January 18, 2013  
       
       
       
         
       
       
        
       
       
                  
        
      
  
            
      
      
Mh.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiimba wimbo wa mshikamano kabla ya kuanza 
mkutano mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa Serekali za mitaa Talgwu jana 
amabao una fanyika mjini Dodoma kushoto kwa waziri mkuu ni Waziri wa 
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa( Tamisemi) Mh Hawa Ghasia na 
kulia kwa waziri mkuu ni mwenyekiti wa (Talgwu) Edna Mwaigomole pamoja 
naviongozi wengine  Picha na Chris Mfinanga
Mh.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda akizindua Tovuti ya chama cha wafanyakazi wa 
wa serekali za mitaa kulia kwa waziri mkuu anaye shuhudia uzinduzi huo 
ni Mwenyekiti wa chama hicho Bibi Edna Mwaigomole na aliye vaa tai ni 
mtalamu wa kompyuta uzinduzi ume fanyika leo mjini Dodoma Picha na Chris
 Mfinanga
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mjini Dodoma baada ya kuuzindua.
Mh.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwasili kufungua mkutano mkuu wa Baraza la 
wafanyakazi wa serekali za mitaa Talgwu kushoto kwa waziri mkuu ni 
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa (Tamisemi) Mh Hawa 
Ghasia na kulia ni Mwenyekiti wa Talgwu Edna Mwaigomole mkutano huo 
unafanyika mkoani Dodoma Picha na Chris Mfinanga
WASANII WA FILAMU BONGO KUCHEZA FILAMU NIGERIA NA DRC CONGO
           
       
       
        
Mkurugenzi wa Mad Mad 
Entertainment, Yasmin Razak (katikati) akizungumza na waandishi wa 
habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kampuni yake kuingia mikataba na
 wasanii wa filamu wa Tanzania watakaokwenda Nigeria na Jmahuri  ya 
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kutengeza filamu. Kushoto ni 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa 
Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba. 
Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa, alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu, kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.
“Hapa kuna kuinua vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika hatua za awali za mchujo,” alisema
Mwakifamba.
Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalie namna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.
Msanii wa filamu, Steve Nyerere 
(kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano hupo.Kushoto ni Mkurugenzi 
Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la
 Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba.  
……………………………………………………………….
KAMPUNI ya Mad Mad Entertainment
 iliyopo jijini London nchini Uingereza, imeanzisha program maalum ya 
kupeleka wasanii wa filamu za bongo nje ya nchi kwa lengo la kukuza 
sanaa hiyo hapa nchini.
 Akizungumza na waandishi wa 
habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo 
Yasmin Razak alisema ameamua kufanya kazi na wasanii  hao ili kuleta 
mabadiliko na kuwakwamua kiuchumi wasanii wa filamu hapa nchini.
 “Kwa muda mrefu niliokaa London
 sioni kama sanaa hii ina maendeleo, nikafikiria kitu gani nifanye ili 
 kukuza tasnia hii, katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza 
filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha Sh. 50 milioni pamoja na 
malipo mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na 
asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini.
“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria
 wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata
 Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia 
katika mchakato huo,”alisema Razak.Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa, alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu, kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.
“Hapa kuna kuinua vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika hatua za awali za mchujo,” alisema
Mwakifamba.
Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalie namna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.
Rais Kikwete apokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Msumbiji na Indonesia
Balozi
 mpya wa Msumbiji nchini Tanzania Dkt.Vicente Mebunia Veloso na Balozi 
Mpya wa Indonesia nchini(4395) Mhe.Zakaria Anshar wakiwasilisha hati zao
 za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es 
Salaam leo(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa  Indonesia ikulu jijini Dar es Salaam.
DK SHEIN KUONGOZA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA
January 17, 2013
            Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
 Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuongoza Mkutano
 wa saba wa Baraza la Biashara Zanzibar utakaofanyika Jumamosi Januari 
19 katika ukumbi wa Salama Hoteli Bwawani mjini Zanzibar.
 Akitoa taarifa kwa Vyombo vya 
habari huko Gulioni katika Jengo la ZSTC Katibu Mtendaji wa Baraza hilo 
Ali Haji Vuai alisema mkutano huo wa saba utazikutanisha Sekta za Umma 
na Sekta Binafsi, ambao utajadili mada mbili muhimu ambazo ni Maendeleo 
ya uwekezaji katika viwanda na Ubiya unaohitajika katika viwanda vya 
Zanzibar.
 Amesema wameamua kuzungumzia 
masuala hayo kutokana na Sekta ya Viwanda Zanzibar kuwa nyuma sana jambo
 ambalo pia huchangia ukosefu wa Ajira kwa vijana na mapato kwa 
maendeleo ya Zanzibar.
 Ameongeza kuwa Zanzibar ina fursa
 nzuri ya kuanzisha viwanda vipya na kuvifufua vile vilivyokuwepo awali 
jambo ambalo litachochea kasi ya maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa 
Zanzibar.
 Vuai amefahamisha kuwa Viwanda 
vilivyokufa Zanzibar vilitokana na sababu mbalimbali na kwamba Mkutano 
huo utakuwa ni sehemu muafaka ya kuelezea chanzo cha kufa viwanda hivyo 
na kubuni mipango mipya ya kufufua sekta hiyo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake (WAMA) Mama Salma Kikwete afunga kongamano la Ulimwengu la afya ya uzazi mjini Arusha
Mke
 wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete 
akifunga kongamano la Ulimwengu la Afya ya Uzazi la  siku 3 Katika 
ukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC mjini Arusha leo, Kongamano hilo 
lilewashirikisha wataalamu wa masuala ya afya ya  uzazi wapatao 800 
kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni, (Picha na Mwanakombo Jumaa- 
MAELEZO).
Baadhi
 ya wataalamu wa  kongamano la ulimwengu la afya ya uzazi wakimsikiliza 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete 
(hayupo pichani wakati wa kufunga kongamano Jan,17,2013 mjini Arusha, 
ambapo wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi zaidi ya 800 kutoka ndani 
na nje ya nchi wamehudhuria, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
Baadhi
 ya wataalamu wa  kongamano la ulimwengu la afya ya uzazi wakimsikiliza 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete 
(hayupo pichani wakati wa kufunga kongamano Jan,17,2013 mjini Arusha, 
ambapo wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi zaidi ya 800 kutoka ndani 
na nje ya nchi wamehudhuria, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa kmataifa wa AICC Arusha leo.
