TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 19, 2015

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI TAREHE 8 MACHI, 2015

imagesd1 

Tarehe 8 Machi, 2015 Tanzania itaungana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Kwa mwaka huu, tunaadhimisha siku hii adhimu katika ngazi ya kitaifa ambapo mkoa wa Morogoro utakuwa mwenyeji wa Maadhimisho haya. Mikoa mingine itakuwa na fursa ya kuandaa maadhimisho haya katika maeneo yao kwa kuzingatia mazingira yao.
Maadhimisho haya hutoa fursa kwa Taifa, mikoa, wilaya na wadau wengine kupima mafanikio yaliyopatikana katika kuwendeleza wanawake na kubainisha changamoto zilizojitokea katika kuwawezesha wanawake na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.
Maadhimisho ya mwaka 2015 ni ya kipekee kutokana na kuwepo kwa matukio muhimu ambayo yote yatagusa masuala ya haki za wanawake na usawa wa jinsia. Matukio hayo ni: Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge, na madiwani; tathmini ya mafanikio ya utekelezaji wa Azimio la Ulingo wa Beijing baada ya miaka 20 (1995 – 2015); tathmini ya Malengo ya Millenia (2005-2015) na mwelekeo wa Agenda 2063; kuhusu kuwa na ‘Afrika Tunayohitaji’ ifikapo mwaka 2063.

Kufuatia umuhimu huu Wizara imeandaa Kongamano la Kitaifa litakalofanyika tarehe 6 Machi, 2015 na maonesho ya shughuli mbalimbali sanjari na utoaji wa tuzo kwa waliochangia uwezeshaji wa wanawake nchini.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka 2015 ni: ‘Uwezeshaji Wanawake; Tekeleza Wakati ni Sasa’. Kaulimbiu hii inalenga kuhamasisha jamii kutambua mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo yao; na kuelimisha wadau kuangalia upya wajibu wao wa kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa wanawake haki sawa katika nafasi za elimu, uchumi na uongozi ili waweze kuwa chachu katika maendeleo yao.
Natoa wito kwa wananchi katika mikoa yote nchini kushiriki kikamilifu kuienzi siku hii adhimu. Ni matumaini yangu kwamba kupitia maadhimisho haya wadau wote na serikali watakumbushwa wajibu na mchango wao katika kutekeleza ujumbe wa kaulimbiu na kubaini mbinu za kukabiliana na changamoto za ushiriki wa wanawake katika maendeleo.
Aidha, nawaomba wanahabari kushirikiana na Serikali kuelimisha jamii kuhusu shuhuda bora zinazoonyesha jinsi gani wanawake walivyoweza kuaminiwa na hivyo kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa kwa ujumla. Nawatakia maadhimisho mema. Anna T. Maembe KATIBU MKUU 19/03/2015

No comments:

Post a Comment