Jeneza
 lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu James 
Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa heshima 
za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili, Dar es 
Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani Muheza, Tanga
 kwa mazishi yatakayofanyika kesho. 
 Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe
Aliyekuwa
 Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, (kushoto) 
akijadiliana jambo na Benny Kiska  mdogo wa marehemu wakati wa kutoa 
heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka. 
Mjane
 wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa pili wa
 marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho.
 Ndugu wa karibu wa marehemu Kisaka akilia alipokuwa akitoa heshima za mwisho 
 Mtoto wa mwisho wa marehemu Kisaka, Christopher akitoa heshima za mwisho
 Mwenyekiti
 wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania ambaye pia ni 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma 
Pinto (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba,
 Hassan Dalali. 
 Wachezaji
 soka wa zamani wakijadiliana jambo nje ya Kanisa la Muhimbili 
walipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
 Kutoka kushoto ni Madaraka Selemani, Peter Tino, Khamis Kinye, Bakari 
Malima na Thomas Kipese. 
Aliyekuwa
 Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, (kushoto) 
akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa 
heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka. 
Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu James Kisaka akisoma wasifu wa marehemu kakake
 Msanii wa filamu Jacob Steven JB akitoa heshima za mwisho
 Mchezaji wa zamani wa Simba Malota Soma akitoa heshima za mwisho kwa mchezaji mwenzie marehemu Kisaka.
 Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula akitoa heshima za mwisho
Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu, akitoa taarisha ya usafiri wa kwenda kwenye msiba baada ya kutoa heshima za mwisho.
 
 
No comments:
Post a Comment