Baadhi
 ya wachezaji wa timu ya Taifa wa ngumi za Ridhaa pamoja na wadau 
wengine wa mchezo huo katika Picha ya pamoja, wakati wa hafra hiyo 
 Aliyesimama
 kushoto ni mkurugenzi wa Afrika Mashariki kupitia kinywaji cha Battery 
Bwana Tony Misokia akiwa anaongea na wananchi walioshiriki katika Hafra 
hiyo.
 Kutoka
 kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania 
(BTF) Bwana. Lukelo  Anderson akiwa sambamba na Afisa habari wa Ngumi za
 ridhaa Tanzania  Bwana Salum Viduka wakati wa Hafla hiyo. 
 Hawa ni Baadhi ya wachezaji wa  Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF)
 Wa kwanza kulia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ngumi za ridhaa Tanzania bwana Nassari Mafuru 
 Kutoka
 kushoto aliyevaa shati jeupe ni Bwana Anthon Mwang’onda ambaye ni 
mjumbe wa mashindano na vifaa wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania 
(BTF) akiwa na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Bwana Hassan Mzonge 
Shirikisho
 la ngumi za ridhaa Tanzania  limefanya hafla fupi iliyojumuisha 
wachezaji wa ndondi , makocha wadau na Vyombo vya habari kwaajili ya 
kuendeleza  mshikamano wa kuweza kuwainua vijana ambao bado
hawajaweza kupata ajira kujiunga na shilikisho la ngumi za ridhaa Tanzania
hawajaweza kupata ajira kujiunga na shilikisho la ngumi za ridhaa Tanzania
Shilikisho
 hilo ambalo limeanzisha mashindano ambayo yanatambulika kwa jina la  
PSPF  Boxing Award sambamba na wadhamini wa mashindano hayo waliandaa 
hafla hiyo  iliyofanyika katika eneo la   (CnG) ambapo waliweza 
kudhamini kwa kuandaa chakula cha usiku kwaajili ya kuendelea kuweka 
mahusiano baina ya washiriki wote wanao shiriki katika kuendeleza mchezo
 wa ngumi Tanzania 
Akizungumzia
 lengo la kuweka hafla  hiyo Afisa habari wa shirikisho la ngumi 
Tanzania Bw.Salum Kuhowa Viduka amesema “Tunawaomba wanajamii kuweza 
kutupa ushirikiano kwa muda wote ambao mashindano haya  huwasili katika 
miji,wilaya, manispaa, nk kuweza kujitokeza kwa wingi ili kuona jinsi 
fursa kwa vijana zinavyo patikana kupitia mchezo wa ngumi za Ridhaa”
Mwisho
 Makamu Rais  Bw.Lukelo Andason aliweza kufunga hafla hiyo kwa 
kuwapongeza watu wote walio weza kufika na kujumuika pamoja ili 
kuendeleza kujenga umoja wa ngumi Tanzania.
No comments:
Post a Comment