TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 18, 2015

Ziara ya Waziri Simbachawene Mtwara na Lindi

chaw1Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda (aliyesimama), akiwasilisha taarifa fupi ya hali ya mmomonyoko wa ardhi uliosababisha mazingira ya hatari kwa Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom Tanzania (M&P), kilichopo Mnazi Bay – Mtwara. Wanaosikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kutoka Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (katikati), na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini walioongozana na Waziri.
chaw2Baadhi ya nyumba wanazoishi wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara
chaw3Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka Kulia) akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Pamoja naye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (Kushoto – sambamba na Waziri) na Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (Kulia kwa Waziri.
chaw4Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka kushoto) wakati akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
chaw5Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
chaw6Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akikagua sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mwanzoni mwa wiki mkoani humo.
chaw7Matanki ya kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali, yaliyopo katika eneo la Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Katika ziara yake mtamboni hapo, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene aliagiza maji hayo yatumike pia kuwasaidia wananchi wanaoishi maeneo jirani.
chaw8Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara yake Mtamboni hapo mwanzoni mwa wiki.
chaw10 chaw11Baadhi ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi huo mwanzoni mwa wiki. chaw12Baadhi ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi huo mwanzoni mwa wiki.
chaw13Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba mkoani Mtwara. chaw15Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akijadili jambo na mmoja wa wasimamizi wa Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara, wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua maendeleo ya Mradi.
…………………………………………………………………..
* Aahidi umeme kwa wana-Msimbati Na Veronica Simba Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amefanya ziara mkoani Lindi na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara yake ambapo aliahidi huduma za umeme na maji kwa wananchi mbalimbali. Akiwa Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi, Waziri Simbachawene alimwagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo. “Kutokana na taarifa yenu, mtakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha hapa. Pamoja na matumizi yenu mbalimbali, hakikisheni mnatoa huduma ya maji kwa wananchi wanaozunguka mtambo,” alisema Waziri. Vilevile, Waziri Simbachawene alitoa ahadi ya umeme kwa Kijiji cha Luvula kilichoko Msimbati. Alisema Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na Kiwanda cha kufua umeme cha Mnazibay, vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. “Tunaendelea na zoezi la kusambaza umeme nchi nzima. Lengo letu ni kuhakikisha idadi ya watanzania wanaopata umeme inaongezeka zaidi na zaidi ili kuwezesha lengo la nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama dira ya maendeleo inavyoonesha,” alisema. Ziara hiyo ya Waziri Simbachawene, ni ya kwanza kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara tangu aliposhika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati na Madini, Januari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment