Wizara
 ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inaadhimisha miaka 50 ya Chuo 
cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 27 
Januari 2014 mpaka tarehe 31 Januari 2014.
Maadhimisho
 ya miaka 50 haya yataenda sanjari na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wizara 
utakaohusisha Maafisa Maendeleo ya Jamii  wa Mikoa na Wilaya kutoka 
Tanzania nzima wanaofanya kazi katika Halmashauri zetu, Wakuu wa Vyuo 
vya Maendeleo ya Jamii, Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na Wadau
 wengine.
KAULI MBIU YA MAADHIMISHO YA MWAKA 2014 NI;
“Taaluma ya Maendeleo ya Jamii: Nyenzo Muhimu katika Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini wa Kaya”.
Vilevile
 kutakuwa na maonesho  ya kazi za mikono, kutoka katika vikundi vya 
wanajamii wa Halmashauri za Arusha na Arumeru. Mfuko wa Taifa wa Bima ya
 Afya (NHIF) watafanya maonyesho, pia watatoa huduma za afya kwa jamii.
Hivyo, wanakaribishwa wadau na wananchi wote kwa ujumla kushiriki maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha
IMETOLEWA NA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO KWA HISANI YA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA

No comments:
Post a Comment