JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAFANIKIWA KULIPATA GARI LILILOPORWA KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.
·                  WATU WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KIKONGWE.
·                  WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA  BARABARANI.
·                  WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLIS KWA KUKUTW A NA BHANGI
JESHI
 LA POLISI MKOA WA MBEYA LAFANIKIWA KULIPATA GARI LILILOPORWA NA WATU 
WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI KATIKA TUKIO LA  UNYANG’ANYI WA KUTUMIA 
SILAHA. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 25.01.2014 MAJIRA YA  20:00HRS
 HUKO MAENEO YA  ISYESYE JIJINI MBEYA  AMBAPO OBADIA JONAS {41} 
MFANYABIASHARA  NA MKAZI WA ISYESYE ALINYANGANYWA GARI LAKE LENYE NAMBA 
ZA USAJILI T.675 CLX AINA YA  TOYATA KLUGER. MUHANGA ALIVAMIWA NA KUNDI 
LA WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA GETINI KWAKE AKITOKEA KATIKA BIASHARA ZAKE 
MAENEO YA ILOMBA JIJINI MBEYA, WATU HAO WAKIWA NA SILAHA AINA YA SMG 
PAMOJA NA MAPANGA WALIPIGA RISASI MBILI HEWANI KISHA KUWAAMURU KUSHUKA 
NDANI YA GARI NA KUMJERUHI MUHANGA KATIKA PAJA LA KULIA NA BAADAE 
KUONDOKA NA GARI HILO PAMOJA NA PESA TASLIM AMBAZO THAMANI YAKE BADO 
KUFAHAMIKA. JESHI LA POLISI LILIFANYA JITIHADA ZA MARA MOJA NA 
KUFANIKIWA KULIPATA GARI HILO. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWASAKA 
WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI. MAJERUHI AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA 
RUFAA MBEYA KWA MATIBABU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA 
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI  AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA 
JAMII/WANANCHI  KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  WALIKO WATUHUMIWA HAO 
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA 
ZICHUKULIWE DHIDI YAO. PIA AMEWATAKA WAFANYABIASHARA WAWE MAKINI KATIKA 
KUSAFIRISHA FEDHA TOKA ENEO MOJA KWENDA LINGINE NA NI VYEMA WAWE NA 
USIRI.  

No comments:
Post a Comment