TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 17, 2015

Ugiriki iko tayari kunusuru uchumi wake

Waziri wa Fedha wa Ugiriki Yanis Varoufakis
Serikali ya Ugiriki imeleezea imani yake kwamba mkataba kuhusu madeni yake, utafikiwa ndani ya saa arobaini na nane, licha ya kupinga muda wa mwisho uliowekwa na nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro.
Mkutano wa mawaziri kutoka nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro waliokutana mjini Brussels, Ubalegiji ulivunjika mapema kuliko ulivyotarajiwa wakati serikali ya Ugiriki kutupilia mbali fursa iliyotolewa kwa nchi hiyo hadi Ijumaa kuhusu mpango wa nchi hiyo kudhaminiwa, au kuona mipango ikiisha kufikia mwishoni mwa mwezi huu.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya serikali ya Ugiriki vinasema pendekezo la nchi za ulaya ni "upuuzi" na "halikubaliki".
Lakini waziri wa fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis, amesema Ulaya itafanya "ulaghai uliozoeleka" kwa kutumia mkataba usio na ufumbuzi wa hali iliyopo.

No comments:

Post a Comment