Moja ya Kikosi cha JKT Ruvu ya Pwani katika mechi za nyuma. Picha Maktaba
Timu 
za Ligi Kuu za Ashanti United na JKT Ruvu Stars zinapambana Januari Mosi
 mwakani kati moja ya mechi za kujaribu matumizi ya tiketi za 
elektroniki kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamzi, Dar es Salaam.
Viingilio
 katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 1,000 na sh. 
2,000 ambapo tiketi zinapatikana kupitia M-Pesa na mawakala wa CRDB 
Fahari Huduma. Tiketi zitaendelea kuuzwa hadi kipindi cha kwanza cha 
mechi hiyo kitakapomalizika. 
Mawakala
 18 wa Fahari Huduma wanaouza tiketi hizo ni ABC Computer- Mtaa wa 
Samora, Abraham Anangisye Mwampetele- Maji Matitu, Apex Security 
Services- Mtaa wa Mibega, Kinyerezi, Athuman Fakhi Adam- Kongowe 
Mbagala, Fedha Investment Limited- Pamba Road na Fuya Godwin Kimbita- 
Tegeta Block.
Ghomme
 Health & Education Limited-Bahari Beach, Herman Arbogast Tarimo- 
Kigamboni, K- Finance Limited- Shekilango, Sinza, Koli Finance Limited- 
Mtaa wa Samora, LB Pharmacy- Mtoni Kijichi, Lista Phares Barnabas- 
Tabata Segerea na Maly Investment Company Limited- Mtaa wa Sikukuu, 
Kariakoo.
Wengine
 ni Micu Enterprises- Mtaa wa Congo, Kariakoo, S&D Collection 
Company Limited- Mikocheni, Shoppers Plaza, Therry Investment Limited- 
Tegeta Kibaoni, TSHS Distributors Limited- Mtoni kwa Aziz Ali na 
Wemerick Independent Vehicle- Mtaa wa Boko.
Pia 
mshabiki anaweza kununua tiketi kwa njia ya simu- mtandao wa Vodacom kwa
 kupiga *150*03*02# ambapo atapata namba atakayoitumia kufanya malipo 
kupitia MPESA. Katika MPESA namba ya malipo kwa TFF ambayo ndiyo 
mshabiki ataitumia kufanya malipo ya tiketi (business number) ni 888800.
 Vilevile mteja wa CRDB aliye katika mtandao anaweza kufanya malipo 
kupitia CRDB simbanking.
Baada
 ya kufanya maombi kupitia njia yoyote ya hizo tatu; MPESA, Fahari 
Huduma na CRDB simbanking, mshabiki atapata namba ambayo ataitumia 
ku-print tiketi yake kupitia mashine maalumu za kuchapia Tiketi ya TFF 
zilizo katika ATM za CRDB kwenye maeneo yafuatayo;
Benki
 ya CRDB tawi la Azikiwe, tawi la Holland House ambapo kuna mashine 
mbili, tawi la Vijana, tawi la Kariakoo, ATM ya Mtaa wa Shaurimoyo 
ambapo kuna mashine mbili na ATM ya CRDB iliyoko kituo cha mafuta cha 
Kobil Sabasaba, Mtoni kwa Aziz Ali.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF

No comments:
Post a Comment