
 ”
 Kati ya  wateja  wakubwa  wa  benk  ya  MUCOBA ni  pamoja na  shule ya 
 Southern Highlands Mafinga na  wazazi ambao  wanasomesha  watoto hapo 
kutokana na   wazazi wa watoto  wanaosomesha  hapo  hulipa ada  kupitia 
 benk  yetu …..hivyo  kwa  ajili ya  kumpongeza  mkurugenzi  wa  shule 
hiyo kwa kuzidi  kuiunga mkono  benk  yetu  bado tunazidi  
kuwahamasisha  wananchi  wa  wilaya ya  Mufindi na nje ya  mkoa  wa  
Iringa kujiunga nasi”
 Mahenge 
 anasema  kuwa  benk hiyo  imeendelea  kutoa  mikopo  mbali mbali  kwa  
wateja  wake  ikiwemo mikopo ya  ujenzi  wa  nyumba  bora , ujasiliamali
 na mikopo  ya kuendeshea  biashara .
 Hata 
 hivyo  Mahenge  anasema  kuwa  wanafunzi  watakaonufaika na msaada  
huo  ni  yule  aliyefanya   vizuri katika matokeo  ya mtihami  wa  
Taifa  wa darasa la  saba pamoja na mwanafunzi Aida  Mhagama  ambae  
aliibuka  mshindi  wa  jumla katika masomo  mbali mbali  na  kupongezwa 
 wakati  wa  mahafali  ya  darasa  la  saba ya  shule  hiyo .
 Anasema 
 fedha  hizo  zitaingizwa katika akaunti   zao baada ya  kufunguliwa na 
 benk hiyo  kwa  lengo la kusaidia  kuwasomesha  elimu  ya  sekondari 
pindi watakaojiunga na  elimu  hiyo ya  sekondari mapema  mwakani .
 Mkurugenzi
 mtendaji wa shule  hiyo Bi Mary Mungai ambae amepata   kuwa 
afisa  elimu shule za msingi anasema  kuwa shule  imekuwa  ikifundisha 
kwa kiingereze, yaani english medium school, imefaulisha tena mwaka  huu
 2013 wahitimu wote wa darasa la saba na kuiwezesha kuwa katika asilimia
 mbili (2%) ya juu ya shule zote zenye kufaulisha vizuri kitaifa, na 
katika 10 bora kati ya shule 449 za mkoani Iringa.
 “…Tunawapa
 hongera wahitimu hao na kuwatakia maendeleo mazuri kokote waendako. 
….pia tunawapongeza wazazi/walezi, tunawatakia kila la heri kuwaendeleza
 watoto wao kufuatia msingi huu ulio bora waliopata kutoka Southern 
Highlands School.
 Anasema
 pia uongozi  wa shule  hiyo hautaacha  kuwapongeza walimu, kwa kazi 
kubwa wanayoendelea kuifanya kila siku kuhakikisha wanafunzi wanapata 
elimu iliyo ya kiwango cha juu.
 “
 Sisi  tunapokea watoto  kutoka pande zote za nchi  na 
watakaotaka  watoto wao wajiunge na Southern Highlands School, nafasi 
zipo kwa wanafunzi wa chekechea, darasa la 1, 2, 3, na 5 kwa wanafunzi 
wote na darasa la 4 na la 6 kwa wanaotoka shule za English Medium
 Anasema  kuwa  toka  shule  hiyo  ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya  vizuri na hakuna mtoto aliyepata  kufeli .
 “Shule  yetu
 mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na 
wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa 
kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza”
 Anasema katika  matokeo
 ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School 
ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza.
 “  
 Tulimshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye. Kwa kuwezesha watoto
 wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo” 
alisema Bi Mungai
 Hata  hivyo  anasema kila mwaka wanafunzi wote  wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari.
 “mwaka  huu
 tena  wanafunzi wote wa darasa la saba 47 waliomaliza mwaka huu 2013, 
wamefaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari”
 Mwenyekiti  wa bodi ya shule  hiyo Bw Omary Mahinya anasema kuwa katika moja ya vielelezo kuwa shule  hiyo ni bora nchini ni wazazi kutoka mikoa karibu yote ya Tanzania kupeleka  watoto wao hapo .
No comments:
Post a Comment