TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 19, 2015

TIMU ya Coastal Union ya Tanga kucheza na Ndanda SC Jumamosi wiki hii

100_0628-610x400 
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeondoka mkoani hapa leo asubuhi kuelekea mkoani Mtwara kwa ajili ya mechi yao ya Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda SC itakayochezwa Jumamosi wiki hii.
     Coastal Union ambayo mechi yao iliyopita dhidi ya Mbeya City iliyochezwa kwenye uwanj wa
                CCM Mkwakwani haikupata matokeo mazuri sana baada ya kulazimishwa sare hivo itaingia kwenye mechi hiyo mithili ya mbogo aliyejeruhiwa msituni

                                                     Akizungumzia maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Kocha Mkuu wa Coastal Union,Mkenya
                            James Nandwa alisema kuwa kikosi chake kimeimarika zaidi baada ya kuyafanyia kazi kwa
                            asilimia kubwa mapungufu yaliyojitokeza mechi iliyopita.
                                          Alisema kuwa dhamira yake kubwa ni kuhakikisha kikosi hicho kinaibuka na ushindi kwenye
         mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na kila timu msimu huu
kuonekana kujiimarisha vilivyo kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.
   “Kikosi changu kipo imara kuweza kuwakabili Ndanda SC ikiwemo kuhakikisha tunapata
matokeo mazuri hii inatokana na maandalizi kabambe tuliyoyafanya hasa kubwa kurekebisha baadhi ya maeneo kwenye kikosi hiki “Alisema Kocha Nandwa. Alisema kuwa mipango yake hivi sasa ni kukiwezesha kikosi cha timu hiyo kuweza kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi kuu hapa nchini. Msafara wa Coastal Union uliondoka leo mkoani hapa kuelekea mkoani Mtwara unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ,Albert Peter ambapo baada ya kuwasili mkoani mtwara utafanya mazoezi.

No comments:

Post a Comment