Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing
………………………………………………………………………………………
Na Immaculate Makilika –Maelezo.
Serikali
 ya Jamhuri ya watu wa China jana  katika uwanja wa Taifa wa  Uhuru 
jijini Dar es salaam imesheherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa 
uhusiano baina ya China na Tanzania ,ikiwa pia ni siku ya mwaka mpya wa 
kichina ambayo hujulikana kama sikukuu ya “Spring”. 
Katika
 kusheherekea siku hiyo Serikali ya China pamoja na makampuni 
yamechangia zaidi ya milioni 300 katika huduma za kijamii,huku michango 
hiyo  ikiwa kama ifuatavyo; Serikali ya watu wa China imechangia milioni
 100 kwa ajili ya kuchimba visima,Uhifadhi wa wanyamapori na mafunzo kwa
 wenyeji,wafanyabiashara wa China wamechangia milioni 50 kwa ajili ya 
visima na elimu huku Jumuiya ya Ujenzi wa Afrika wamechangia milioni 15 
kwa ajili ya viatu vya wanafunzi.
Halikadhalika,Kampuni
 ya Madawa imechangia milioni 25 kwa ajili ya madawa ya kutibu 
malaria,huku milioni 100 zilichangwa na Jumuiya ya Muungano wa Wachina 
na fedha hizo zikielekezwa kwa vijana na wananchi wa Tanzania na 
kuhitimishwa na mchango kutoka Benki ya Biashara ya China ambayo 
imechanga milioni 20 kwa ajili ya vijana na elimu ya Tanzania.
Aidha
 ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary 
Nagu aliyekuwepo kwenye sherehe hizo kwa niaba ya Waziri Mkuu  Mizengo  
Pinda, aliwashukuru sana watu Serikali ya China pamoja na 
wafanyabiashara na makampuni hayo  kwa misaada katika kuchangia 
maendeleo ya huduma za kijamii kwa watanzania.Urafiki wetu utaendelea 
kukua kwa faida ya watu wetu kama alivyosema waziri Nagu “China na 
Tanzania tunaurafiki wa dhati kwa muda mrefu sasa”.
Balozi wa 
China nchini Lu Youqing kwa upande wake alisema mwaka huu si tu 
kusheherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini pia 
ni miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China 
na Tanzania.“Mwaka uliopita nchi hizi mbili zilikua na ziara kwa kiasi 
kikubwa ,huku tukishuhudia ujio wa Rais  wa China Xi jinping, hali hiyo 
imeleta msukumo mpya wa mahusiano unaolenga kuleta manufaa yenye usawa 
kwa nchi hizi mbili”.
Alisema
 watu wa China wamejidhatiti katika kujenga Taifa lao la China, watu wa 
Tanzania na Afrika kwa ujumla pia wamejidhatiti kufufua ndoto za 
maendeleo kwa nchi zao,tuungane sote pamoja katika kutimiza ndoto zetu 
za maendeleo katika mwaka huu mpya.
Sherehe
 hizo zilizohudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi wa China nchini,huku 
wakionekana wenye furaha wakati wote na kufuatilia kwa makini kila aina 
ya burudani iliyokuwa ikiendelea uwanjani hapo.
Bwana
 Jerome Wu,mwananchi wachina alisema hii ni mara yake ya tatu kuhudhuria
 sherehe za mwaka mpya wa kichina akiwa nchini Tanzania na kuongeza kuwa
 amefurahishwa sana na utofauti uliopo mwaka huu,na kupongeza jitihada 
zinazofanywa na Serikali za nchi hizi mbili katika kudumisha urafiki huo
 na kuongeza kuwa yeye hupata fursa ya kukutana na jamaa na marafiki 
kwenye sherehe hizi.
Aidha
 viongozi mbalimbali wa Serikali na Jeshi  walihudhuria ikiwemo Waziri 
wa Katiba na Sheria Dr. Asha Rose Migiro,Waziri wa Ardhi, Nyumba na 
Maendeleo ya Makazi  Prof. Anna Tibaijuka na Naibu Waziri wa Nishati na 
Madini Stephen Masele.
Uhusianao
 baina ya nchi hizi mbili ulianzishwa na Baba wa Taifa hayati Mwl Julius
 Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong kwa nia ya kuhudumia wananchi 
wao,hatahivyo umekua ni uhusiano wenye manufaa makubwa kwa kusaidia 
kujengwa kwa reli ya Tanzania – Zambia,kiwanda cha nguo Urafiki, uwanja 
wa Taifa Uhuru, na miradi mingine ikiendelea ikiwa ni pamoja na  ujenzi 
wa Bandari ya Bagamoyo na bomba la gesi asilia toka Mtwara wakati miradi
 hiyo ikitazamiwa kuboresha uchumi na maisha ya watanzania pamoja na 
kudumisha urafiki huu baina ya Tanzania na China.

No comments:
Post a Comment