Mke
 wa Rais na Mwenyikiti wa Taasisisi ya WAMA ,Mama salma Kikwete (alievaa
 kitnge) akiogozana na watendaji wakuu wakielekea katika eneo la kupigia
 picha ya pamoja
Picha ya pamoja na watendaji wakuu wa kongamano la Ulimwengu la Afya ya Uzazi.
Mama Salma Kikwete akifurahia ngoma ya msanja ya kikundi cha akina mama huko Arusha
WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUJICHULIA SHERIA MIKONONI
Mahmoud Ahmad Arusha
…………………………………………..
Wananchi wenye hasira kali hapa nchini wametakiwa kuacha kujichukulia sheria mikononi na kuwapiga ama kuwachoma moto watu wanaodaiwa kuwa ni wezi bila ya kujua kama madai wanaotuhumiwa nayo ni ya kweli au la na wengine kujikuta wakipoteza maisha bila ya kuwa na hatia na kutakiwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na usalama.
Kauli hiyo imetolewa na wananchi mbali mbali wakati wakiongea
 na waandishi wa habari kwenye matukio mawili tofauti yaliyotoke kwenye 
sehemu mbili tofauti kwenye kituo kikuu cha mabasi na kituo kidogo cha 
vifodi jijini hapa jana.Wananchi wenye hasira kali hapa nchini wametakiwa kuacha kujichukulia sheria mikononi na kuwapiga ama kuwachoma moto watu wanaodaiwa kuwa ni wezi bila ya kujua kama madai wanaotuhumiwa nayo ni ya kweli au la na wengine kujikuta wakipoteza maisha bila ya kuwa na hatia na kutakiwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na usalama.
Katika tukio la kwanza kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 37 mkazi wa jijini hapa mwenye ugonjwa wa akili alipata mkong’oto wa kufa mtu baada ya kupiga gari la mtu lililokuwa kwenye stand hiyo na kumwaga vyakula na karanga za wafanyabiashara ndogo ndogo na vijana stand hapo kumpa mkong’oto huo.
Vijana hao huku wakimpa mkong’oto kijana huyo walikuwa wakimwambia kuwa wanampa dawa ya sigareti kubwa kwani dawa yake wanayo wao kijana huyo aliendelea kupatiwa mkong’oto nhadi askari wa jeshi la polisi aliyekuwa doria stand hapo kumuokoa na kumfikisha kwenye vyombo vya usalama kumuokoa na kipigo hicho kutoka kwa vijana wasio na chembe hata ya huruma kwa mgonjwa huyo.
Katika tukio la pili kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 17 mkazi wa jiji hili alipata mkong’oto wa paka mwizi hadi kushindwa kujua uelekeo wake wa kwenda baada ya kudai kuiba vitu kwenye duka moja stand ndogo ya vifodi
Waandishi walipohoji kwa mwenye duka hilo ni vitu gani vimeibiwa kwenye duka hilo alishindwa kuthibitisha kuwa alIIbiwa nini dukani humo huku mgambo wa jiji wakiangali bila ya kuchukuwa hatua yeyote.
Taarifa zinadai kuwa wananchi mbali mbali wamekuwa wakipatiwa mkong’oto bila ya kuwa na hatia ya makosa wanayotuhumiwa na kuwataka wananchi mbali mbali kutokujichukulia sheria mikononi
Alipohojiwa kamanda wa polisi 
mkoani hapa Liberatus Sabas kuhusiana na wananchi kujichukulia sheria 
mkononi alisema matukio mengi ya kujichukulia sheria mkononi ni tatizo 
hapa nchini huku akiwataka watanzania kujenga mazoea ya kujichunguza 
kabla  ya kujichukulia sheria mkononi.
WAZIRI MWANRI AWACHACHAMALIA WANAOPIGA MIMBA WANAFUNZI
Na Kibada Kibada wa Fullshangwe-Katavi
Naibu  Waziri wa nchi  Ofisi ya 
waziri mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)  Agrey 
Mwanri amewaagiza viongozi na Watendaji wa serikali kuhakikisha 
wanakomesha suala la mimba mashuleni.
Waziri Mwanri alitoa agizo hilo 
(leo) wakati akizungumza na wananchi  kwenye mkutano wa hadhara 
uliofanyika katika kijiji cha  Kilida Kata ya Mamba wilayani Mlele 
Mkoani Katavi katika ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za 
maendeleo na kuona jinsi gani Halmashauri zinasimamia fedha za serikali 
zinazoletwa kwenye halmashauri kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika
 kutekeleza miradi na kupeana mikakati jinsi ya kusimamia fedha hizo ili
 zifznye kazi iliyokusudiwa.
 Amesema  ni wajibu wa viongozi 
kuhakikisha suala la mimba linakomeshwa kabisa mashuleni na haitoshi 
kila mara viongozi kuripoti tu, suala la mimba mashuleni bila hatua 
kuchukuliwa kwa wale wahusika wanaofanya vitendo hivyo vya kuwapa mimba 
watoto wa kike.
“Haitakiwi kuripoti tu,pia 
inatakiwa kueleza ni hatua gani zimechukuliwa  kuhakikisha hao wanofanya
 vitendo hivyo wamechukuliwa hatua zipi za kisheria ili kukomesha 
vitendo hivyo”alisema kwa kufoka Mwaniri.
Aliagiza kufuatia kusomewa 
 taarifa ya Mkoa kuhusu maendeleo ya Mkoa  iliyosomwa na Kaimu Katibu 
Tawala wa Mkoa wa Katavi Lauten Kanoni   ikieleza hali ya elimu na jinsi
 suala la mimba kwa watoto wa kike linavyo shughulikiwa
 Aidha katika taarifa hiyo 
ilieleza  hali ilivyo kwa sasa ilieleza kuwa mimba kwa mkoa wa katavi 
zimepungua kutoka wasichana waliopata ujauzito mwaka 2011  (63)  na 
 mwaka 2012  mimba zilipungua kufikia  (61)   sawa na asilimia tano 
.taarifa ambayo haikueleza namna wanavyolishughulikia tatizo la mimba na
 kueleza wangapi walichukuliwa hatua za kisheria kulingana na makosa 
hayo.
