Mjumbe
wa bodi ya wakurugenzi ya PSPTB, Bw, Aziz Kilonge akifungua mafunzo ya
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki
kwa kutoa mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa fani ya
ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya
stashahada ya ununuzi na ugavi mafunzo hayo yamefanyika kaktika ukumbi
baraza la Maaskofu TEC jijini Dar es salaam.
Mwezeshaji
wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr.Eli Tumsifu
akitoa mafunzo kwa wataalamu hao wa usimzmizi wa Manunuzi na Ugavi
Baadhi ya wataalamu wa Manunuzi na Ugavi wakifyuatilia mafunzo hayo.
Wataalamu hao wakiandika mambo muhimu wakati wa mafunzo hayo.
Bw. Godfrey Mbanyi Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB akiandaa mada katika kompyuta yake wakati wa mafunzo hayo.
Mjumbe
wa bodi ya wakurugenzi ya PSPTB, Bw, Aziz Kilonge akiwa katika picha
ya pamoja na wataalamu hao mara baada ya kufungua rasmi mafunzo hayo.
……………………………………………………………………….
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na
Ugavi imeendesha mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa
fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya
stashahada ya ununuzi na ugavi.
Mafunzo hayo yalifunguliwa jana, na mjumbe wa bodi ya
wakurugenzi, Bw, Aziz Kilonge, ambaye aliwaasa wataalam hao kuhakikisha
kwamba wanasimamia wanafunzi kwa ukamilifu ili kuongeza ubora wa kazi za
utafiti zinazofanywa.
Aidha, alifafanua kuwa uzingatiaji wa maadili katika kufanya
tafiti, ndio msingi na matakwa ya Bodi, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi
wanafanya tafiti na sio kuchukua kazi zilizofanywa na wanafunzi/watafiti
wengine au kufanyiwa na watu wengine.
Pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti, pia wanafunzi
wanajengewa uwezo wa kuandika ripoti na hata kuwasilisha ripoti katika
sehemu zao za kazi. Hivyo lengo kuu ni kuwejengea uwezo wa kutoa huduma
bora kwa taifa.
Aliwakumbusha wasimamizi hao kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa
kujiamini na kujieleza kwani ufaulu wa mwanafunzi, unategemea sana uwezo
wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani huo mwanafunzi
atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima uwezo wake.
Tesha Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Dr Clemence akizungumza katika mafunzo hayo mara baada ya kufunguliwa rasmi.
No comments:
Post a Comment