TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 17, 2015

Mfumo wa Mtandao wa Upatikanaji Taarifa za Ardhi Zanzibar kuzinduliwa

08
Balozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Sinnika Antilla.
==============================================
Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar
Idara ya Ardhi na Mazingira inatarajia kufanya Uzinduzi wa Mfumo wa Mtandao wa Upatikanaji Taarifa za Ardhi
r (Zanzibar Land Information Service) (ZALIS) itakayosaidia upatikanaji wa taarifa sahihi za Ardhi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara hiyo uzinduzi huo utafanyika siku ya Jumatano ya tarehe 18/02/2015 katika jengo la Ardhi liliopo Forodhani Mjini Zanzibar.
Kwa mujibu taarifa hiyo imesema mtandao huo wenye teknolojia rahisi itakayosaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa habari na taarifa zote za Ardhi ikiwemo usajili, utambuzi, upimaji, uhaulishaji eneo, kijografia, mipaka na kuongeza ufanisi wa shughuli zote ardhi kwa kiasi kikubwa.
Sambasamba na hayo taarifa hiyo imeeleza kuwa mfumo wa ZALIS utarahisisha upatikanaji wa taarifa na takwimu zinazohitajika Kijamii na Kiuchumi juu ya masuala ya Ardhi na kuzifanya shughuli hizo kuwa rahisi na nyepesi zaidi.
Aidha Serikali ya Finland kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nchi za Nje imekuwa ikiisaidia Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo Maji, Mazingira, Misitu pamoja na Ardhi kwa zaidi ya miaka 10 hadi sasa.
Taarifa hiyo imefahamisha kuwa Shughuli za usajili wa Ardhi zilizinduliwa rasmi mnamo mwaka 2013 na Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein zikiwa zinaendelea vizuri nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo imeeleza maendeleo ya usajili wa Ardhi yamekuwa yakiendelea vizuri nchini ambapo hadi sasa jumla ya vikataa 34,000 vimeshapatiwa  usajili wa kudumu Zanzibar.
Taarifa hiyo imesema hadi sasa tayari kumeshaanzishwa Sera ya Taifa ya Ardhi, Mkakati wa Kitaifa wa Maendeleo ya Matumizi ya Maeneo ya Ardhi, Mipango Kimkoa Kaskazini na Kusini, Upitiaji wa Sheria zinazohusu Ardhi na Sera ya Mazingira na ile ya Misitu zimeshafanyiwa mapitio na marekebisho.
Mfumo wa ZALIS umefadhiliwa na Serikali ya Finland ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni 100 ambapo mgeni rasmi katika Uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Balozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Sinnika Antilla.

No comments:

Post a Comment