Juma
 Kaseja `Tanzania One` amekingiwa kifua na bosi wake ,Yussuf Manji baada
 ya kufungwa mabao matatu jana kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe
MWENYEKITI
 wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji amemkingia kifua mlinda mlango wao 
mpya, Juma Kaseja baada ya kufungwa mabao matatu jana akiwa langoni 
katika mchezo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya watani zao wa jadi, Simba Sc 
ambao Mnayama alishinda 3-1.
Mbao 
ya Simba sc katika mechi ya jana yalifungwa na Amis Tambwe aliyepiga 
mawili na kiungo Juma Awadh Issa, wakati la Yanga lilifungwa na Emmanuel
 Okwi.
Akizungumza
 leo na waandishi wa habari, Manji amasema hawakumsajili Kaseja kwa 
ajili ya kuifunga Simba SC, bali malengo yao ni kupata msaada wake 
katika michuano mikubwa ya soka barani Afrika.
Baada
 ya Yanga kufungwa jana, huku Kaseja akiwa langoni, katibu mkuu wa 
baraza la wazee la klabu hiyo, Mzee Ibrahim Akilimali, iliulaumu uongozi
 kwa kusema kuwa  usajili wa kipa huyo ni makosa na hauna baraka zao.
Manji
 amejibu mapigo na kueleza kuwa umri unazidi kumtupa mkono mzee 
Akilimali  kwani ameshindwa kukumbuka kuwa , huyo Ivo mwenyewe aliondoka
 Yanga akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita na uongozi wa 
wakati huo kwa tuhuma za kufungisha kwenye mechi dhidi ya  Simba SC.
Pia 
Manji alihoji wakati Simba ikisawazisha mabao yote matatu  katika mchezo
 wao wa ligi kuu soka Tanzania bara oktoba 20 dhidi ya Simba sc , Kaseja
 alikuwa langoni?.
Mwenyekiti
 huyo alisema  si jambo zuri kulaumiana pale yanapotokea makosa, bali ni
 kuwa na mshikamano kwa ajili ya maendeleo ya Yanga.
“Tunaheshimu
 uwezo wa Kaseja, thamani yake ni kubwa. Hakuna kipa yeyote nchini 
aliyedaka mechi nyingi za kimataifa kama kipa huyu. Kamwe hatuwezi 
kumshusha thamini yake na uwezo wake kwa kufungwa mabao matatu kwenye 
mechi ya jana ambayo ilikuwa sawa na bonanza tu”. Alisema Manji.
Manji
 alisema mechi ya jana walicheza kumfurahisha mdhamini wao, TBL, lakini 
haikuwa na maana yoyote na matokeo ya kufungwa wala hayajawaingia 
akilini.
Hata hivyo Manji amewapongeza Simba SC kwa kucheza soka safi, hivyo walistahili ushindi katika mchezo wa jana.
 Kuelekea
 ngwe ya lala salama ya ligi kuu na michuano ya Kimataifa , Manji 
alisema wataboresha timu pamoja na benchi la ufundi  kwa tafsiri ya 
kuwaondoa makocha wao Ernie Brandts na wasaidizi wake, Mzawa Fredy Felix
 Minziro na Mkenya, Mkenya Razack Ssiwa 
“Timu
 itaenda tena Ulaya kuweka kambini kama walivyofanya waka jana. Naamini 
tutajivua vizuri na kuwa makali zaidi kutetea ubingwa wetu na kufanya 
vizuri michuano ya kimataifa”. Alisema Manji.
Ili 
kuongeza makali, Yanga imesajili wachezaji watatu katika dirisha dogo la
 usajili ambao ni mlinda mlango, Juma Kaseja, kiungo Hassan Dilunga na 
mshambuliaji mahiri raia wa Uganda, Emmanuel Anord Okwi.
Wachezaji hao walitumika jana, lakini hawakufua dafu mbele ya kikosi cha Simba Sc kilichoonekana kuwa bora zaidi Yanga.

No comments:
Post a Comment