TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, February 20, 2015

Wasanii wa nje na miaka 15 ya Tamasha la Pasaka

images 
Na Mwandishi Wetu
 
MSAMA Promotion kwa mara nyingine tena imeandaa Tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu litakalofanyika wakati wa sikukuu ya Pasaka katika mikoa tofauti hapa nchini.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama anasema kwamba tamasha hilo mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa ukilinganisha na matamasha mengine yaliyopita, kwani limeboreshwa zaidi na watakuwa wanafurahia miaka 15 tangu lianzishwe.
 
“Kwanza kabisa tofauti na matamasha yaliyopita, mwaka huu tutakuwa na waimbaji wengi zaidi wa muziki wa Injili kutoka nchi za nje.
 
“Kutakuwa na waimbiaji kutoka Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na nje ya Afrika, ambapo lengo kubwa ni kulifanya tamasha hili kuwa na utofauti,” anasema.
 
Moja ya maboresho makuwa katika miaka 15 ya Tamasha la Pasaka la mwaka huu Msama amesema kwamba litakuwa na kiingilio rahisi zaidi ili kila mmoja aweze kuhudhuria na kupata baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu.
 
“Waimbaji wote maafuru wa muziki wa Injili watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakiksha kwamba tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali,” anasema.
 
Anasema kutokana na ukumbwa na maboresho mazuri zaidi ya tamasha hilo, kamati ya maandalizi imewashirikisha watu 100, wakiwa ni wachungaji na Wainjilisti.
 
ED_003124_564364598Anasema lengo kubwa la kuwashirikisha wachungaji na Wainjilisti ni kwa sababu watu wengi waweze kubarikiwa kiroho kwa kuwa tamasha hilo ni la kumsifu Mungu.
 
“Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho.
 
“Tutaheshimu mno maoni ya wapenzi wa tamasha hili kutoka sehemu mbalimbali na kila watakalotushauri tutalifanyia kazi, lengo kubwa lilikuwa n kiboresha tamasha letu,” anasema.
 
Mwaka huu Tamasha la Pasaka linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam na limekuwa likijiongezea umaarufu na kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya maadhimisho ya Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa kiroho kupitia matamasha hayo.
 
Umaarufu wa matamasha hayo pamoja na mambo mengine, unatokana na ukweli kuwa yamekuwa yakifanyika kwa ubunifu na umakini mkubwa huku kila mwaka yakiongezeka na kubadili waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi.
 
Baadhi ya nyota waliowahi kutumbuiza katika matamasha hayo ni marehemu Angela Chibalonza kutoka Kenya, ambaye naye aliwahi kutikisa.Baadhi ya nyimbo zake zilizotikisa na kukonga nyoyo ni Yahwe Uhimidiwe na Uliniumba Nikuabudu.
 

Wengine walioweka historia nchini ni pamoja na Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini. Mwimbaji huyo alivunja rekodi ya waimbaji wote licha ya kuwa hafahamu lugha ya Kiswahili vilivyo, lakini aliweza kuimba nyimbo kadhaa za Kiswahili kama Mwambamwamba ili kwenda sawa na Watanzania aliokonga nyoyo zao kwa kuwapa neno la Mungu kupitia muziki wa Injili.
 
Sipho Makhabane, Rebeka Malope nao kwa nyakati tofauti, walifanya vizuri ukiachilia mbali waimbaji wengine kama Ephraim Sekeleti kutoka Zambia, Ambassadors of Christ (Rwanda), Faraja Ntaboba na Solomoni Mukubwa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), 24 Elders  (Uganda) na Anastazia Mukabwa (Kenya).
 
Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).
 
Kwa upande wa Mukubwa ambate ametamba sana na wimbo wa Mfalme wa Amani amepata kutamba katika tamasha hilo na albamu mbalimbali ikiwemo ya Usikate Tamaa yenye nyimbo kama Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo,  Usikate Tamaa, Moyo Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri.Pia ana albamu nyingine mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu. Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio. Albamu yake ya pili ya Mungu Mwenye Nguvu ina nyimbo za Mungu Mwenye Nguvu, Mkono wa Bwana, Mfalme wa Amani, Siku Moja, Tabia Ina Dawa na Roho Yangu Ikuimbie.
 
Pia yupo msanii, Solly Mahlangu ‘Obrigado’ wa Afrika Kusini ambaye ingawa alitumbuiza Tamasha la Krismasi, lakini amekuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki.
 
Mahlangu ni muimbaji ambaye anashika kasi katika anga ya muziki wa Injili Afrika ambaye pia anamudu kuimba Kiswahili kizuri kwa  baadhi ya nyimbo zake.
 
Mbali ya kuwa maarufu katika nyimbo za Iinjili nchini mwake, pia ni Mchungaji ambaye ana uwezo wa kufanikisha muziki wa Injili na kanisa lake ambalo ni Word Praise Christian Centre Intenational lililoko Tembisa.

No comments:

Post a Comment