Na ni mikakati gani inafanywa 
kuhakikisha wanakomesha kabisa suala la mimba mashuleni kwa wanafunzi 
wengi wanapatiwa mimba na wazazi na jamii inaangali badala yake 
wanamalizana kwa kupeana zawadi huko huko majumbani hali hiyo inayofanya
 kuendelea kila mwaka.
 “Juhudi kubwa inatakiwa kufanyika
 ili kuhakikisha  wale wote wanaohusika wanachukuliwa hatua kali za 
kisheria kukomesha suala hili kwa kushirikiana wote viongozi wananchi, 
serikali, jamii, wazazi, walimu na wanafunzi kwa nafsi yao kukomesha 
suala la mimba kwa watoto wa kike mashuleni”alimaliza Mwanri.
Push Mobile, Channel Ten kutoa zawadi ya gari Valentine Day
Meneja
 Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo 
wakati wa uzinduzi wa shindano la kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu 
ya wapendanao ‘ Valentine Day’ iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Kampuni
 ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel 
Ten na Redio Magic FM. Kushoto ni AFISA Masoko na Mauzo wa AMG,  Prosper
 Vedasto
………………………………………………………………….
KAMPUNI ya Push Media Mobile 
itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya shs milioni 8 kwa 
mshindi wa kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanoa 
“Valentine Day” ikayoa adhimishwa Februari 14.
Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo katika uzinduzi wa kampeni hiyi pamoja na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM.
Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo katika uzinduzi wa kampeni hiyi pamoja na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM.
Rugambo alisema kuwa wameamua 
kutoa zawadi kubwa hiyo ili kuwafanya wapendanao wegi kushiriki na 
kupata nafasi ya kushinda. Alisema kuwa ili kuingia katika droo ya 
shindano hilo, unatakiwa kutuma neno “Penzi” kwenda namba 15678 na 
kujibu maswali mbali mbali yahusiyo masuala ya mapenzi na siku ya 
Valentine.
“Hii ni promosheni ya kwanza kubwa hapa nchini na mshindi kujishindia gari, lengo kubwa ni kutoa ufahamu kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vile vile kuwazawadia wadau waokwa kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa taifa,” alisema Rugambo.
Alisema kuwa mbali ya zawadi hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata nafasi ya kujisha kompyuta (Laptop) aina ya HP yenye thamani ya shs milioni 1.5, simu aina ya Blackberry Curve yenye thamani ya shs 500,000 na Home theatre ya thamani ya shs 400,000 na Ipad.
Kwa mujibu wa Rugambo, lengo lao kubwa ni kuifanya sikukuu ya wapendanao kuwa kubwa kama nyingine kwani mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku.
Alisema kuwa mipango yao ni kuwekeza katika sikukuu hiyo ambayo jamii imeanza kuitilia mkazo japo si siku ya mapumziko kama sikukuu nyingine. Alisema kuwa kwa mwaka huu, wameweka bajeti ya shs milioni 30 ili kufanikisha zaoezi hilo.
“Hii ni promosheni ya kwanza kubwa hapa nchini na mshindi kujishindia gari, lengo kubwa ni kutoa ufahamu kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vile vile kuwazawadia wadau waokwa kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa taifa,” alisema Rugambo.
Alisema kuwa mbali ya zawadi hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata nafasi ya kujisha kompyuta (Laptop) aina ya HP yenye thamani ya shs milioni 1.5, simu aina ya Blackberry Curve yenye thamani ya shs 500,000 na Home theatre ya thamani ya shs 400,000 na Ipad.
Kwa mujibu wa Rugambo, lengo lao kubwa ni kuifanya sikukuu ya wapendanao kuwa kubwa kama nyingine kwani mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku.
Alisema kuwa mipango yao ni kuwekeza katika sikukuu hiyo ambayo jamii imeanza kuitilia mkazo japo si siku ya mapumziko kama sikukuu nyingine. Alisema kuwa kwa mwaka huu, wameweka bajeti ya shs milioni 30 ili kufanikisha zaoezi hilo.
MAKAMO MWENYEIKI CCM ZANZIBAR DK. SHEIN, AZUNGUMZA NA VIONGOZI OFISI KUU YA CCM KISIWANDUI
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisisitiza jambo alipokua akizungumza na Viongozi wa Tawi la
CCM Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali
mbali za Chama hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Mjini Zanzibar jana,Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya
kusalimiana na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisisitiza jambo alipokua akizungumza na Viongozi wa Tawi la
CCM Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali
mbali za Chama hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Mjini Zanzibar jana,Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya
kusalimiana na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(wapili kulia) akizungumza na Viongozi wa Tawi la CCM Afissi
Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali mbali za
Chama hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini
Zanzibar jana,Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimana
na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(wapili kulia) akizungumza na Viongozi wa Tawi la CCM Afissi
Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali mbali za
Chama hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini
Zanzibar jana,Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimana
na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Makamo
 Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza 
la Mapinduzi Dk.Ali MohamedShein,akizungumza na  Viongozi wa Tawi la CCM
 Afissi Kuu ya CCMKisiwandui,wakiwemo Viongozi wa  Jumuiya mbali mbali 
za Chama  hichokatika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui  Mjini 
Zanzibarjana,Makamo  Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimana 
naViongozi hao ikiwa  ni pamoja na  kuimarisha Chama cha 
Mapinduzi,(CCM)(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali 
Vuai,na (kushoto)Mwenyekiti wa Tawi  Nadra Juma  Mohamed.[Picha na 
Ramadhan
 Othman,Ikulu.]
36 WACHUKUA FOMU TFF, 18 WAREJESHA
Wakati kesho ndiyo mwisho wa 
kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania
 (TPL Board) waombaji 36 wameshachukua na 18 tayari wamesharejesha.
