
 Rais
 mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiapishwa rasmi rais wa 
nchi hiyo mjini Antananarivo kufuatia ushindi mkubwa alioupata katika 
uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013.

 Rais
 mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akisani kiapo chake tayari 
kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa Madagascar mbele ya Jaji Mkuu wan
 chi hiyo Jean –Michael Rasolonjatovo (kushoto) wakati wa sherehe za 
kumuapisha rais huyo zilizofanyika mjini Antananarivo.

 Rais
 mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akizungumza na wananchi wa 
Madagascar  waliofurika ndani ya uwanja wa Antananarivo mara baada ya 
kuapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo mjini.

 Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe 
akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumuapisha rais 
mpya wa Madagascar akiwa kwenye jukwaa kuu pamoja na viongozi wengine wa
 nchi za Afrika waliohudhuria sherehe hizo mjini Antananarivo.Wengine 
wanaoonekana kutoka kulia ni Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano, 
Rais wa Zambia Ipikefunye Pohamba na aliyekuwa rais wa Madagascar Andry 
Raojolina.

 Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akikagua gwaride la majeshi ya Madagascar baada ya kuapishwa.CHANZ HAKI NGOWI
No comments:
Post a Comment