TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, March 24, 2016

Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani katika jeshi la kuzima moto na uokozi, na Mkandarasi. Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd Bw. Webu Manoth Masawe wamehukumiwa leo tarehe 24/3/2016 kwa kesi ya kuhujumu uchumi katika Mahakama ya wilaya ya Ilala.

Aliyekuwa Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani katika jeshi la kuzima moto na uokozi na Bw. Naamini Hendry Sangiwa pamoja na Mkandarasi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd Bw. Webu Manoth Masawe wamehukumiwa leo tarehe 24/3/2016 kwa kesi ya kuhujumu uchumi katika Mahakama ya wilaya ya Ilala. Hukumu hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Hassan.

Washtakiwa tajwa hapo juu walishtakiwa kwa makosa 7 yakiwemo Matumizi Mabaya ya Madaraka, Kutumia Nyaraka Kumdanganya Mwajiri kinyume na kifungu cha 22 na 31 mtawalia vya Sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007, Kughushi Nyaraka kinyume na Kifungu cha 333, 335 (d) (1) na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, na kuisababishia Serikali hasara kinyume na Aya ya 10(1) ya Jedwali la Kwanza, Kifungu cha 57(1) na 60(1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200.

Mnamo mwaka 2009 Serikali ilitoa zabuni ya Ujenzi wa uzio wa Chuo cha Zimamoto na Uokozi kilichopo Mbopo Bunju katika Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Kiareni Investment Ltd (Mzabuni), ilipatiwa zabuni hiyo na kulipwa Kiasi cha Shilingi 81, 963, 360/=.
Hata hivyo taratibu za utoaji zabuni hazikufuatwa, na Mzabuni ambaye ni Kampuni ya Kiareni Investment Ltd, alifanya kazi yenye thamani ya kiasi cha Shilingi 13, 784, 652/= tu kati ya fedha yote aliyolipwa. 

Ili kuwezesha malipo ya Shilingi 81, 963, 360/= kulipwa pasipo kazi kukamilika, Washtakiwa walitoa zabuni kwa Mkandarasi pasipo Mkataba (LPO), na Kughushi Hati ya kuonesha kazi imekamilika (Certificate of Works Completion).
Washitakiwa wote watatu walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mwanzoni mwa mwaka 2014 na kusomewa mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mkazi Hassan, ambapo washitakiwa walifunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi No. 06/2014. 

Upande wa Jamhuri katika Kesi hii uliwakilishwa na Wakili STANLEY HILMAR LUOGA akisaidiana na Wakili EMMANUEL JACOB, wote waendesha Mashitaka wa TAKUKURU Makao Makuu.
Upande wa washtakiwa wote waliwakilishwa na Wakili wa Kujitegemea MDUMA.
Upande wa Jamhuri uliita Mashahidi 7 na kupeleka vielelezo 21 ili kuthibitisha kesi dhidi ya washtakiwa. Upande wa washtakiwa hawakuita shahidi hata mmoja walijitetea wenyewe.
Mshitakiwa wa kwanza Dotto Salehe Mgogo, ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Mafunzo wa Wizara ya Mambo ya Ndani katika idara ya Jeshi la Zimamoto na Uokozi alifariki dunia mwaka 2014 baada ya kusomewa mashitaka na hivyo Mashitaka dhidi yake yalifutwa kwa mujibu wa sheria. 

Kufuatia kifo cha Mshitakiwa wa kwanza, Mshitakiwa wa Pili Bw. Naamini Hendry Sangiwa ambaye alikuwa Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Katika Jeshi la Zimamoto na Uokozi alikuwa anakabiliwa na makosa manne (4) ambapo makosa mawili ni ya Matumizi Mabaya ya Madaraka, Kughushi na Kuisababishia Serikali Hasara, ametiwa hatiani katika makosa yote mawili ya Matumizi ya Madaraka na kupewa adhabu ya kulipa faini ya Tshs.300, 000 kwa kila kosa la Matumizi Mabaya ya Madaraka kama atashindwa kulipa faini, kwenda jela miezi 6 kwa kila kosa.

Katika Kosa la Kughushi Nyaraka, Mshtakiwa ametiwa Hatiani na Kuamriwa kutotenda kosa lolote la jinai kwa muda wa miezi 12.
Mshitakiwa wa tatu ambaye ni Bw. Webu Manoth Masawe, ambaye ni Mkandarasi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd, anakabiliwa na Kosa moja la Kuisababishia Serikali Hasara.
Mahakama imemtia hatiani na kumpa adhabu ya kwenda Jela miaka mitatu (3) pamoja na Kuirudishia Serikali kiasi cha Shilingi 67, 913, 748/= ikiwa ni hasara aliyoisababishia Serikali.