 Idadi hiyo ni kufikia leo
 mchana (Januari 17 mwaka huu). Pia Kamati ya Uchaguzi ya TFF 
inasisitiza kuwa wanaorejesha fomu hizo kwa email wanatakiwa kuzituma 
kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa email ya tfftz@yahoo.com na si kwa email binafsi za wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi au maofisa wa TFF.
 Waombaji wanne walioongezeka 
katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi na Rukwa, Eliud 
Mvella (Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na Pwani), na Omari 
Abdulkadir kwa Kanda ya Dar es Salaam.
 Orodha kamili ya waombaji ni 
Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais) wakati 
waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael Wambura, Ramadhan 
Nassib na Wallace Karia.
 Kwa upande wa wajumbe wa Kamati 
ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita),
 Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara 
na Mwanza).
 Epaphra Swai na Mbasha Matutu 
(Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na 
Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy 
Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James
 Mhagama (Njombe na Ruvuma).
 Athuman Kambi na Zafarani Damoder
 (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na 
Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange na Twahili Njoki (Morogoro na 
Pwani), Elias Mwanjala na Eliud Mvella (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed
 (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih 
Dauda (Dar es Salaam).
 Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu 
(TPL Board) waliochukua fomu mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji 
amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya 
kuwania umakamu mwenyekiti.
ZAIDI YA MILLION 31.9 ZAGHARAMIA VIFAA LIGI YA MOHAMMED DEWJI, SINGIDA
Mwenyekiti
 wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa 
vya michezo kwa kiongozi wa tawi la Mitunduruni.
 
Foleni
 ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa
 vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa 
kuanza Januari 20 mwaka huu.
Baadhi
 ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la 
Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo 
wa soka jimboni kwake. (Picha zote na Nathaniel Limu).
……………………………………………………….
Mbunge
 wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa 
mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9 
vitakavyotumika kwenye ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua 
vumbi januari 20 mwaka huu.
Vifaa
 hivyo ni pamoja na jezi pea 854,mipira 122,soksi pea 854 na cloves za 
magolikipa 61.Vifaa hivyo ni kwa ajili ya timu zitakazoshiriki ligi 
ngazi ya kitongoji katika jimbo la Singida mjini.Baada ya ligi 
hiyo,itafuatwa na ligi ngazi ya kata ambayo atakuwa na vifaa vyake pia.
Akizungumza
 kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,mwenyekiti wa CCM jimbo la 
Singida mjini, Hamisi Nguli amepongeza mbunge Dewji kwa kuendelea kutoa 
misaada mikubwa mbalimbali katika jimbo lake kwa lengo la kuendeleza 
wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.
“Dewji
 toka awe mbunge wa jimbo la Singida mjini,siku zote yupo karibu zaidi 
na vijana. Amewasaidia mambo mengi makubwa ikiwemo kuwaendeleza 
kimichezo na pia ametoa pikipiki kwa ajili ya vijana wa bodaboda 
watakaojiunga katika vikundi”,alisema.
Awali
 msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni
 mwendelezo wa Dewji kuhakikisha vijana wanatumia michezo kujiendeleza 
kimaisha.
MKE WA RAIS NA MWENYEKITI WA TAASISI YA WAMA AFUNGA MKUTANO WA MAMA NA MTOTO LEO JAN 17,2013-ARUSHA
Mke
 wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama 
Salma Kikwete(kushoto) pamoja na Naibu wa Wizara ya Afya Dkt.Seif Rashid
 (mwenye miwani) wakielekea kupanda ndege katika Uwanja wa ndege wa 
kimataifa wa- JK- Nyerere jijini Dar es Salaam 16-jan 2013 kuelekea  
Arusha kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya na Mtoto jan. 
17,2013. Mkutano huo unawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje
 ya nchi. (picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mke
 wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama 
Salma Kikwete (mwenye kilemba) akisalimiana na wafanyakazi wa ndani ya 
ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini 
Dar es Salaam Jan 16,2013 wakati akielekea kufunga mkutano wa Masuala ya
 Afya na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Mkutano huo 
anawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi, (kulia) ni 
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid. (Picha na Mwanakombo Jumaa- 
MAELEZO).
Mke
 wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama 
Salma Kikwete(kulia) akiangalia vikundi vya sanaa ya  ngoma mbalimbali 
za utamaduni  alipowasili  katika  kiwanja  cha ndege cha Kimataifa cha 
Kilimnjaro (KIA) jan 16.2013 kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya 
Afya ya Mama na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani  Arusha. Aliengozana nae  
wapili ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Arusha (UWT) Flora 
Zelote (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Kikundi
 cha kinamama  cha ngoma ya Msanja  kikitumbuiza katika mapokezi ya Mke 
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama 
salma Kikwete (hayupo pichani)   kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa 
Kilimanjaro  (KIA ) Jan 16,2013.(Picha na Mwanakombo  Jumaa  wa 
MAELEZO).
Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo  Wanawake(WAMA) kulia, Mama Salma 
Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa Arusha Magesa Mulongo (kushoto)  
wakati  alipowasil katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA)
 Jan 16,2013.- Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Mke
 wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama 
Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John 
Mongela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Jan 
16,2013. –Picha na Mwnakombo Jumaa- MAELEZO.
………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Kauli mbiu ya kongamano la 
ulimwengu la Afya ya uzazi linaloendelea jijini Arusha imepewa msisitizo
 na kuwa hakuna mama atakayekufa wakati akileta kiumbe duniani na pia 
Afya ya mama na mtoto ipewe kipaumbele.
 Kauli hiyo imeendelea kutolewa na
 Mke wa Rais mama Salma Kikwete wakati akiwasilisha na kuzungumza na 
washiriki wa kongamano hilo jijini hapa na kuwataka watafiti na 
wataalamu hao kuja na majibu yatakayosaidia kupunguza vifo vya 
wakinamama wakati wa kujifungua.
 Mama kikwete alisema kuwa takwimu
 zinaonyesha kupungua kwa kiasi kidogo tatizo la kujifungua na kupoteza 
maisha hapa nchini na kuwataka wataalamu humu nchini kuchukuwa uzoefu 
walioupata kuchangia kupunguza vifo vya wamama wakati wa kujifungua 
sanjari na watoto huku wajawazito zaidi ya 459 hufa kila mwaka wakati 
wakijifungua.
