Rais
 Jakaya Kikwete  akiteta jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na
 Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiteta jambo na Waziri Mkuu 
mstaafu  Edward Lowasa. 

Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
 akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa 
tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya 
marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya 
ya Bagamoyo. Picha na OMR 

Rais
 Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa 
Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki 
dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake 
Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo. Picha na OMR 

Rais
 Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza
 waombolezaji kuswalia mwili wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, aliyekuwa 
Mbunge wa Chalinze, aliyefariki juzi. Mazishi ya mbunge huyo yamefanyika
 leo kijijini kwao Miono. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
 Bilal, akimfariji mke wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, wakati alipofika
 nyumbani kwa marehemu Miono leo wakati wa shughuli za maziko. Picha na 
OMR 

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiweka udongo kaburini 

Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
 akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, 
kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko 
ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, 
Wilaya ya Bagamoyo. Picha na OMR 

Waombolezaji wakibeba jeneza la Marehemu Ramadhan Bwabamdogo 

Rais
 Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe 
(kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na
 Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati wakiwa katika maziko ya 
aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia 
juzi. Picha na OMR 

Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi katika mazishi hayo 
Waombolezaji mbalimbali wakiswali 
 
No comments:
Post a Comment