TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, April 18, 2016

HADITHI: NDOA YA MTOTO WA TAJIRI BILIONEA NA MTOTO WA MASIKINI_MKULIMA.( SEHEMU YA PILI).



Zilikuwa ni ndoto za alfajiri wakati nilipostuka kutoka usingizini, nikagundua kwamba nilitoka kwenye lindi la mawazo mazito(ndoto) ambazo zilinionyesha jinsi viumbe walivyoweza kubarikiwa na mungu kuishi wawili wawili, hapo hapo niliinuka haraka hadi bafuni ambapo niliweza kujimwagia maji kasha nilivaa nguo kwa ajili ya kwenda kanisani.
Kwa upande wa Regina yeye ilikuwa ni tofauti baada ya kuwa ametoka kwenye viwanja vya michezo yetu ya kikapu maeneo ya Tanesco drive in opposite na jingo la drive in Cinema(Ubalozi wa Marekani), alikuwa amechanganyikiwa kutokana na kauli zangu kwake siku hiyo, ambapo aliondoka bila furaha kuelekea nyumbani kwake mikocheni maeneo ya mlalakuwa katika nyumba za watu matajiri, akiwa na gari aina ya rand lover discover, akuweza kufika nyumbani salama baada ya kupata ajali mbaya ambayo hata hivyo ni gari pekee iliyoweza kuharibika huku yeye akitoka mzima bila jeraha lolote.


Maisha yaliendelea tena kama kawaida ambapo siku iliyofuata mimi kama kawaida yangu siku za jumatatu hadi ijumaa uwa ni lazima kufanya mazoezi asubuhi na jioni, hivyo nilikwenda mazoezi ya mpira wa miguu, ambapo niliamka mapema sana ili kuwahi kwenda kwenye miangaiko yangu ya kila siku motto wa mlala hoi, nakumbuka nilikuwa nasoma huku nafanya kazi za vibarua mbali mbali kwenye viwanda na mida ya jioni nilipendelea kwenda kwenye viwanja vya michezo ili kutimiza ndoto yangu ya kucheza basketball(mpira wa kikapu).

Jambo moja kubwa tulilokuwa nalo kwa kila mmoja wetu, yaani mimi na Regina ni ushawishi wa kuweza kusikilizwa na watu, na mara zote alipokuwa amesimama regina basi utakuta amejaliwa na vijana wakiendelea kumsikiliza , naye bila ajizi alikuwa akipenda sana kuwapa michapo mbali mbali za hapa na pale ikiwemo stori za soka la majuu, zaidi ikiwa ni ligi ya uingereza na mchezo wa kikapu nchini marekani, maana nakumbuka wakati huo bado kulikuwa na uhaba wa vyombo vya habari hivyo wenye pesa ndiyo waliokuwa wakitazama zaidi mambo ya kwenye mitandao na hata tv pia walikuwa nazo wachache.

Baada ya kufika uwanjani muda huo nikitokea kwenye viwanja vya mchezo wa soka ili niende kucheza kikapu, na nilipofika uwanjani taa za uwanja zilikuwa zimezima kutokana na itilafu ya umeme, hivyo siku hiyo hakukuwa na mazoezi zaidi ya kupiga stori na wakati huo tayari regina alikuwa bize kuwapa michapo, ndipo mimi baada ya kuwasili eneo hilo maana sikuwa na tabia ya kwenda kujichanganya sehemu alipokuwa regina, nilikuwa na tabia ya kukaa  sehemu ingine ili kumpa uhuru wake na pia sikupenda kujichanganya kuwa mmoja wa wasikilizaji wake au wapambe wake.

Lakini jambo kubwa nililokuwa pia likimuumiza kicha ni pale ambapo alikuwa akishindwa kuelewa jambo hili, nikiwa sipo uwanjani alikuwa akisikilizwa yeye wakati wote lakini mara nilipokuwa nikiwasili maeneo hayo vijana wengi walikuwa na tabia pia ya kuja kwangu kunisikiliza, maana nakumbuka nilikuwa na vipaji vingi sana, wakati huo nilicheza mpira wa migu katika timu ya taifa ya vijana wenye umri wa miaka chini ya 23, lakini pia nilikuwa naigiza filamu ya Oparation ya hatari, iliyokuwa gumzo kwa wakati huo, mtunzi wake akiwa ni nyakasagani masenza, mtunzi maarufu sana wa adithi natamthilia  za cinema.

