“PRESS RELEASE” TAREHE 27.12. 2013.
WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU  KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
 TAREHE 26.12.2013 MAJIRA YA SAA 20:10HRS HUKO ENEO LA KATUMBA, KATA YA 
KATUMBA, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA, BARABARA YA 
MBEYA/TUKUYU. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE  
LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AMANI S/O ABILIA, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA,
 MKAZI WA KIJIJI CHA KATUMBA NA  KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. 
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA 
TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU. 
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI 
BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI HASA 
KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA KWA KUZINGATIA SHERIA NA 
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. 
AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA
 TUKIO HILI AZITOE KWENYE MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE 
MKONDO WAKE. 
[B.N.MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:
Post a Comment