| 
 
Na Francis Godwin Blog
JESHI la  polisi  mkoa  wa 
 Iringa  limewakamata  watu  wawili  akiwemo  dereva  wa tenki  la 
 mafuta  lenye namba za usajili  T 247 BHP  wakisafirisha shehena  ya   
vipodozi maboksi 779 vikiwa vimewekwa ndani ya tenki  hilo la mafuta 
 kutoka nchi  za  kusini  mwa Tanzania  kuelekea  jijini  Dar es Salaam . 
  
Kamanda
  wa  polisi wa mkoa  wa  Iringa Ramadhan  Mungi  alisema  kuwa  lori 
hilo lenye namba za usajili  T 247 BHP  likiwa na tela  lenye namba T 
598 BMK   ni mali ya kampuni ya  World OIL Ltd  ya  Jijini Dar es Salaam
 lilikuwa  likiendeshwa na  Mohamed  Sadru (23) mkazi  wa  Mbezi Temboni
 jijini  Dar es Salaam . 
  
 Mbali
  ya  dereva   huyo  pia  jeshi  hilo  linamshikilia mfanyabiashara 
 aliyekuwa akisafilisha  mzigo  huo  Bw Kassim Kaifa (23) mkazi  wa 
jijini Dar es Salaam  kwa tuhuma  za  kuhusika na mzigo  huo. 
  
Kamanda
 Mungi  aliwaeleza  wanahabari  leo    kuwa  mtego wa jeshi  la  polisi 
 uliweka  baada ya  kupokea  taarifa  kutoka kwa rai  wema kuhusiana na 
lori  hilo kutumika isivyo  kwa kusafirisha vipodozi  hivyo. 
  
Alisema
  kuwa  taarifa  kuhusiana na lori  hilo kusafirisha vipodozi  badala ya
  mafuta   waliitapata  kutoka  jana  na mtego  wa  kulikamata  lori 
hilo  umefanikiwa majira ya saa 9 alfajiri  ya leo  
  
Hata
   hivyo  alisema  kuwa  sehemu  kubwa ya  vipodozi  hizo   ni  vile 
 ambavyo vilipigwa marufuku na  serikali kutokana na kuwa na madhara 
 makubwa kwa afya  ya  watumiaji  wa vipodozi  hivyo. 
  
Alisema
  kuwa  jeshi la  polisi  limefanikiwa  kumata  vipodozi hivyo kwa 
 kushirikiana na mamlaka ya  chakula na  dawa ,wakala  wa  barabara 
 mkoa  wa Iringa  na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)  
  
Kamanda
 huyo  alisema kuwa  watuhumiwa hao   watafikishwa mahakamani  mara 
 baada ya  uchunguzi  kukamilika na  kuwa ni mapema  kwa  sasa  kuitaja 
thamani  ya vipodozi  hivyo na  nchi  ambayo lori  hilo  lilikuwa 
 likitoka kutokana na sababu  za kiusalama. 
 | 
No comments:
Post a Comment