IMETOLEWA NA OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
24 MACHI, 2016

............Comments.................
Muddy Muddy Kosa la kughushi lina exception kumbe.ninavyofahamu nikifungo cha miaka saba hiyo hukumu ya kughushi ni JIPU

Like · Reply · 2 · 5 hrs
Kayanda Nurdin
Kayanda Nurdin komaa komaa,mhe............!!
مجوو سعيد ابراهيم
مجوو سعيد ابراهيم Endelea kuwanyoosha mweshimiwa magu
Abbs Chris Maheri
Abbs Chris Maheri Laki 3 tuu kwa kosa la matumizi mabaya? Afu matumizi hayo yamepelekea hasara ya 67mil.Izi sheria ziangaliwe upya.
Like · Reply · 1 · 5 hrs
Abeid Mbano
Abeid Mbano Adhabu hazitoshi Hawa mahakim na majaji wanabidi wafatiliwe hata kama sheria inataka mahakama kuwa huru lakini nivyema kuvunja sheria kwaniaba ya watanzania walio wengi mfano mtu anaiba billion 10 unaenda kumuhukum miaka 3 sasa hata mimi ukiniambia unanipa billion 10 halafu nikafungwe miaka 3 nakubali namaanisha adhabu zinanzotolewa hazitoshi hata kidogo lazima mtu afungwe miaka 20 au 30 ndio itakua fundisho
Abeid Mbano
Abeid Mbano Naomba nitoe maoni zaidi 0714297033
Ally Khatibu BabaNeyuu
Ally Khatibu BabaNeyuu Hii.sheria mbona siielewi mtu anahujumu mabilioni anafunga miaka michache mfano miaka 3..mwingine kagushi majina hewa ya wanafunzi kaipatia serikali hasara ya milion 4 kafungwa miaka 23...sielewi
Like · Reply · 1 · 4 hrs
Henry Sufa
Henry Sufa A Luta Continua....waliokuwa wanajilipa mishahara hewa warudishe pesa zetu au kufilisiwa (sijui kama sheria inaruhu) na baada ya hapo gerezani.
Chande Kijuni
Chande Kijuni dah mbona adhabu ndogo sana kias hiki? kwa nini lakini? kuisababishia hasara serikali ni kosa kubwa mno adhabu ndogo hiyo bkra ijengwe tu hiyo mahakama ya mafisadi
Mnyamani Amiri
Mnyamani Amiri Serekali bado muangalia na kesi ya Askari wa Zima moto waliostaafishwa kinyume cha taratibu. Wale wazee wamefanyiwa figisu, wapewe haki Yao.
Mickah Peter
Mickah Peter Yule wa milungi kahukumiwa kifungo chamaisha,hyu matumizi mabaya ya ofisi lak 3,anyway kuna siku ambo yatabadilika
Sohail Thakur
Sohail Thakur Very good..wako wengi tu kila kona kama hao..fuatilieni
Agano John Ng'asi
Agano John Ng'asi Kama sheria ndivyo zinavyosema ,basi waacheni wapete.pia nadhani adhabu hizo ziliwekwa na watu ambao walikuwa wanafikiria kuwa nawao yanaweza kuwakuta so adhabu ziwe ndogo.
Jozee Simba
Jozee Simba Kama mtu kakamatwa na mirungi huko Kilimanjaro kafungwa maisha je kuhujumu uchumumi inakuwaje? Duuuh Mimi napita tuu
James Bombi
James Bombi angekua mwizi wa cm au tv miaka 5 au 10 jela duh! kwel noma
Izack Musa
Izack Musa Sijaridhika, wote walishirikiana kuhujumu nchi, je hukumu si sahihi
Wafungwe kama yule wa ngorongoro
Deusdedith Rwebangira
Deusdedith Rwebangira Pccb ihundwe upya na kufuta iliyopo imekuwa sehemu ya tatizo kidonda sugu jamii inakilalamikia hawahfanyi kazi wanaishia vikesi vya watendaji wa vijiji kifutwe kiundwe upya.
Sadock Mahanga
Sadock Mahanga Safi sana kwa kazi nzuri. Ila pia mngewafilisi kabisa iwe fundisho kwa wengine.
Naboth Longo
Naboth Longo kazi nzuri ila adhabu ni ndogo sana, tunaomba sheria ziangaliwe upya hasa wakati wa kuaandaa mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi. adhab zinatakiwa kuwa kubwa.
George Mzule
George Mzule Upuuz uleule
Like · Reply · 1 hr
Samweli Njama
Samweli Njama Hivi jamani huo sikutufanya watoto huyu mwenye faini silaki tatu makosa matatu la tisa sasa kala shiringi ngapi asiweze kutoa faini ahsanteni sana kwa kutuona wajinga.

No comments:

Post a Comment