TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 16, 2015

Waziri Haji Omar Kheri amewapongeza Walimu na Wazazi wa Almadrasatul Nurul-Munawwara

index Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh; Haji Omar Kheri amewapongeza Walimu na Wazazi wa Almadrasatul Nurul-Munawwara kwa kuonyesha mashirikiano kati yao jambo ambalo linalopelekea kuwepo kwa ufaulu mzuri wa wanafunzi chuoni hapo. Pongezi hizo amezitoa huko Tumbatu Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja katika Madrasa hiyo wakati wa mahfali ya kusheherekea maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW). Waziri huyo amemshukuru Mwalimu Mkuu wa Madrasa hiyo kwa kuiendeleza sambamba na kumuenzi Marehemu Bakari Juma Khamis ambae ndiye muanzilishi wa Madrasa hiyo. “Namshukuru marehemu Bakari kwa mchango wake Mungu amlaze mahala pema Peponi na sisi tuliobaki nyuma yake atujaalie kila la kheri”, alieleza Waziri huyo.

Aidha amesema kuwa katika kumuenzi Marehemu huyo ni vizuri watu wakatoa mali zao kwa ajili ya Allah (SW) kwa wenye uwezo na asiye na uwezo ni vizuri akajitolea kwa hali na mawazo mazuri ambayo yatasaidia kwa njia moja au nyengine katika kuindeleza madrasa hiyo. “Watu wa Tumbatu watoe kwa hiari yao na waichangie madrasa hii kwani kufanya hivyo itakua ni bora zaidi kuliko kusubiri Wageni kutoa michango yao’’, alisema Waziri huyo. Hata hivyo Waziri huyo ameahidi kuichangia Madrasa hiyo kwa hali na mali ili iwe katika kiwango kizuri, cha kisasa na chenye kuridhisha. Nae Mwalimu Mkuu wa Madrasa hiyo Nd. Jecha Ali Saleh amemshukuru Waziri huyo kwa mchango huo mkubwa alioutoa kwa kuchangia zaidi ya asilimia 55 katika ujenzi wa Madrasa hiyo. Akielezea baadhi ya changamoto zinazoikabili madrasa hiyo Mwalimu huyo amesema mfumo wa kuanzishwa kwa masomo ya ziada maskulini kunapelekea kuporomoka kwa mfumo mzima wa mwenendo wa Madrasa kwani wanafunzi huwa hawahudhurii ipasavyo masomo Chuoni hapo sambamba na ukosefu wa Banda lenye nafasi ya kutosha kwa ajili ya kusomea wanafunzi hao kwani huchanganyika pamoja wakati wa masomo chuoni hapo. “Tuna Madarasa matatu lakini hayatoshelezi kwani Wanafunzi wa miaka 4 hawawezi kukaa na Wanafunzi wa miaka 20 wala miaka 14 hawawezi kukaa na wa miaka 4 hivyo tunahitaji Darasa kubwa zaidi kwa ajili ya watoto wetu”, Mwalimu huyo alisema. Mwalimu Jecha amewataka wafadhili wazingatie njia za kukuza imani ya Dini kuongeza misaada yao kwa kuisaidia Tumbatu Jongowe. “Watu waondokane na dhana potofu kwa kuona kuwa watu wakitoa msaada haitofanyiwa jambo lenye maana hiyo sikweli na watu waachane na dhana hiyo”, amesema Mwalimu Jecha. Aidha Shekh Haji Makame Mshenga amewataka watu wenye uwezo kutoa misaada katika mambo ya kheri, ili walimu wazidi kua na moyo wa kuwafundisha wanafunzi pamoja na kutoidharau Dini ya Kiislamu kwani ndio muongozo wa maisha ya kila siku ya mwanadamu. Sherehe hizo zimehudhuriwa na Madrasa mbalimbali ikiwemo Madrasatul Jauharil-Atfaal, Maamur, Nurul- Islamiyah, Tawhid Lilah, Manaqibul-Kadriya na Madrasatul Murabiyatul- Islamiyah zote kutoka kijijini Tumbatu.
NA RAHMA KHAMIS Maelezo-Zanzibar

No comments:

Post a Comment