 “Asilimia 90% ya nchi 
zilizoendelea wanaweza kupunguza ama kuokoa maisha ya kinamama na watoto
 huku hapa nchini wakiandaa mpango endelevu wa kuokoa maisha ya 
wamamawajawazito wakati wa kijifungua na kutoa rai kuwa wamama wasife 
kwa magonjwa ambayo yanaweza kupatiwa tiba”alisema mama Salma.
 Mama Salma alisema kuwa suala la 
afya ya uzazi liwe mpango endelevu kwa serekali na asasi mbali mbali na 
kuitaka serekali kulipa kipaumbele suala la afya ya mama na mtoto licha 
ya majukumu mbali mbali iliyonayo.
 Nae naibu waziri wa Afya na 
maendeleo ya jamii hapa nchini Seif  Raishid alisema kuwa serekali 
kupitia wizara hiyo wameweka kipaumbele suala la mama afya ya uzazi na 
kuwa hakuna mama atakaeyekufa wakati akiwa analeta kiumbe duniani 
sanjari na watoto na wamejipanga kuongeza wigo wa kuwafikia wakinamama 
kwa kuongeza zahanati kuwa karibu na usafiri sanjari na huduma muhimu.
 Rashid akwataka watanzania 
walioshiriki kongamano hilo kutoa uzoefu walioupata kutatua tatizo la 
afya ya mama na watoto ilikupunguza vifo ambvyo vinawezekana kuepukika 
kutokana na kukosa eidha huduma muhimu wakati wakujifungua.
 Kwa upande wake mkurugenzi wa 
afya dkt dumilia chalamila alisema kuwa mkutano huo umewashirikisha 
zaidi ya wataalam na watoa maamuzi zaidi ya 800 kutoka mataifa mbali 
mbali ulimwenguni wakichangia uzoefu katika kulipatia ufumbuzi suala la 
afya ya uzazi.
TANZANIA YAANZA RASMI KUTUMIA MFUMO WA KIMATAIFA WA UKAGUZI
NA GLADNESS MUSHI -ARUSHA
 Tanzania imeanza kutumia rasmi mfumo wa kimataifa katika masuala ya ukaguzi wa ndani ambapomfumo huo utaweza kupunguza Viashiria mbalimbali vya ubadilifu wa fedha za umma
 Hayo yamebinishwa  leo na mkaguzi
 mkuu wa ndani hapa Nchini Bw Mohamed Mtonga wakati akifungua mafunzo 
kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika kanda ya kaskazini
 Mohamed alisema kuwa mpango huo 
wa ukaguzi kwa mfumo wa Kimataifa umeanza kutumika rasmi hapa nchini 
July  Mosi ambapo utaweza kutoa na kuonesha viashiria mbalimbali ambavyo
 vinakwamisha shuguli za ukaguzi ndani ya Serikali kuu pamoja na  
Serikali za Mitaa.
 Alisema kuwa kupitia mfumo huo 
mpya wa kimataifa wa ukaguzi wa ndani utaweza kuboresha  na kuwafanya 
wakaguzi wa ndani kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi tofauti na mfumo 
uliokuwa hapo awali ambao ulikua hautoi fursa kwa wakaguzi wa ndani
 Alifafanua kuwa hapo awali 
wakaguzi wa ndani walikuwa wanashindwa kutekeleza  majukumu yao kutokana
 na viashiria vya vitu mbalimbali kama vile rushwa na uhusiano baina ya 
mkaguzi na mkaguliwa hali ambayo ilikuwa chanzo cha kukwamisha malengo 
mbalimbali ya ukaguzi hapa nchini ingawaje  ndani ya mfumo wa ukaguzi 
kimataifa suala hilo halipo kabisa.
SHIRIKA LABUNI MBINU MPYA YA KUWAFUATILIA MAMA WAJAWAZITO KWA SIMU ILI KUPUNGUZA VIFO NYAKATI ZA KUJIFUNGUA
Na Gladness Mushi -Arusha
 SHIRIKA  la Jhpiego  la jijini 
Dar es saalam limefanikiwa kubuni aina mpya ya mradi ujulikao kama 
Maisha ambapo mradi huo utaweza kutumia simu za mkononi kwa ajili ya 
kufuatilia afya za mama wajawazito  kwa malengo ya kupunguza vifo vya 
wajawazito
 Akiongea na 
“Fullshangweblog”mjini hapa mapemajana Meneja mradi wa shirika hilo Dkt 
Dunstan Bishanga alisema kuwa mradi huo wa maisha umeanza kutekelezwa 
kwa mkoa wa Morogoro
 Dkt Bishanga aliongeza 
kuwa mradi huo una malengo ya kuhakikisha kuwa inapunguza vifo vya mama 
wajawazito hapa nnchini lakini njia pekee ya kuwakutanisha wahudumu wa 
afya pamoja na wajawazito ni simu za mkononi hasa  kwa kuwapa wajawazito taarifa mbalimbali
 Pia alisema kuwa Mradi huo ambao 
kwa sasa umeanza kutumika katika Mkoa wa Morogoro lakini wanaendelea 
kufanya tathimini mbalimbali za kuhakikisha kuwa unasambaa nchi nzima 
kwani una uwezo mkubwa sana wa kuokoa maisha ya mama wajawazito
 Hataivyo aliongeza kuwa mara 
baada ya mkoa wa Morogoro kunufaika na mradi huo wataweza kwenda mikoani
 ikiwa ni pamoja na kuongeza zaidi ubunifu zaidi ili kuimarisha zaidi 
afya ya mama kwa manufaa ya Nchi nzima kwani vifo hivyo vinasababisha 
sana Umaskini katika jamii.
 Awali alisema kuwa suala la mama 
wajawazito ni suala ambalo linatakiwa kuchukuliwa tahadhari kubwa sana 
ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu sahihi za afya kutoka kwa wataalamu 
hivyo nao wazazi wa kiume wana nafasi kubwa sana ya kufanya hivyo
Miss Demokrasia Tanzania- INAKUPA POLE SANA BW. ERASTO MAPUNDA KWA KUMPOTEZA MKE WAKO MPENDWA
Marehemu Judith Chikaka Mapunda enzi za uhai wake.
