TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 16, 2015

Tamasha la Pasaka lasambaa mikoa 17

34
Na Mwandishi Wetu
IDADI ya mikoa ambayo imeomba iandae onesho la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka sasa imefikia 17, waandaaji wamesema.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama ilisema kuwa idadi hiyo ni kubwa na haijawahi kutokea tangu walipoanzisha tamasha lao mwaka 2000.
“Tumepokea maombi ya wadau kutoka mikoa 17 wakitaka tupeleke Tamasha la Pasaka mikoani kwao. Tunachofanya kwenye kamati yangu ni kupokea maoni kwa njia mbalimbali kwa wadau wetu wa huko.
 “Lakini si kupendekezwa au kuombwa tu na wadau ndiyo kigezo cha kupewa nafasi, lazima tuangalie na mazingira ya mkoa husika katika mambo ya matamasha,” alisema Msama.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Morogoro, Rukwa,  Mara, Singida, Arusha, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga, Dar s Salaam, Mtwara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Kilimanjaro na Zanzibar.
Alisema kamati yake inatarajia kukutana Jumatano wiki hii na kufanya tathmini ya maombi kwa wadau wao wa maeneo hayo ili kupata mikoa sahihi ambayo tamasha hilo litafanyika mwaka huu.
Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Krismas kila mwaka, lakini wanataka Tamasha la Pasaka mwaka huu liwe bora zaidi kwa sababu wanasherehekea miaka 15 tangu waanzishe tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment