TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 28, 2014

UCHAGUZI 2015 WATANZANIA WATAKIWA KUWA WAANGALIFU KATIKA KUCHAGUA VIONGOZI

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa,Bi Jesca Msambatavangu akizungumza na wakazi wa wilaya ya Mufindi wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa kugombea nafasi ya Udiwani 
 Baadhi ya Wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamejumuika katika kijiji cha cha Kilala Ibumu wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri kwenye kampeni za kugombea udiwani 
Pichani ni Bwa.Hemed Mbena ambaye ndiye mgombea Udiwani katika kijiji cha Kilala Ibumu kupitia chama cha CCM akiwahutubia wakazi wa kijiji hicho,wilayani Mufindi wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa kugombea nafasi ya Udiwani 

========================================================================
Wananchi wametakiwa kuwa makini katika kuchagua viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo na sio bora kiongozi kwa kufuata ushabiki wa vyama.
Hayo yamesemwa na katibu wa CCM wilaya ya Mufindi, MIRAJI MTATURU wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Madiwani katika kijiji cha kilala ibumu kata ya image wilaya ya kilolo.
Mtaturu amesema kuwa wananchi wanapaswa kutumia busara katika kuchagua viongozi na kuangalia chama ambacho kinaweza kuwaletea maendele na sio kuchagua chama ambacho hawajui kimetoka wapi wala hawajui kina malengo gani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa ,JESCA MSAMBATAVANGU amesema kuwa wananchi wanapaswa kuchagua kiongozi anayetoka katika chama cha ccm kwani ndiyo chama pekee kinachoweza kuwaletea maendeleo katika nchi na kutokimbilia chama cha chadema kwa sababu kinachagia kuwapotosha vijana kwa kuleta fujo.
Aidha amewataka wananchi kuiamini CCM na kuipa uongozi huku akiwataka wananchi wa kijiji cha Kilala Ibumu kumchagua HEMEDI MBENA ambaye ndiye mgombea udiwani katika kijiji hicho kupitia chama cha CCM.

No comments:

Post a Comment