Mwili wa Judith Chikaka ukiwa umelazwa ndani ya Jeneza Pamoja na mwili wa marehemu Mtoto wake mchanga. 
Marehemu Judith Chikaka 
alifariki siku ya Jumapili  ya tarehe 13/01/2012 katika Hospitali ya 
Mwananyamala wakati alipofikishwa hapo kwa ajili ya kujifungua, kwa 
bahati mbaya na mapenzi yake muumba alifariki kabla ya kujifungua.
Mume wa Marehemu Judith, Bwana Erasto Mapunda akiwa amembeba mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mkewe.
Baba mzazi wa marehemu Judith, Mzee Chikaka
Mama mzazi wa marehemu Mama Chikaka sakiwana majonzi makubwa baada ya kumpoteza mtoto wake kipenzi
Padre kutoka Parokia ya 
Kigamboni akiendesha Ibada ya misa takatifu ya kumwombea Judith alale 
kwa amani. Ibada hiyo ilifanyika nyumbani kwa Marehemu Judith maeneo ya 
Kigamboni Kibada.
Baadhi ya viongozi wa CCM Temeke wakitoa rambi rambi zao.
Spika wa Bunge la wanafunzi wa chuo cha Ardhi akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bwana S. Nyambui akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanachama na chama chao kwa ujumla.
Mume wa marehemu Judith akiweka Shada la maua katika nyumba ya milele ya mkewe
Kushoto ni mwakilishi wa Familia
 ya marehemu akipokea rambi rambi kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa 
marehemu kutoka wizara ya Ardhi
Mwakilishi kutoka Wizara ya Ardhi upande wa michezo akitoa salamu zake kwa niaba ya wanamichezo wenzake.
 Hii ndio nyuma ya milele ya marehemu Judith Chikaka Mapunda. 
Marehemu Judith  alizikwa jana katika makaburi ya Kibada maeneo ya Kigamboni, ameacha Mume na Mtoto mmoja.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEME MAHALI PEMA PEPONI. 
AMIN.
SOKO LA BUGURUNI WAMUOMBA RAIS JAKAYA KIKWETE KUTEKELEZA AHADI YA KUJENGO SOKO
 WAFANYABIASHARA
 wa soko la Buguruni lililoko wilayani Ilala jijini Dar es Salaam 
wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza ahadi yake kwa vitendo kwa 
kuwajengea soko jipya wafanyabiashara hao kinyume chake watasitisha 
kulipa ushuru.
 Akizunguza na Mwandishi wa habari hizi kwa
 niaba ya wenzake jijini, mmoja wa wafanyabiashara hao, Maulu Mali 
alisema hawaamini kama serikali haina fedha za kujenga soko hilo. 
Alisema wamefikia hatua hiyo 
baada ya viongozi mbambali akiwemo Rais kushindwa kutekeleza ahadi zao 
za kujenga soko hilo ambapo kwa uchakavu wa soko hilo inawafanya 
washindwe kufanyabiasha zao kwa mafanikio.
Mali alisema hadi sasa wamechoka
 kudanganywa hivyo ni vema wakasitisha kulipa ushuru hadi hapo 
watakapohakikishiwa vingine tena kwa vitendo wala si kwa maneno.
Alisema hali ni mbaya katika 
soko hilo haswa katika kipindi hiki cha mvua, bidhaa za wafanyabiashara 
hao zinaharibika kutokana na kuvujiwa. 
Alisema ndani ya soko hilo hivi 
sasa kumejaa maji yaliyochanganyika na uchafu, baada ya mifereji  kuziba
 hali inayohatarisha afya zao na maradhi ya mlipuko. 
Alipoulizwa Ofisa Masoko wa 
wilaya hiyo, Athuman Mbelwa, kuhusu tatizo linalowakabili 
wafanyabiashara hao, Mbelwa alikiri kuwa soko hilo liko katika hali 
mbaya likifanana na kiota cha ndege.
BONDIA IDDY MNYEKE AJIFUA KUMKABILI SADIKI MOMBA FEBRUARI 14
| Bondia Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com | 
RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA AU NA RAIS WA BENIN MHE BONI YAYI
Rais
 Jakaya Mrisho akiongea na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa
 Benin Mhe Boni Yayi Ikulu jijini Dar es salaam jana Januari 16, 2013
Rais
 Jakaya Mrisho akimuaga Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa 
Benin Mhe Boni Yayi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Julius 
Nyerere  jana Januari 16, 2013
Rais
 Jakaya Mrisho akimuaga Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa 
Benin Mhe Boni Yayi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Julius 
Nyerere  jana Januari 16, 2013
Rais
 Jakaya Mrisho na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin 
Mhe Boni Yayi wakiongea katika mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es
 salaam leo Januari 16, 2013
Rais
 Jakaya Mrisho akiandika jambo akiangaliwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika
 (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi Ikulu jijini Dar es salaam leo 
Januari 16, 2013
MZEE MKAPA NA MZEE MSUYA WATOA MAONI
Rais
 Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akifurahia jambo na Wajumbe wa Tume na 
Sekretarieti ya Tume Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam 
jana(Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo 
Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika 
uandishi wa Katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba na 
kulia ni Mjumbe wa Tume Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu Mwenyekiti wa 
Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume Bw. Assaa 
Rashid.
PICHA NAKATIBA TUME YA KATIBA
Waziri
 Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa Msuya akiongea na Wajumbe wa Tume ya 
Mabadiliko ya Katiba kuhusu mchakato wa Katiba Mpya jana (Jumatano, 
Januari 16, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji
 Joseph Warioba.
Mwenyekiti
 wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akibadilishana 
mawazo na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo 
(Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo 
Mstaafu jana jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika
 uandishi wa Katiba Mpya.
