TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, April 21, 2016

Benki ya Exim yashiriki mbio za Ngorongoro kuikabili Malaria


BENKI ya Exim Tanzania imeshiriki kikamilifu kwenye mbio za tisa za Ngorongoro ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa kupitia mbio hizo katika kukabiliana na ugonjwa wa malaria hapa nchini.

Mbio hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita wilayani Karatu chini ya ushiriki wa Waziri wa Maliasiri na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, aliyekuwa mgeni rasmi zinalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria sambamba na kusaidia elimu ya awali kwa jamii wa Wamasai waishio jirani na kivutio hicho.

Mbali na kushiriki katika udhamini wa mbio hizo baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walijumuika na washiriki wengine katika mbio za kilometa 5 zilizohusisha kundi la washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali (corporate challenge category). Watoto pia walipewa fursa ya kukimbia mbio fupi za kilometa 2.5, wakati shindano refu lilikua la kilometa 21 tokea Ngorongoro hadi Karatu.

“Ni wazi kwamba taasisi za kifedha tukiwemo Benki ya Exim ustawi wetu unategemea sana uwepo wa jamii yenye afya na ndio maana tumekuwa mstari wa mbele kushiriki mbio hizi kwa maana ya kuhamasisha michezo lakini pia kuunga mkono malengo yake yaani kuikabili malaria na kusaidia elimu,’’ alisema mwakilishi wa benki hiyo Bw. Emmanuel Mwamkinga, meneja wa benki ya Exim tawi la Karatu.

Aliongeza kuwa benki hiyo itaendelea kushiriki katika kusaidia michezo na matukio mbalimbali hasa yale yenye kuleta tija kwa jamii hususani kwenye sekta ya afya, elimu na mazingira.

Katika mbio hizo zilizoanzia katika lango la kuingilia na kutokea Hifadhi ya Ngorongoro na kuishia kwenye uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu ilishuhudiwa mwanaridha Ismail Juma akivunja rekodi ya mbio hizo kwa kutumia saa 1:02:48 na kuipiga kikumbo ile ya awali ya saa 1:03:00 iliyowekwa miaka ya nyuma.
 

No comments:

Post a Comment