Lango
 kuu la kuingilia kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar 
panapofanyika shindano kali la kusaka kipaji cha SUPA STAA wa watoto na 
vijana! la “MO Kids Got Talent 2013″
.Wazazi wahamasishwa kujitokeza kwa wingi, kuona vipaji vya watoto wao.
.Fainali kuanza saa kumi na moja jioni
 Chief
 Judge wa Shindano la vipaji vya watoto na vijana wadogo la “MO Kids Got
 Talent”, Salma Mziray, akitoa maoni yake kwa baadhi ya washiriki 
walioingia semi finals za shindano hilo linalofanyika kwenye hotel ya 
Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji Neema 
Theobald na kushoto ni msanii wa filamu nchini Hidaya Njaidi wakiwa meza
 kuu.
Sehemu
 ya zawadi zilizotolewa kwa watoto walioshiriki kwenye usaili wa 
shindalo la “MO Kids Got Talent 2013″ ambapo fainali zake zinafanyika 
leo kuanzia saa Kumi na moja jioni ndani ya Hoteli ya Ledger Plaza 
Bahari Beach jijini Dar.
Pichani
 juu na chini ni baadhi ya kati ya watoto 15 wakionyesha vipaji vyao 
kwenye semi finals za shindano la kusaka vipaji kwa watoto na vijana la 
“MO Kids Got Talent” lililoandaliwa na Kampuni ya Frost Africa na 
kudhaminiwa na kampuni ya MeTL Group, ambapo leo jioni kutafanyika 
fainali za mashindano hayo kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach 
jijini Dar na mshindi kujinyakulia fedha taslim shilingi Milioni 5 za 
Kitanzania.
Mambo ya Sugua Gaga hayo…… Wapi Shaa….??? Kipaji hicho…!!!
 Sehemu ya watoto wakionyesha vipaji vyao vya aina mbalimbali ikiwemo kucheza, kuimba na vingine kibao.
 Kipaji cha mchezo wa Karate pia kilikuwepo.
Sehemu ya watoto wakisubiria kuingia kwenye chumba maalum kuonyesha vipaji vyao. 
Afisa
 Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko akigawa zawadi 
zilizotolewa na MeTL Group pamoja na kupata picha ya kumbukumbu kwa 
washiriki waliojitokeza kwenye usaili wa shindano la “MO Kids Got 
Talent” ambapo fainali za shindano hilo zitafanyika leo kuanzia saa kumi
 na moja jioni kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar.
Afisa
 Mtendaji Mkuu wa Frost Africa ambao ndio waandaji wa shindano la “MO 
Kids Got Talent” Bw. Peter Sekasiko, katika picha ya pamoja na 
Operations Manager wa MOblog, Zainul Mzige na Mwandishi wa Gazeti la 
Nipashe, Enles Mbegalo.























No comments:
Post a Comment