TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 16, 2015

ATCL yazindua ndege nyingine mpya aina ya CRJ - 100

 Abiria wakishuka toka kwenye ndege mpya ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-100 yenye uwezo wa kubeba abiria 50 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakitoa mkoani Kigoma. Huo ukiwa ni mkakati wa kimaendeleo wa shirika hilo katika kuongeza idadi ya ndege na safari zake. Picha na mpiga picha wetu.
Meneja wa Air Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Bw James Mbago akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-100 yenye uwezo wa kubeba abiria 50, mara baada ya ndege hiyo kutua ikitokea mkoani Kigoma. Huo ukiwa ni mkakati wa kimaendeleo wa shirika hilo katika kuongeza idadi ya ndege na safari zake

SHIRIKA la ndege la Taifa (ATCL) mwishoni mwa wiki iliyopita lilizindua ndege yake mpya aina ya CRJ-100 yenye uwezo wa kubeba abiria 50 ikiwa ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kuongeza idadi ya ndege zake sambamba na kuongeza idadi ya safari zake.

Shirika hilo ambalo kwa sasa linalotoa huduma zake katika mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Mtwara na visiwa vya Komoro limejipanga kufanya safari za kila siku kati ya mikoa ya Dar es Salaam na Kigoma huku pia likiwa tayari kufanya safari za Mtwara na visiwa vya Komoro mara sita kwa wiki katika siku za Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam mara tu baada ya ndege hiyo kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Meneja wa shirika hilo katika kiwanja hicho, James Mbago alisema ndege hiyo imekodiwa kutoka nchini Afrika Kusini kwa jitihada za Serikali ya Tanzania na sasa ipo tayari kuwahudumia wateja wa shirika hilo.

“Kuja kwa ndege hii kunaongeza idadi ya ndege zetu hadi kufikia mbili na tunashukuru kuona kwamba imepokelewa vizuri na abiria wetu. Ndege yetu nyingine aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 kwa sasa inapata matengenezo makubwa kwenye karakana yetu iliyopo hapa hapa uwanja wa ndege,’’ alisema Mbago.

Kwa mujibu wa Mbago kupona kwa ndege hiyo inayofanyiwa matengenezo kiwanjani hapo kutalifanya shirika hilo lianzishe tena  safari zake za ndani kwa mikoa ya Mwanza, Tabora, Arusha na Mbeya.

“Muda si mrefu mambo yatakuwa mazuri zaidi…inafurahisha zaidi tunapopata mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wetu wanaofurahia huduma za shirika lao mama,’’ aliongeza Mbago. Zaidi, Mbago aliongeza kuwa shirika lake linatarajia ongezeko kubwa la abiria kutokana na ukweli kuwa ndege yao hiyo mpya ina uwezo wa kusafiri kwa haraka zaidi ikilinganishwa na ndege nyingine huku safari zake zikiambatana na huduma nzuri inayotolewa kwa wateja wake.

Wakizungumza mara tu baada ya kushuka kwenye ndege hiyo, baadhi ya abiria waliotoka Kigoma walisema licha ya kutumia muda mfupi zaidi lakini pia walifurahia huduma nzuri walizozipata kutoka kwa wahudumu wa ndege hiyo.

“Kwa kweli hii ilikuwa ni moja ya safari zangu za ndege ambayo nimeifurahia sana. ATCL wanahitaji pongezi kwenye hili na zaidi wafikirie kuboresha huduma zaidi ya hapa…sisi abiria tupo tayari kuwaunga mkono kwa sababu ndio wanabeba nembo ya taifa letu,’’ alisema mmoja wa abiria hao aliyejitambulisha kwa majina Gaudence Kashoka.

No comments:

Post a Comment