   Ilibidi niamaki baada ya kuona vijana wote wametoka kwa regina ambaye alikuwa anawapa michapo na sasa wameamia kwangu, moyoni nilitamani waendelee kumsikiliza yeye, lakini aikuwa hivyo waliweza kumwacha mpweke, kitendo ambacho mimi hakikuwa kikinifurahisha, alibaki peke yake eneo alilokuwa akiwasimulia vijana habari zake, na kwa kuwa mafahari wawili hawakai zizi moja yeye pia hakuwa na desturi ya kuja eneo nililokuwapo, ni kama tulikuwa na tabia zinazofanana kimatendo, hivyo aliishia kunitazama tu hadi ilipofika wakati wa kuondoka maeneo hayo ya viwanja.

Kwa kuwa siku hiyo hakukuwa na umeme, nilipata fulsa nzuri ya kuweza kumtokea bint rafiki yake regina Edna, kwa kweli alikuwa ni dada mrembo ambaye pia alikuwa amebarikiwa kuwa mchezaji hodari sana wa mchezo huo, na katika timu ya pazi qeen yeye na regina ndiyo waliokuwa wachezaji wakali kutokana na kuufahamu vyema mchezo huo wa kimarekani, wengine walikuwapo kwa upande wa timu ya wadada lakini hawakuwa wakicheza lama hawa, naweza kusema kwamba walikuwa wakijifunza zaidi katika kuutambua mchezo huo chini ya kocha mzoefu wa siku nyingi Kalemaa mkongo aliyebobea Tanzania katika fani ya ufundishaji wa mchezo wa kikapu, na alifanikiwa kuinua vipaji vingi kwa upande wa timu ya wavulana na wasichana.

Baada ya kufanya mazungumzo ya kina na Edna dauson, akusita kunikatalia wazi wazi kwa madai yake, ambapo aliweza kunieleza juu ya upendo aliokuwa nao dada yake kwangu, edna alinieleza vitu vingi sana kuhusu regina na azima yake kwangu, kwamba asitaili kuwa mpenzi wangu kwa kuwa yupo ambaye alikuwa akinitamani usiku na mchana, ambaye ni regina, “dada yangu anakupenda sana shaaban, na sijui kama unatambua hilo, si unamuona mwenyewe amefikia umri wa kuwa na mume, sasa wewe kwa nini usipeleke barua ya kwenda kuchumbia? Au utaki awe mke wako, niambie shaaban, na ikitokea akakuta umesimama na mimi hapa sijui nitambebea mbeleko gani, tafadhali nakuomba sana usije ukanigombanisha na rafiki yangu, wewe ukitaka mfuate yeye mweleze maana yupo na anakuzungumzia kila siku, na hata ujio wake hapa siku hizi ni kwa ajili yako, nadhani umenielewa shaaban” alimaliza edna nikabaki nimeduwaa sina jibu.

Ilikuwa ni siku ya jumatano nilipopigiwa simu kupewa taarifa ya kwenda kujiunga na timu ya mpira wa miguu iliyokuwa ikishiriki ligi kuu ya Tanzania, wakati huo ikijulikana kama safari lager, nilitakiwa kwenda kwenye majaribio mjini Dodoma kujiunga na timu ya CDA watoto wa nyumbani, hivyo sikuwa na njia ingine zaidi ya kuondoka jijini dare s salaam kuelekea Dodoma kwa ajili ya kufanya majaribio nakumbuka ulikuwa mwezi wa kumi baada ya kuwa ligi kuu imemalizika na wakati huo timu zote za ligi kuu zilikuwa katika maandalizi ya kufanya usajiliwa wachezaji.

Sikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na regina, maana tulikuwa hatujazoeana na wote kila mmoja alikuwa ni fahari kwa mwenzie, kwa tabia yangu ya kutopenda kujipendekeza kwa mtu au kunyenyekea kwa watu wenye pesa, sikuwahi kuwa mtumwa wa aina hiyo, niliamini nab ado naamini kwamba maisha siyo pesa, unaweza kuwa na pesa lakini ukawa hauna afya nzuri, kikubwa mimi niliamini kwamba maisha ni kumtumainia mungu pekee, hivyo niliishi Dodoma kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye hoteli ya jambo lee.

Nilirejea dare salaam baada ya mwaka mmoja, na kwa kipindi hicho chote sikuweza tena kuwasiliana ama kukutana na regina, sikuwa nimemuweka sana moyoni kwa wakati huo kutokana na kwamba yeye alionekana kuwa na umri mkubwa sana, na hata maelezo ya edna pia niliyasikiliza lakini sikumpa majawabu zaidi ya kubaki natafakari juu ya maelezo aliyokuwa ameniwasilishia edna.

