TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 19, 2015

WAZIRI MKUU: WASAIDIENI WAKULIMA WA MPUNGA KUNUFAIKA NA ZANA ZA KISASA

index 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa mkoa wa Iringa utafute njia bora ya kuwasaidia wakulima wanaotumia na skimu ya umwagiliaji ya Magozi katika tarafa ya Pawaga, wilayani Iringa ili waweze kunufaika na matumizi ya zana za kisasa kwenye kilimo cha mpunga.
Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo na uongozi wa vijiji hivyo, mara baada ya kukagua eneo zima la mradi huo pamoja na zana za kilimo walizonazo leo mchana (Alhamisi, Februari 19, 2015), Waziri Mkuu alisema kwa zana walizonazo hawawezi kufikia lengo lao la uzalishaji wa tani nane kwa ekari moja kama wataendelea na kilimo cha majaruba.
“Hii combine harvester umesema inavuna ekari 12 kwa siku moja, sasa hapa kuna mtu ana robo eka, jirani yake ana nusu eka, pale kuna mwingine ana ekari mbili utawezaje kutumia mashine hii? Kimsingi haiwezekani,” alihoji Waziri Mkuu.

Alimtaka Mkuu wa Mkoa huo, Bi. Amina Masenza awasiliane na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kupata taarifa wao walifanyaje katika mradi unaohusisha wakulima wadogo na mwekezaji kwenye kilimo cha mpunga wilayani Kilombero.
“Pangeni naye muone jinsi ya kuwachukua baadhi ya wakulima wadogo wa kata hii ili waende huko na kuona wenzao wamefanyaje kwenye kilimo kama chao lakini kinachotumia zana za kilimo za kisasa,” alisema Waziri Mkuu.
“Kikubwa hapa ni kuwaunganisha wawe na ushirika, walime kwa staili ya block farm… lakini wakishavuna kila mmoja apate mgao wake kulingana na eneo lake analomiliki. Mkifanya hivi mtaona tija katika matumizi ya mashine hizi, matumizi ya dawa za kuua magugu na hata matumizi ya mbegu bora,” aliongeza.
Katika skimu hiyo ya umwagiliaji ya Magozi, Waziri Mkuu alikagua mashine ya kupandia mpunga yenye uwezo wa kupanda miche 1,856 kwa ekari moja ama ekari tano kwa siku moja. Pia alikagua mashine ya kupurura mpunga yenye uwezo wa kupurura tani moja nusu za mpunga kwa siku. Vilevile, alionyeshwa mashine mbili za kuvuna mpunga ambapo kila moja ina uwezo wa kuvuna ekari 12.
Waziri Mkuu ambaye aliwasili mkoani Iringa jana jioni (Jumatano) akitokea Dodoma, ameanza ziara ya kikazi ya siku tano katika mkoa huu ili kukagua shughuli za maendeleo.

No comments:

Post a Comment