Rais
 Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya 
Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na
 Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu
 jana (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na 
uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Rais
 Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya 
Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na
 Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu
 jana (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na 
uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
MAOFISA WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL ARUSHA
RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AZINDUA AWAMU YA KWANZA YA JENGO JIPYA LA HOSPITALI YA SHREE HINDU MANDAL JIJINI DAR ES SALAAM
Rais
 Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasha mshumaa kama ishara ya uzinduzi wa 
Awamu ya Kwanza ya jengo jipya na Awamu ya pili ya Hospitali ya Shree 
Hindu Mandal ya jijini Dar es salaam leo katika Mtaa wa Nyanza, ambapo 
huduma hiyo itapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali jijini na
 kuongeza wigo wa utoaji huduma n kuongeza vitanda vya kulaza wagonjwa, 
Hospitali ya Shree Hindu Mandalilianzishwa mwaka 1931 ikianza na 
Zahanati anayeshuhudiatukio hilowa pili katikati ni Mwenyekiti wa 
hospitali hiyo Bw Ramesh Patel.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa hoapitali hiyo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo leo.
Waziri
 wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi akimkaribisha Rais Jakaya
 Kikwete ili kuzungumza na wafanyakazi wa hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa Hospitali ya Shree Hindu Mandal Bw. Ramesh Patel akielezea historia ya hospitali hiyo.
Rais
 Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili 
hospitalini hapo kwa ajili ya kuizindua, kushoto ni Waziri wa Afya na 
Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na Kulia ni Bw. Ramesh Patel 
Mwenyekiti wa Hospitali hiyo.
Mkuu
 wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi akizungumza na Waziri wa Afya na 
Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na Kulia ni Bw. Ramesh Patel 
Mwenyekiti wa Hospitali hiyo.
Baadhi ya madaktari na wauguzi wakisubiri kuwasili kwa Rais Jakaya Kikwete 
Baadhi ya madaktari na wauguzi wakisubiri kuwasili kwa Rais Jakaya Kikwete
Baadhi ya wauguzi na wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo.
Rais
 Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi , Madaktari , 
Wauguzi pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya Shree Hindu Mandal mara 
baada ya kuzindua rasmi leo
Waziri Simba akabidhi vyerehani kwa wajane
Waziri
 wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akimsikiliza
 Gavana wa Lions Ukanda wa Uganda na Tanzania, Joseph Kiwanuka, wakati 
alipomtembelea leo ofisini kwake akiwa na ujumbe wa watu watano.
Waziri
 Simba akiangalia baadhi ya vyerehani viwili viliyotolewa na Lions kwa 
ajili ya kuwasaidia wanawake wajane. Vyerehani hivyo ni kati ya 100 
vitakavyotolewa na Lions kuwawezesha wanawake kujikimu kimaisha.
Waziri
 Simba akimkabidhi mmoja wa wafaidi wa vyerehani vilivyotolewa na Lions 
Bi. Jane Fuiko wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi zilizofanyika leo 
ofisini kwa Waziri.
Gavana Kiwanuka akimkabidhi cherehani Waziri Simba kabla ya kumkabidhi mfaidika wa pili wa vyerehani hiyo Bi. Mariam Mohamed.
………………………………………………………………
Usu-Emma Sindila na Sakina Mfinanga
Waziri
 wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba  amekabidhi 
msaada wa vyerehani  viwili kati ya 100 vilivyotolewa kwa wanawake  
wajane wa Mkoa wa  Dar es Salaam  ofisini kwake leo kutoka Taasisi ya 
Lions Club, 
Akizungumza
 kwenye hafla fupi ya kukabidhi  vyerehani hivyo, Gavana wa Lions Ukanda
 wa Tanzania na Uganda, Ndg. Joseph Kiwanuka, amesema taasisi yao 
imekuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii hasa wanawake na watoto, 
kuboresha huduma za maji kwa kuchimba visima ambavyo huwasaidia wananchi
 hasa wanaokaa sehemu zenye shida ya maji.
Amesema
 Lions imekuwa ikisaidia watoto wenye matatizo ya moyo kuwapeleka nchini
 India kwa ajili ya matibabu,kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye 
mazingira magumu kwa kuwapeleka shule hasa zile za awali na wameanzisha 
mkakati wa kuwaelimisha wanafunzi mashuleni kuhusu utumiaji wa madawa ya
 kulevya ili watoto wasijihusishe na vitendo hivyo.
Kwa
 upande wake Waziri Simba ameishukuru taasisi ya Lions kwa misaada 
mbalimbali ambayo wamekuwa wakiisaidia jamii na zaidi kwa msaada huo wa 
vyerehani kwa wajane kwa kuwa utawawezesha kujikwamua kimaisha wao 
wenyewe,  watoto na familia zao.
Aidha,
 Waziri Simba amewapongeza Lions kwa kazi kubwa wanayofanya kupitia 
mradi wao wa kuelimisha wanafunzi juu ya madhara ya utumiaji wa dawa za 
kulevya na kuongeza kuwa Serikali inafanya jitihada kuhakikisha kila 
kata inakuwa na shule ili kusaidia kupunguza wimbi la watoto wasiojua 
kusoma na kuandika.
UJUMBE KUTOKA JIJI LA MWANZA WATEMBELEA MANISPAA YA ILALA KUJIFUNZA MBINU ZA UKUSANYAJI MAPATO
Mstaiki
 meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula na ujumbe wa kamati yake ya
 fedha wametembelea halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa maagizo ya 
Mhe.Waziri Mkuu kuja kujionea mbinu za kisasa za kukusanya mapato.
 Mstaiki
 Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa amewakaribisha
 na kuwaeleza jinsi walivyoweza na wanavyoendelea kukusanya mapato.
Mstahiki
 Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa akiueleza 
ugeni huo kutoka jiji la Mwanza mambo mbalimbali  jinsi walivyoweza na 
wanavyoendelea kukusanya mapato.
Mtahiki
 Meya wa Ilala  Mhe Jerry Silaa akiwa na ugeni huo kutoka jiji la Mwanza
 katika kikao kilichozungumzia mbinu za ukusanyaji wa  mapato.