 Baada ya mwaka mmoja kupita nilirejea tena kwenye makazi yangu maeneo hayo ya drive in, nakumbuka nilirudi majira ya saa za jioni na kupitia maeneo hayo ya viwanja vya wazi drive in tanesco, na kwa bahati nzuri siku hiyo kulikuwa na watu (vijana wengi) waliokuwa wamekwenda kufanya mazoezi na wengine kuangalia, mara baada ya kuniona ilikuwa kama shangwe maana vijana kutokana na kutoniona kwa kipindi cha mwaka mmoja, wengi walikuwa na hamu sana ya kuniona na hakika walikuwa wamemisi sana habari na dondoo za stori nilizokuwa nikiwapa, ghafla nilijikuta nimezungukwa na kundi la vijana wengi walipenda kuniita kaka shaaban, “kaka shaaban karibu sana,yaani tumekumisi sana kaka yetu,  ilikuwa ni kauli ya Kelvin ambaye tuliishi nyumba jirani, nilipenda sana kuwa naye karibu katika kumfundisha mambo mbali mbali, asante mdogo wangu nimerudi tena kwa hiyo tuko pamoja, nawaomba nifike nyumbani kwanza niweke mizigo yangu kisha nitarejea tena, niliwaacha vijana wengi na shahuku kubwa ya kuningoja nirudi, nawakumbuka kina Eric Mwingizi, Dotto, Gwantwa Mwasakyeni pamoja na wengine wengi akiwepo mdogo wangu(Milobo Mkama) ambaye ni afrikast yaani chotara wa kizungu niliyekuwa nikiishi naye nyumba moja.

Ni siku ya jumamosi ilikuwa wakati nimeamka asubuhi nikiwa na uchovu wa safari  pamoja na uchovu wa mzunguko wa muda wa mwaka na timu ya CDA ya Dodoma watoto wa nyumbani, kwa kuwa niliitaji kupumzika zaidi siku hiyo sikuweza kuamka asubuhi kama inavyokuwa kwa siku zingine, nilihisi uchovu sana hivyo niliamua kupumzika tu kusubiri kwenda kuangalia na kujifunza kucheza mpira wa kikapu, na kama unavyojua tena mchezo wa kikapu ni mchezo wa watu wastarabu ambao hawapendi kuchafuka, na sifa yao kubwa ni kwamba utofauti uliopo kati ya wacheza soka na wacheza kikapu ni jinsi ya miili yao, wacheza soka wao misuli yao imekakamaa sana, kutokana na kufanya mazoezi sana wakati wa jua kali, huku wacheza kikapu wao misuli yao iko laini kutokana na kufanya mazoezi muda mwingi wakati wa usiku ama eneo ambalo jua limepungua hivyo wanaonekana laini hata kama misuli yao imejengeka, lakini uwezi kulinganisha na wacheza soka.

Niliamka majira ya saa nne, nikaenda kujimwagia maji, kasha niliweza kunywa chain a wadogo zangu, Aghata, emele, joo na jovi mkama ambao kwa wakati huo walikuwa ni wadogo na walinipenda sana, hivyo muda mwingi walifurahi kutembea na mimi na hata wakati mwingi pia niliweza kwenda nao maeneo hayo ya uwanja nikiwa pia na binamu yangu mzungu Eugen.

Kati ya vitu ninavyovipenda sana ni ufugaji wa wanyama, hivyo nilikuwa na mifugo hapo nyumba (Mbuzi) ambao sikuona aibu kuwatoa na kwenda kuwafunga kwa ajili ya kupata chakula, na wakati mwingine nilipenda kwenda kuwafunga pembezoni mwa viwanja vya kikapu vilivyopo ndani ya makazi yetu, hiyo ilikuwa ni tabia yangu ya kila siku kuwakumbuka mbuzi wangu kwenda kuwatafutia maeneo ambayo wangeweza kupata majani mazuri.

Shaaban mpalule, iliita sauti kutoka kwa rafiki yangu Aluta Warioba, na mimi niliitika, bwana mkubwa, nikiwa namaanisha ni heshima ambayo utolewa na watu waliopo Gerezani wakiwa na maana ya kuwapa heshima askari magereza na heshima hiyo ilikuwa kama imekuwa ni tabia kwa rafiki zangu, na hiyo ilitokana na mimi mwenyewe kuwa niliwahi kuishi gerezani wakati nilipokwenda kufanya utafiti kuchunguza vifo vya mahabusu vilivyokuwa vikiendelea ndani ya gereza hilo.

Wakati huo tulikuwa kwenye viwanja hivyo na muda huo tayari wachezaji wengi walikuwa wameshafika eneo hilo akiwepo Regina wakiendelea na mazoezi kama kawaida ya siku za mazoezi viwanjani hapo.

Usikose kufuatilia Adithi hii kila siku 0713869133/0767869133

No comments:

Post a Comment