Rais
 mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiapishwa rasmi rais wa 
nchi hiyo mjini Antananarivo kufuatia ushindi mkubwa alioupata katika 
uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013. 

 Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akisani kiapo chake 
tayari kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa Madagascar mbele ya Jaji 
Mkuu wan chi hiyo Jean –Michael Rasolonjatovo (kushoto) wakati wa 
sherehe za kumuapisha rais huyo zilizofanyika mjini Antananarivo. 
 
 
Rais
 mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akizungumza na wananchi wa 
Madagascar  waliofurika ndani ya uwanja wa Antananarivo mara baada ya 
kuapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo mjini. 
 
Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe 
akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumuapisha rais 
mpya wa Madagascar akiwa kwenye jukwaa kuu pamoja na viongozi wengine wa
 nchi za Afrika waliohudhuria sherehe hizo mjini Antananarivo.Wengine 
wanaoonekana kutoka kulia ni Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano, 
Rais wa Zambia Ipikefunye Pohamba na aliyekuwa rais wa Madagascar Andry 
Raojolina. 
Viongozi
 mbalimbali na wanachi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya 
wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina mjini Antananarivo 
 
Viongozi
 mbalimbali na wanachi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya 
wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina mjini Antananarivo 
 
Gwaride maalum la jeshi la Madagascar wakati wa sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Hery Rajaonarimampianina. 
 
 
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akikagua gwaride la majeshi ya Madagascar baada ya kuapishwa. 
 
 
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiwasili Ikulu ya nchi hiyo mjini Antananarivo.
……………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Antananarivo, Madagascar.
Tanzania
 imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Madagascar katika masuala 
mbalimbali  na kuhakikisha kuwa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo na 
jumuiya za kimataifa vinaondolewa kufuatia nchi hiyo kurejesha utawala 
wa kidemokrasia.
Akizungumza
 katika mahojiano maalum  mjini Antananarivo, Madagascar, Waziri wa 
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe amesema kuwa 
sasa serikali ya Madagascar imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano sio tu
 na Tanzania bali nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa 
Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya za kimataifa.
Waziri
 Membe ambaye alikuwa amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe 
za kuapishwa kwa rais mpya wa Madagascar Bw. Hery Rajaonarimampianina 
zilizofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Antananarivo jana  amesema 
kuwa Tanzania imefurahishwa na hatua hiyo na kuongeza kuwa huo ni 
ushindi mkubwa kwa SADC.
Amesema
 kuwa mwaka 2009 Madagascar iliingia katika machafuko yaliyosababisha 
serikali halali iliyokuwepo madarakani ya Rais Mark Ravalomanana 
kupinduliwa na kufafanua kuwa Tanzania ikiwa Mwenyekiti wa Kitengo cha 
Amani na Usalama cha nchi za jumuiya ya SADC (TROIKA) imekuwa mstari wa 
mbele kuhakikisha kuwa amani ya kudumu inapatikana nchini humo.
“Kiongozi
 mpya wa Madagascar aliyepatikana na kuapishwa ni ushindi kwa Tanzania 
kwa sababu Rais Jakaya Kikwete amejihusisha sana na upatikanaji wa 
kiongozi huyo, kama tunakumbuka rais Kikwete alimuita nchini Tanzania 
kwa mazungumzo rais aliyekuwa madarakani Bw. Andry Rajoelina mara nne, 
mazungumzo haya yamezaa matunda tunayoyaona leo” amesema Mh. Membe. 
Amefafanua
 kuwa yapo mambo makubwa ambayo Tanzania imeyafanya kufanikisha 
kupatikana kwa amani ya kudumu nchini Madagascar ikiwemo upatikanaji wa 
katiba  ambayo ilikamilika mwezi wa 8 mwaka 2013 ,kufanikiwa 
kuwashawishi Andry Rajoelina na Mark Ravalomanana waliokuwa mahasimu 
kutoshiriki kugombea katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Amesema
 Tanzania imefurahishwa na kitendo cha rais Andry Rajoelina aliyeingia 
madarakani kwa kufanya mapinduzi kukubali kuachia madaraka na kuachia 
utawala wa demokrasia utawale nchini humo.
Ameeleza
 kuwa Tanzania sasa iko tayari kushirikiana na Madagascar na kama mjumbe
 wa SADC itahakikisha kuwa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo vinaondolewa 
pia kuhakikisha kuwa kiongozi huyo mpya anashiriki mkutano wa wakuu wa 
nchi za Afrika utakaoanza tarehe 30 mwezi huu.
 “Tulimwahidi
 rais aliyekuwa madarakani Bw. Andry Rajolina kuwa atakapotekeleza hayo 
tunayoyataka ikiwemo kuanzisha mchakato wa katiba,  kuruhusu utawala wa 
demokrasia, na kuruhusu uchaguzi ili kupata rais mpya sisi tutakuwa 
mstari wa mbele kushawishi nchi za SADC na nchi za AU kuwaruhusu 
kushiriki mikutano yote ili waweze kuijenga nchi yao na jambo hilo 
tutalifanya ” amesisitiza Mh.Membe. 
Katika
 houtuba yake mara baada ya kuapishwa rais Rajaonarimampianina amesema 
kuwa utawala wake unaanza ukurasa mpya wa kuijenga upya nchi hiyo 
iliyokuwa imegawanyika kisiasa na kusababisha chumi wake kudorora huku 
akiueleza umati mkubwa wa watu waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake 
kuwa ataongeza mapambano dhidi ya rushwa na kuleta amani, utulivu na 
maridhiano kwa mustakabali wa taifa hilo.
Madagascar
 ambayo sasa inaingia katika utawala mpya wa rais Hery 
Rajaonarimampianina ambaye hapo awali alikuwa Waziri wa Fedha wa nchi 
hiyo iliingia katika machafuko yaliyosababisha kuondolewa kwa utawala wa
 rais Mark Ravalomanana aliyekimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini.
 Hery
 Rajaonarimampianina  akiungwa mkono na rais aliyepita Andry Rajoulina 
anakuwa rais wa 4 wa nchi hiyo  kufuatia ushindi  mkubwa alioupata 
katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013 
uliompatia  asilimia 53.3  dhidi ya mpinzani wake Bw. Jean Louis 
Robinson aliyepata asilimia 46.5.
No comments:
Post a Comment