MFANYAKAZI WA NDANI AJINYONGA TABATA MARAKUDA
Mwili
 wa mwanadada ambaehatukulipata jina lake mara moja unkichukuliwa na 
Polisibaada ya kujinyonga katika eneo la Tabata Barakuda jijini Dar es 
salaam bado haijafahamika ni chanzo cha kujinyongwa kwake,taarifa zaidi 
zinasema msichana huyo alikuwa akifanya kazi za ndani (House Girl) Picha
 kwa hisani ya www.tzdadaz.blogspot.com.  
Hapa
 mwili ukitolewa  na Polisi katika chumba alichojinyongea katika eneo la
 Tabata Barakuda jijini Dar es salaam bado haijafahamika ni chanzo cha 
kujinyongwa kwake
SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUTEKELEZA MPANGO WA MIRADI WA AFYA YA MAMA
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi
……………………………………………………………………….
Na Gladness Mushi -Arusha
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
SERIKALI kwa kushirikiana 
na wadau inaendelea kutekeleza mpango wa miradi ya miaka mitano wa 
kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga wakati wa kujifungua na walio
 chini ya miaka mitano ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma ya mama na mtoto na kuokoa maisha yao.
 Hayo yameelezwa na Daktari bingwa
 wa akina mama na watoto wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ,Dk Koheleth 
Winani, kwenye kikao cha pamoja na baadhi ya wakuu wa  mashirika 
mbalimbali wanaohudhuria mkutano mkuu wa kimataifa wa afya ya mama na 
mtoto, wanaoshirikiana na serikali kutekeleza mpango huo wa kupunguza 
vifo vya mama na watoto nchini walipokuwa wakitoa ufafanuzi wa maswala 
mbalimbali kwa wanahabari.
 Dakta Winani, amesema 75% ya 
watanzania wanaishi vijini ambako hawapati huduma zilizo bora wakati wa 
kujifungua kutokana na umbali na maeneo mengine kutopitika hasa wakati 
wa maska kutokana na miundo mbinu duni na kusababisha wajawazito 
kujifungulia majumbani au wengine kupoteza maisha wakati wakipelekwa 
kwenye Hospital , Vituo vya afya na Zahanati..
 Amesema kuwa mpango huo unalenga 
kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito na watoto 500 mwaka 2000 hadi 
kufikia 19 ifikapo mwaka 2015 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo 
ya Milenium, na kusisitiza kuwa ushirikiano kati ya serikali na wadau 
hao ni muhimu kwa kuwa serikali peke yake haiwezi kutekeleza mpango huo 
kwa ufanisi.
 Kwa upande wake daktari Dustan 
Bishanga, ambae ni mkurugenzi wa mradi wa Maisha unaofadhiliwa na 
,shirika la misaada la Kimarekani, USAID , kwa kipindi cha miaka mitano 
kuanzia mwaka 2008 kwa thamani ya Dola milioni 40 umeboresha huduma ya 
afya ya mama na mtoto mchanga.
 Dakta Bishanga, amesema  mradi 
umetengeneza mwongozo unaotumika na wadau wengine kutekeleza mradi hiyo 
,pia mradi huo unatengeneza mitaala ya kufundishia  watoa huduma kwa 
kushirikiana na wizara ya afya ili kutoa mafunzo  na uratibu wake katika
 vituo tofauti tofauti vipatavyo 250 nchini kote Tanzania bara na 
Zanzibar lengo ni kuboresha huduma ya mama na mtoto mchanga na kuokoa 
maisha
HABARI ZA UA MIGUU TFFCHAGUZI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA W
WATATU WACHUKUA FOMU ZA URAIS TFF
Wadau watatu wa mpira wa miguu 
wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu 
Tanzania (TFF) na kufanya idadi ya waliojitosa katika uchaguzi huo 
utakaofanyika Februari 24 mwaka huu kufikia 30.
 Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa 
wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile 
zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
 Waliochukua leo (Januari 16 mwaka
 huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne 
Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), 
Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa 
Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo.
 Mwengine aliyechukua leo ni 
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias 
Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuwakilisha 
Kanda ya Iringa na Mbeya.
 Orodha kamili ya wadau 
waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal 
Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael Wambura, Ramadhan 
Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais).
 Kwa upande wa wajumbe wa Kamati 
ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita),
 Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara 
na Mwanza). 
SERIKALI KUFUATILIA MAENDELEO YA MIRADI INAYOZINDULIWA WAKATI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU
Mkurugenzi
 wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
 Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza kwa wajumbe
 wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kuhusu 
serikali kufuatiliaji  maendeleo ya miradi inayozinduliwa wakati wa mbio
 za Mwenge mjini Zanzbar.
Mkuu
 wa mkoa wa Shinyanga  Ali Nassoro Lufunga akizungumza na viongozi na 
waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu 
maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013.Mkoa wa shinyanga 
ulikuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kwa mwaka 2012.
…………………………………………….
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 Zanzibar.
Serikali inaandaa utaratibu wa 
kufuatilia maendeleo ya miradi yote inayozinduliwa wakati wa mbio za 
Mwenge wa Uhuru ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakua endelevu na 
kuwanufaisha wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini 
Zanzibar na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka 
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole 
Gabriel wakati akitoa tathmini ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2012 na 
maendeleo ya miradi iliyozinduliwa wakati wa mbio hizo kwenye mkutano wa
 viongozi na waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Amesema serikali ina wajibu wa 
kufuatilia kwa karibu miradi yote iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2012
 katika Halmashauri za wilaya, manispaa na Miji ili kuhakikisha kuwa 
gharama kubwa iliyotumika wakati wa uanzishaji na ujenzi wa miradi hiyo 
inawanufaisha wananchi kutoka kizazi kimoja hadi kingine ili kutunza 
hadhi na heshima ya Mwenge wa Uhuru.
Amesema mbio za Mwenge wa uhuru 
zimezindua miradi mingi nchini yenye thamani ya mabilioni ya fedha na 
kuongeza  kuwa si dhamira ya serikali kuona kuwa mwenge wa uhuru 
unatumika tu kuzindua miradi ya maendeleo bali kuhakikisha uendelevu wa 
miradi hiyo.












































































No comments:
Post a Comment