Waziri
 wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akisaini moja ya 
Leseni alizozitoa za uchimbaji Madini. Wanaoshuhudia, aliyesimama ni 
Kaimu Kamshina wa Madini anayeshughulikia Leseni Bw.  John Mayopa na 
anayeangalia ni Kamshina wa Madini Paul Masanja.
Mmoja
 wa Wamiliki Kampuni ya J.S Contractors Bw. Sisti Siyvester Mganga 
akieleza jambo kuhusu Kampuni ya J.S na namna itakavyofanya kazi. 
Kampuni hii inatarajia kuzalisha madini  aina ya ‘dimension stone’ na 
kokoto za ujenzi katika eneo la  Kihangaiko Bagamoyo.
Mwakilishi
 wa Kampuni Ya Osiris Gold T) Ltd. Bw.Shehzada Walli akimweleza Waziri 
wa Nishati na Madini Mhe. Prof esa.Sospeter Muhongo kuhusu Kampuni hiyo.
 Leseni  iliyosainiwa ya kampuni hiyo itaiwezesha kuchimba madini ya 
Dhahabu katika eneo la Rwamgaza Geita.
Mwakilishi
 wa Kampuni ya Kamal Steel akieleza jambo wakati wa kikao cha kusaini 
Leseni za Uchimbaji Madini. Kampuni hiyo imepewa Leseni ya kuchimba 
madini aina ya ‘Marble’ katika eneo la Kidayi Kilosa.
Na Asteria Muhozya
Waziri
 wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo   ameweka saini Leseni tatu 
za Uchimbaji wa Madini kwa Kampuni zinazotarajia kuzalisha madini aina 
mbalimbali kulingana na maeneo waliyoomba kufanya shughuli hizo.
Kampuni
 zilizosainiwa Leseni ni Kampuni ya J.S Construction, inayomilikiwa na 
Bw. Sisti Slyvester Mganga ambaye ameingia ubia Bw. Nakui Chen Kampuni 
hiyo yenye Leseni ML 501/2014 ina eneo la ukubwa wa km 0.29. Aidha, 
shughuli za uchimbaji zitafanyika katika eneo la Kihangaiko Bagamoyo na 
  Madini yatakayozalishwa ni ‘dimension stone’ na kokoto za ujenzi za 
granite.
Vilevile,
 kampuni nyingine iliyowekewa saini ya Leseni ni Osiris Gold (T) Ltd. 
inayomilikiwa na Watanzania Ezekieli Kihali na Shehdaza Walli leseni 
namba ML 513/2014. Madini yatakayozalishwa na Kampuni hii ni dhahabu 
katika eneo la ukubwa wa km 9.94, Rwamgaza Geita
Aidha,
 Mhe. Muhongo ameweka saini leseni ya uchimbaji wa madini aina ya Marble
 kwa Gagan S.Gupta, Sameer S.Gupta na Shailesh B.Bhandari ambao 
wanamiliki Kampuni ya Kamal Steel katika eneo la Kidayi Kilosa. Kampuni 
hii yenye Leseni ML 514/2014 ina eneo la Km 9.52.
Wakati
 akitoa Leseni hizo za uchimbaji, amewakumbusha wamiliki wa leseni 
kuhusu kodi na wajibu wa mwenye leseni katika jamii inayohusika ili 
wananchi na Taifa waweze kufaidika na rasilimali hizo. Uwekaji saini huo
 umefanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Dare s Salaam.
No comments:
Post a Comment