TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 17, 2015

Maisha ya Albino mashakani Tanzania

Watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania
Nchini Tanzania kumetokea mkasa mwingine kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, albino kutekwa katika wilaya ya Chato mkoa wa Geita, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Polisi wameeleza kuwa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Yohana Bahati mwenye umri wa mwaka mmoja alitekwa nyumbani kwao na watu wasiojulikana jana usiku.
Kwa mujibu wa taarifa za mwandishi kutoka eneo hilo Renatus Masuguliko, polisi wamefika eneo la tukio na kuanza msako mkali dhidi ya watu wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho.
Habari zinasema watu waliokuwa na silaha za jadi waliwaweka chini ya ulinzi Bahati Misalaba na mkewe ambao ni wazazi wa mtoto albino ambaye walimteka na kutoweka naye.
Familia hii pia ina watoto wengine wawili wenye ulemavu wa ngozi, Tabu Bahati mwenye umri wa miaka miwili na Shida Bahati mwenye miaka kumi na mmoja ambao walinusurika kuchukuliwa na watu hao kwa sababu wakati unyama huo ukitendeka nyumbani kwao hawakuwepo walikwenda kucheza kwa majirani zao.
Mama wa mtoto huyo alijeruhiwa vibaya wakati akimpigania mtoto wake asichukuliwe na watu hao.

No comments:

Post a Comment