TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 16, 2015

TAMASHA LA WANAWAKE KUFANYIKA MACHI 7MLIMANI CITY

antu3 Zuleiha Samwix  aksoma taarifa ya maandalizi hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wanaofuatia katika picha ni Agnes Mgongona Anto Mandoza.
……………………………………………………………………………
Siku Ya Wanawake Dunia huadhimishwa kila ifikapo Tarehe 8, mwezi wa tatu. Siku hii huadhimishwa kwa shughuli mbalimbali na kutambua mchango wa mwanamke katika maendeleo ya Jamii.
Mwaka huu kitaifa Siku hii itaadhimishwa mkoani Morogoro lakini kampuni ya TruMark ya mjini Dar es Salaam imeandaa warsha maalum katika maadhimisho hayo ambayo itafanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam Machi 7 mwaka huu.
Kauli mbiu ya Siku hii ni Women Make It Happen’ ikiwa inamaanisha wanawake wanafanikisha.
TruMark imeamua kufanya tamasha hili, baada ya uzoefu tulioupata katika shughuli zetu za mafunzo ambazo tunatoa kwa watu mbalimbali, tulioana kuna changamoto mbalimbali ambazo wanawake wanazipata.
Hii likafanya tuone kuwa Siku Ya Wanawake ni jukwaa ambalo linaweza kukutanisha wanawake katika kada mbalimbali na kuzungumza mambo yao katika kujikwamua kiuchumi na kujifunza kwa wengine ambao walipitia changamoto hizo lakini leo hii wameweza kufika mbali baada ya kupambana.
TruMark imepata Baraka zote kutoka Wizara ya Wanawake Jinsia na Watoto katika kuandaa siku hii muhimu. Kwenye maadhimisho haya, kutakuwa na mada ambazo zitatolewa na wanawake kutoka katika kada tofauti, juu ya uongozi, biashara na uchumi, ujasiriamali.
Lakini pamoja na elimu ambayo itatolewa kutakuwepo na burudani pia kutoka kwa wasanii wanawake maarufu na chipukizi nchini ambao wataungana na wanawake wengine kusheherekea siku yao hii.
Wanawake wanakaribishwa kushiriki katika siku hii ili kuweza kupata elimu ambayo itawasaidia kwenye shughuli zao za kila siku. Kwa upande mwingine tunatoa wito kwa wadhamini kujitokeza ili kufanikisha siku hii kwani mama ndiye kiungo cha familia.

No comments:

Post a Comment